Raia wa Pakistan Asma Aziz: Mke aliyenyolewa nywele kwa kutaa kucheza dansi

Picha ya Asma Aziz iliyopatikana kwenye video mtandaoni

Chanzo cha picha, Twitter

Maelezo ya picha, Asma Aziz aliomba msaada kwenye video aliyoweka mtandaoni
Muda wa kusoma: Dakika 2

Mwanamke mmoja raia wa Pakistani amemshutumu mume wake hadharani kwa kumpiga na kumnyoa nywele baada ya kukataa kucheza mbele za mwanaume huyo na rafiki zake, Kesi ambayo imeleta maswali mengi kuhusu usalama wa wanawake nchini humo.

Asma Aziz, kutoka jimbo la Lahore, alisababisha kuzungunzwa kwenye vichwa vya habari vya vyombo mbalimbali baada ya kusambaza video kwenye mitandao ya kijamii akionyesha kichwa chake kilichonyolewa na uso wenye alama zilizotokana na vipigo.

Mume wake, Mian Faisal, na msaidizi wote wanashikiliwa na polisi.Bwana Faisal amekana kumtesa mkewe.

Hatahivyo,tukio hilo limeamsha hisia kali na kutolewa wito kuwa hatua zaidi zichukuliwe ili kukomesha unyanyasaji.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Shirika la Amnesty International limesema mabadiliko ni lazima.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Katika video iliyowekwa tarehe 26 mwezi Machi, bi Aziz alidai kuwa siku mbili zilizopita aliteswa baada ya kukataa kucheza muziki mbele ya marafiki wa muewe ambao walifika nyumbani kwao.

''Alinivua nguo mbele ya wafanyakazi wake.Wafanyakazi walinishika wakati akininyoa nywele na kuzichoma.Nguo zangu zilijaa damu.Nilikua nimefungwa, akatishia kunining'iniza nikiwa mtupu,'' alieleza.

Alisema alipokwenda polisi kufungua mashtaka polisi hawakuonyesha kujali.Lakini polisi walijiteteta kuwa mara tu baada ya Bi Aziz kuripoti askari waliondoka kuelekea kwenye makazi ya mlalamikaji lakini waliikuta nyumba imefungwa na hawakuruhusiwa na mamlaka ya ulinzi wa makazi kuingia eneo hilo

Polisi walichukua hatua baada ya video hiyto kuonwa na naibu waziri wa mambo ya ndani Sheheryar Afridi, ambaye aliamuru mwanamke huyo asikilizwe.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Bwana Faisal na wafanyakazi wake walikamatwa siku iliyofuata.Ripoti ya awali ya daktari imeonyesha majeraha, uvimbe na wekundu kwenye mikono ya bi Aziz na kuzunguka jicho lake la kushoto.

Mawakili wa bi Aziz wamesema kesi hiyo iko chini ya sheria ya kupambana na ugaidi badala ya uhalifu wa kawaida.

Mawakili wamesema kesi hiyo imeleta hali ya mshangao na hofu kwenye jamii.

Bwana Faisal aliwaambia polisi juma lililopita kuwa mke wake alianza kukata nywele akishawishiwa na madawa na kwamba yeye pia alikula madawa, ambayo yalimsaidia kumaliza kazi yake.

Kesi hiyo ilisababisha mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamiii, wengi wakieleza hasira zao kuhusu unyanyasaji nchini Pakistan.

Mcheza filamu na muimbaji Sanam Saeed alikua mmoja kati ya waliozungumzia madhila ya Bi Aziz.

Ruka X ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 3

Haki za wanawake imekua hoja ya miaka mingi sana kwa muda sasa.

Umoja wa Mataifa umeiweka Pakistani kwenye orodha kuwa ya 147 kati ya nchi 188 zenye rekodi mbaya kuhusu masuala ya afya ya wanawake, elimu, siasa na uchumi.

Unyanyaaji dhidi ya wanawake na wasichana bado ni tatizo kubwa .Wanaharakati wanasema takwimu hazionyeshi ukubwa wa tatizo.Matukio mengi hayajaripotiwa.