Mkenya Eliud Kipchoge akosa rekodi ya dunia kwa sekunde chache

Mwanariadha wa Kenya, Eliud Kipchoge, amekimbia mbio za masafa marefu, yaani marathoni kwa kasi zaidi duniani lakini hata hivyo akashindwa kuvunja rekodi iliyonuiwa.
Huku akiwa ameandamana na wanariadha wa kumhimiza kuongeza kasi, yaani pacers, alikimbia kilomita 42 kwa muda wa saa mbili na nukta 24.
Shindano hilo lilipangwa na kampuni ya kutengeneza vifaa vya riadha, Nike, na rekodi hiyo haitatambuliwa rasmi na shirika la riadha duniani IAAF.

Shindano hilo lilifanyiwa katika uwanja wa magari ya langalanga Formular One kwa sababu Kipchoge hakukimbia katika mazingira ya kawaida ya marathon.
Licha ya yote Kipchoge alitabasamu kwa kuwa alikuwa amepunguza muda wa kumaliza marathon kwa dakika mbili u nusu.








