Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumanne: Juventus inawataka nyota hawa wa Liverpool na Man U
Nottingham Forest wametoa ofa ya pauni milioni 35 kumsajili mshambuliaji wa Crystal Palace, Jean-Philippe Mateta, lakini Palace (Eagles) wanataka kifurushi cha pauni milioni 40 na watamruhusu Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 28 kuondoka ikiwa bei hiyo itafikiwa. (Athletic)
Juventus pia wanavutiwa na winga wa Liverpool, Mtaliano, Federico Chiesa, 28, na mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee, 24, ambaye yuko Manchester United . (Gazzetta dello Sport)
Mshambuliaji wa Everton na Guinea-Bissau Beto, 27, ni mojawapo ya chaguo la Juventus wanapotafuta kumsajili mshambuliaji wakati wa dirisha la uhamisho la majira ya baridi. (Gazzetta dello Sport)
Mshambuliaji wa Ufaransa Randal Kolo Muani, 27, yuko Tottenham kwa msimu mzima akitokea Paris St-Germain na ni chaguo jingine ambalo Juventus wanalitazama (Fabrizio Romano)
Kiungo wa kati wa Manchester United Bruno Fernandes anatarajiwa kusubiri hadi mwisho wa msimu kabla ya kuamua kuhusu mustakabali wake, huku mkataba wa sasa wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 ukiendelea hadi 2027 na akiwa na chaguo la kuongeza mwaka mmoja zaidi. (Mirror)
Atletico Madrid wanatarajiwa kufanya mazungumzo na Atalanta kuhusu kumsajili kiungo wa kati wa Brazil mwenye umri wa miaka 26 Ederson. (AS)
Everton wamekataa ofa kutoka Lazio kwa kiungo wa kati wa Uingereza, Tim Iroegbunam mwenye umri wa miaka 22. (Corriere dello Sport)
Beki wa Newcastle United , Mwingereza Jamal Lascelles, 32, ameambiwa anaweza kuondoka klabuni hapo ikiwa mkataba sahihi utapatikana. (Chronicle)
Wolves wamekataa ofa ya pauni milioni 6.9 kutoka Roma kwa ajili ya beki wa kushoto wa Norway mwenye umri wa miaka 23, David Moller Wolfe. (Sky Sports)
Meneja wa zamani wa Southampton na Rangers, Russell Martin ni miongoni mwa wanaotarajiwa kuchukua nafasi ya meneja wa Leicester City kufuatia kufukuzwa kwa Marti Cifuentes. (Football Insider)
Mchezaji wa zamani wa Leicester City, Gary Rowett na meneja wa Hearts, Derek McInnes pia wanafikiriwa na City. (Mail)