Siku ya wanawake: Taaluma ya picha kwa wanawake

Wapiga picha Jennifer McCord, Iulia David, Holly-Marie Cato na Amy Shore wanaongoza katika kuwavutia wanawake wengine zaidi kuwa wapiga picha.
Wanawake hao wamekuwa wakiwavutia wanawake wengine katika ujuzi wao wa kupiga picha .
Mpiga picha wa wanamuziki

Chanzo cha picha, Jennifer McCord
Jennifer McCord mwenye umri wa miaka 23, mara nyingi huwa anaonekana juu ya jukwaa akiwa anapiga picha wanamuziki katika ziara zao za muziki.
Msichana huyo alianza kazi yake ya kupiga picha akiwa na umri mdogo kwa kujitolea katika kituo cha kusaidia vijana kupata ujuzi.
"Nilikuwa ninapiga picha katika maonesho manne kwa wiki bila kulipwa kwa mwaka mzima ," McCord alisema.

Chanzo cha picha, Jennifer McCord

Chanzo cha picha, Jennifer McCord
McCord anasema kuwa mitandao ya kijamii inawasaidia kuibua na kukuza vipaji vya wapiga wanawake wanaopiga picha vizuri katika tasnia hiyo.
"Nilipoanza kazi hii, sikuwa ninajua kuwa kuna wapiga picha wa wanamuziki ambao ni wanawake lakini miaka mitano iliyopita mtazamo huo umebadilika sana,"McCord aeleza .
Licha ya kuwa mpiga picha huyo kudai kuwa wanawake wamepenya katika tasnia ya upigaji picha lakini bado wanaume ndio wako wengi zaidi ya wanawake.

Chanzo cha picha, Jennifer McCord
"Jitihada zaidi zinahitajika kutoka kwa wanawake katika wapiga picha wa wanamuziki na wanaokuingia katika kazi hiyo wanahitaji kuungwa mkono na marafiki,familia na tasnia yenyewe,"
McCord alisisitiza.
Mpiga picha wa safari na jamii

Chanzo cha picha, Holly-Marie Cato
"Mimi ni mwanamke mweusi mwenye nywele za asili na kamera mkononi mwangu," anasema Holly-Marie Cato ambaye ni mpiga picha mwanamke mwenye miaka 27.
Yeye anapenda kupiga picha za jamii mtaani na kuziweka katika makala.

Chanzo cha picha, Holly-Marie Cato
Kupitia kazi yake na kujiamini kwake anaamini kuwa anatoa mwanya kwa wanawake wengine kufanya kazi hiyo ya kupiga picha.
"Tunaona wazo la upigaji picha za safari au upigaji picha kwa ujumla linavyoweza kuwavutia watu wengi katika kazi hiyo " Cato alisema.

Chanzo cha picha, Iulia David
Wapiga picha wa urembo
Iulia David's alianza kazi yake ya kupiga picha kwa kuanza kuwapiga picha marafiki zake na baadae akaanza kupata maombi ya watu wengi waliotaka kupigwa picha naye.
Alipoanza kufanya kazi hiyo wengi walimuona kuwa amechanganyikiwa lakini sasa akiwa na umri wa miaka 30, anamiliki studio mbili za upigaji picha huko Birmingham.

Chanzo cha picha, Iulia David
"Ninapenda kupiga picha lakini ninapenda kuzihariri kidogo katika komputa, huwa ninatumia saa mbili kutengeneza picha moja.
Watu wengi huwa wanakuja kwangu ili niwapige picha ambazo zina muonekano mzuri wa ngozi."

Chanzo cha picha, Iulia David

Chanzo cha picha, Iulia David













