Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Jumanne: 'Messi amtaka Kevin de Bruyne Miami'
Inter Miami inapanga kumpa kandarasi kiungo wa kati wa Manchester City na Ubelgiji Kevin de Bruyne, 33, lakini inakabiliwa na ushindani kutoka kwa timu za Saudi Arabia. (Mirror) . Lionel Messi anachezea Klabu hii ambayo ana sehemu ya umiliki.
Tottenham Hotspur haitamsajili mshambuliaji wa RB Leipzig na Ujerumani Timo Werner, 29, kwa uhamisho wa kudumu mara tu mkataba wake wa mkopo utakapokamilika msimu huu wa joto. (Fabrizio Romano)
Chelsea hawana nia tena ya kumsajili mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 26, msimu huu. (CaughtOffside)
Manchester United wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Wolves na Brazil Matheus Cunha, 25, ambaye kifungu cha kuachiliwa kwake cha pauni milioni 62.5 kitaanza kutumika msimu huu. (Talk sport)
Winga wa chini ya miaka 21 wa England Jamie Gittens, 20, anataka kuondoka Borussia Dortmund msimu huu wa joto. Vilabu kadhaa vya Ligi Kuu vinavutiwa naye. (Sky Germany)
Everton na Brighton wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Ipswich na England U21 Liam Delap, 22, ambaye kifungu chake ha kuachiliwa cha pauni milioni 40 kitaanza kutumika iwapo Ipswich itashushwa daraja kutoka Ligi ya Premia. (TeamTalk)
Fiorentina itawezesha kuongeza mwaka mmoja katika kandarasi ya mlinda mlango wa Uhispania David de Gea, 34, na kumbakisha mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United hadi Juni 2026. (Fabrizio Romano)
Leicester City wanatazamia kumtimua meneja Ruud van Nistelrooy baada ya kushindwa mara tisa mfululizo. (Football Insider)
Bayer Leverkusen inavutiwa na mlinda lango wa Brentford na Uholanzi Mark Flekken, 31, huku Bees ikitaka takribani euro 15m (£12.8m). (Sky Germany)
Imetafsiriwa na Lizzy Masinga na kuhaririwa na Ambia Hirsi