Kwanini serikali ya DRC inaikataa ripoti ya Human Rights Watch (HRW)?

Muda wa kusoma: Dakika 4

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imepinga ripoti ya shirika la Human Rights Watch, iliyochapishwa tarehe 20, Januari kuhusu hali ilivyo ya hatari kwa sasa katika eneo la Uvira na Kusini mwa mji wa Kivu.

Katika taarifa yao, Serikali ya DRC ilisisitiza kuwa hali tete ya usalama inatokana na majeshi ya Rwanda (RDF) na waasi wa M23, ila wao wana wajibu wa kuwalinda raia wote eneo hilo.

DRC imekanusha madai yaliyochapishwa katika ripoti ya Human Rights Watch kuhusu usalama wa eneo la Uvira kwa kusema kuwa madai yao hayakuwa ya kweli, na yamechukuliwa nje ya muktadha wa kisheria na kiusalama.

Kulingana na mamlaka, shirika la Human Rights Watch, linahusika na hatari ambazo zimejitokeza baada ya kuondoka kwa majeshi ya RDF na waasi wa M23, bila kuguzia uharibifu uliofanyika kipindi walikuwa wameteka maeneo hayo kabla ya kuondoka.

Serikali ya DRC inasisitiza kuwa kundoka kwa RDF/M23, uliofanyika tarehe 16, January,2026, na ulifuatiwa na wizi, vitisho, na kunyanyaswa kwa jamii hali ambayo iliathiri usalama na umoja wa Uvira. Kuondoka kwa kundi hilo pia kulifuatwa na machafuko yaliyofanywa kimakusudi ilikuendeleza hali ya utovu wa usalama eneo hilo.

Kulingana na serikali ya DRC, wale wanaotishia usalama wa raia ni RDF/M23 kutokana na kuidhibiti mji huo kwa mabavu, na kuwalazimu jamii ya Banyamulenge kukimbia makwao kutokana na hofu na machafuko.

Mamlaka za DRC zinaamini kuwa kuhama kwa watu kuliko shuhudiwa eneo la Uvira, kulichochewa na hofu, na vitisho dhidi ya familia kadhaa, na shinikizo kwa raia. Kulingana na serikali huu ndio ukweli ambao hukusemwa na viongozi wa Banyamulenge.

Wakisisitiza kuhusu jukumu lao la kulinda raia, ikiwemo jamii ya Banyamulenge, serikali ya DRC inasema kuwa hali ya ukosefu wa usalama Uvira kunatokana na Rwanda kuingilia mipaka yake na kuunga mkono kundi la waasi lililoko eneo hilo. DRC inasisitiza kuwa uwepo wa majeshi ya Rwanda eneo hilo na kujiondoa kwao, unakiuka sheria za kimataifa.

DRC pia inasema kuwa, iko tayari kushikirikiana na mashirika ya kimataifa ili mradi uchambuzi utakaofanyika utafuata sheria za kimataiafa na hautapunguza majukumu ya serikali na kufuta ukweli.

Ripoti ya Human Rights Watch inasema nini?

Ripoti ya Human Rights Watch iliyochapishwa Januay 20, inatoa picha ya Maisha ya raia wa Uvira baada ya kuondoka kwa M23.

Kulingana na shirika hilo, kuondoka ghafla kwa kundi la waasi la M23, linaloungwa mkono na Rwanda tarehe 17, Januari, 2026, iliwaacha familia nyingi katika hali ya hatari na mateso, haswa kutoka kwa kundi lililojihami la Wazalendo.

Human Rights Watch inasema kuwa tangu M23 na majeshi ya Rwanda kuchukua udhibiti wa Uvira mwezi Disemba tarehe 10, wakaazi wametishiwa maisha, kunyanyaswa na kushambuliwa.Wakihofia hali hiyo kujirudia tena, familia nyingi kutoka jamii ya Banyamulenge waliondoka eneo la Uvira, baada ya waasi hao kuondoka, huku familia chache tu zikisalia.

Shirika hilo la HRW, linasema jeshi la DRC, lilitumwa eneo la Uvira tareje 18, Januari, ila linaonya kuhusu uwepo wa kundi lililojihami la Wazalendo wanaoungwa mkono na jeshi la Congo la FARDC, ambayo mara nyingi imelaumiwa kwa kuwatesa raia.

Ripoti ya Human Rights Watch iliyochapishwa Januay 20, inatoa picha ya Maisha ya raia wa Uvira baada ya kuondoka kwa M23.

Kulingana na shirika hilo, kuondoka ghafla kwa kundi la waasi la M23, linaloungwa mkono na Rwanda tarehe 17, Januari, 2026, iliwaacha familia nyingi katika hali ya hatari na mateso, haswa kutoka kwa kundi lililojihami la Wazalendo.

Human Rights Watch inasema kuwa tangu M23 na majeshi ya Rwanda kuchukua udhibiti wa Uvira mwezi Disemba tarehe 10, wakazi wametishiwa maisha, kunyanyaswa na kushambuliwa.Wakihofia hali hiyo kujirudia tena, familia nyingi kutoka jamii ya Banyamulenge waliondoka eneo la Uvira, baada ya waasi hao kuondoka, huku familia chache tu zikisalia.

Shirika hilo la HRW, linasema jeshi la DRC, lilitumwa eneo la Uvira tareje 18, Januari, ila linaonya kuhusu uwepo wa kundi lililojihami la Wazalendo wanaoungwa mkono na jeshi la Congo la FARDC, ambayo mara nyingi imelaumiwa kwa kuwatesa raia.

Waziri wa ulinzi wa DRC, tarehe 20 Januari, aliwaambia jamii ya Banyamulenge kuwa, wasilazimishwe kuyahama makazi yao, na wako huru kurejea eneo la uvira.

HRW pia inasema serikali ya DRC ilitangaza kurejesha utawala wa serikali eneo hilo, ikiwemo usalama, mahakama na misaada ya kibinadamu.

HRW pia imetoa wito kwa rais wa DRC Felix Tshisekedi, na mamlaka za Congo, kutangaza wazi kuwa watatoa usalama kwa jamii ya Banyamulenge na raia wengine, na pia kuwaamuru kundi la Wazalendo kuondoka eneo hilo, ili kuzuia unyanyasaji zaidi. Aidha shirika hilo pia linataka serikali na mashirika ya kijamii kuwahakikishia usaidizi wa kifedha raia walioathirika na wizi na uharibifu wa mali uliotokea eneo hilo.

Nini tunachokijua kuhusu kuondoka kwa M23?

Mwezi Disemba 2025, waasi wa M23 waliuteka mji wa Uvira, Kivu Kusini karibu na mpaka wa Burundi, mashariki mwa DRC.

Tarehe 17, Januari 2026, kundi hilo lilitangaza kujiondoa katika mji wa Uvira, wiki moja tu baada ya kuchukua udibiti wake, na kusema kuwa walikuwa wanataka kuunga mchakato wa amani ulioafikiwa Marekani, na pia kuunga mkono mazungumzo ya amani yanayoendelea mjini Doha.

Ila M23 ilesema imeacha mji wa Uvira chini ya jeshi la kudumisha amani la MONUSCO, na kutaka jeshi huru kutumwa eneo hilo ili kulinda raia.