Mkenya Eliud Kipchoge atawazwa mwanariadha bora wa dunia kwa mwaka 2018

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkimbiaji wa mbio ndefu kutoka Kenya Eliud Kipchoge ndiye mwanariadha bora wa kiume kwa mwaka 2018.
Kipchoge ametawazwa wadhifa huo mkubwa katika ulimwengu wa michezo katika hafla iliyoandaliwa na shirikisho la riadha duniani, IAAF, usiku wa jana Jumanne huko Monte Carlo, Monaco.
Tuzo hiyo inathibitisha kuwa Kepchoge mwenye miaka 33 ndiye mkimbiaji mbio za masafa marefu bora zaidi wa zama hizi.
Septemba mwaka huu, Kipchoge aliandika rekodi mpya ya mbio za 2018 Berlin Marathon, kwa kukimbia kilomita 42 kwa muda wa saa 2 dakika 1 na sekunde 39, na kuvunja rekodi ya mwenzake wa Kenya Dennis Kimetto aliyeweka rekodi mpya ya dunia ya saa 2, dakika 2 na sekunde 57 aliyokimbia mwaka wa 2014 katika mbio hizo. Hii ilikua ni mara ya tatu kwa Kipchoge kuibuka mshindi kwenye mbio hizo za Berlin marathon.

Chanzo cha picha, Reuters
Kipchoge pia alishinda medali ya dhahabu mwaka 2016 katika mashindano ya Olimpiki yaliyofanyika jijini Rio de Janeiro, Brazil.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameongoza mamia ya Wakenya ambao wametuma ssalamu zao za pongezi kwa Kipchoge baada ya kutuzwa.
Katika salamu zake alizozituma kupitia ukurasa wake wa Twitter, Kenyatta amesema 'utawala' wa Kipchoge kwenye riadha umemfanya bingwa huyo kuingia kwenye vitabu vya kumbukumbu na pia kuhakikisha kuwa Kenya inaendelea kuwa kinara wa riadha duniani.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Naibu Rais William Ruto pia alitumia ukurasa wake wa Twittwer kutuma salamu zake za pongezi kwa Kipchoge.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2

Kwa ujumla, Kipchoge ameshinda mashindano 10 ya marathon kati ya 11 aliyoshiriki toka alipong'oa nanga kwa mara ya kwanza mwaka 2013. Ukiacha Berlin na Rio, pia ameshinda mashindano hayo katika miji ya Chicago, Hamburg, Rotterdam na London.
Kabla ya mbio za marathon Kipchoge alikuwa akikimbia mbio za mita 500 ambapo alishinda medali ya fedha katika michuano ya Olimpiki ya 2004 na medali ya fedha 2008.












