Macron aonya kuhusu mipango ya EU kwa vituo vya wahamaiji wa Afrika

macron akiwa Lagos

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Macron amesema Umoja wa Ulaya utashughulikia wahamiaji kutoka Afrika kwa miongo kadhaa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron ameiambia BBC kuwa EU mipango ya kujenga vituo vya kusadia wahamiaji kaskazini mwa afrika haitafanya kazi mpaka pale michakato hiyo iendeshwe na nchi hizo husika.

Akizungumza alipofanya ziara nchini Nigeria, Macron amesema nchi nyingi za Afrika zilikuwa zikipata hofu kuwa vituo hivyo vitakuwa vikiwavuta wahamiaji

Hakuna nchi yeyote afrika iliyokubali kuhodhi vituo hivi

Viongozi wa EU walikubaliana kuwasilisha wazo hili kwenye mkutano mwanzoni mwa mwezi huu.

Macron amesema ulaya itashughulikia wahamiaji kutoka Afrika kwa miongo kadhaa kutokana na changamoto ya ongezeko la watu Afrika

Hatahivyo amesema umoja wa ulaya haiwezi kuchukua maamuzi kwa niaba ya nchi za Afrika

Mpango huu utaweza ''kufanikiwa ikiwa Serikali za Afrika zitaamua kuratibu''.

Macron amesema jambo la kipaumbele ni kuzuia watu kuweka hatarini maisha yao ili kufika ulaya

Viongozi wa EU walikubaliana nini juma lililopita?

Walifikia makubaliano baada ya mazungumzo mjini Brussels, lakini tangu wakati huo wamekuwa wakitofautiana kuhusu namna mpango huo utakavyofanya kazi.Hatua walizokubaliana kuzichukua ni pamoja na:

  • Kuona uwezekano wa kufanya jitihada pamoja kupambana na makundi ya watu yanayofanya biashara ya kusafirisha binaadamu kwa kuwa na mipango ya kuwasajili wahamiaji nje ya
  • kuweka vituo vya wahamiaji katika nchi za ulaya, ingawa hakuna nchi ambayo imejitolea kuweka kituo.Macron amesema Ufaransa haitakuwa na kituo kwa sababu haikuwa nchi ambayo wahamiaji walifikia lakini waziri mkuu wa Italia Giuseppe Conte amesema vituo hivyo vinaweza kuwa popote pale ulaya.
  • Kuboresha mipaka ya nje, na kuongeza rasilimali fedha kwa Uturuki na nchi za Kaskazini mwa Afrika.
  • Kuongeza uwekezaji Afrika kulisaidia bara kuyafikia mabadiliko ya kijamii na kiuchumi hali itakayosaidia watu wasishawishike kuondoka Afrika ili kutafuta maisha bora ulaya.

Awali katika safari yake mjini Lagos, Macron aliwaambia wajasiriamali kuwa nia yake ni kusaidia Afrika kufanikiwa, kuwapatia matumaini mapya vijana wa kiafrika.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Presentational white space

Zaidi ya watu 100 wamezama na wengine 100 wameripotiwa kupotea baada ya boti za wahamiaji kuzama katika matukio mawili tofauti katika kipindi cha juma lililopita, Shirika la kimataifa linaloshughulikia wahamiaji (IOM)

Zaidi ya watu 1,000 wamepoteza maisha wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranea mwaka huu, shirika la IOM limeeleza

Takriban wahamiaji 56,000 wamewasili ulaya mwaka huu idadi tofauti na zaidi ya milioni moja mwaka 2015

chart
The best way to get news on the go

Download the BBC News App.
News imageNews image