Kwa nini wanawake wana uwezekano mkubwa wa kufa katika ajali za magari?

Muda wa kusoma: Dakika 4

Je, vipimo vya usalama wa magari vinazingatia miili ya wanawake? Kwa kweli, kwa miongo kadhaa watengenezaji wa magari wametegemea magari bandia kwa majaribio kupima vipimo vya miili ya wanaume, ambayo inamaanisha kuwa matokeo ya mtihani wa ajali hayaonyeshi kiwango cha hatari ambayo wanawake wanakabili katika ajali za trafiki.

Ripoti ya hivi majuzi iliyotolewa na Utawala wa Kitaifa wa Usalama Barabarani nchini Marekani, iliyochapishwa mapema mwezi huu, ilithibitisha kuwa wanawake wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi kuliko wanaume wanapohusika katika ajali za barabarani.

Tafiti zilizokusanywa kwa miaka mingi zinaonyesha hali inayosumbua ya wanawake kujeruhiwa vibaya zaidi, na hata kuuawa, katika ajali za magari ambazo hazisababishi majeraha sawa kwa wanaume, hatua ilioshinikiza mamlaka rasmi ya trafiki na watafiti kote ulimwenguni kuangazia pengo hili na kujaribu kuelewa sababu zake.

Katika muktadha huu, Idara ya Uchukuzi ya Marekani ilitangaza Novemba mwaka jana kuundwa kwa kifaa cha kwanza cha kupima ajali ya gari kilichoundwa mahsusi kupima kiwango cha usalama cha mwili wa mwanamke katika tukio la ajali ya gari akiwa katika kiti cha dereva, katika hatua ambayo itabadili njia iliopitishwa miongo kadhaa iliyopita, ambayo inategemea zaidi sifa za mwili wa mwanamume.

Gari bandia lililotumika katika majaribio ya usalama wa magari liliidhinishwa mnamo 1978, na liliundwa kulingana na vipimo vya mtu ambaye ana urefu wa sentimita 175 na uzani wa kilo 78.

Mwili bandia wa mwanamke bandia ambao ulitumika katika mtihani wa kike, na ambao kwa sasa uko chini ya maendeleo na majaribio, unaitwa "Thor-05F." Ni mdogo, kwa usahihi zaidi huonyesha tofauti kati ya wanaume na wanawake, ikiwa ni pamoja na shingo, mtulinga, mfupa wa nyonga, na miguu. Pia ina fulana ya mpira ili kuwakilisha matiti na una sensa zaidi ya 150, kulingana na Idara ya Usafiri ya Marekani.

Je, takwimu za ajali zinasemaje?

Takwimu zinaonyesha kuwa wanaume wengi hupoteza maisha kila mwaka katika ajali za magari ikilinganishwa na wanawake. Hii inachangiwa na ukweli kwamba wanaume, kwa wastani, huendesha gari kwa umbali mrefu na huathirika zaidi na mazoea hatari ya kuendesha gari, kama vile kutovaa mikanda ya usalama, kuendesha kwa kasi, na kuendesha gari wakiwa wamekunywa pombe au vitu vingine.

Kwa hiyo, ajali ambazo madereva ni wanaume mara nyingi huwa mbaya zaidi kuliko zile ambazo madereva ni wanawake.

Hata hivyo, tafiti kadhaa zilizofanywa katika miaka ya hivi karibuni zinaonyesha kuwa uwezekano wa wanawake kujeruhiwa au kufa katika ajali zinazofanana za kiwango sawa cha hatari bado ni kubwa kuliko uwezekano wa wanaume kujeruhiwa au kufa katika ajali sawa, hali ambayo inazua maswali kuhusu sababu za tofauti hii.

Utafiti uliofanywa na Utawala wa Kitaifa wa Usalama wa Barabarani nchini Marekani unaonyesha kwamba wanawake wana uwezekano wa asilimia 73 kujeruhiwa katika migongano ya mbele kuliko wanaume, na asilimia 17 wana uwezekano mkubwa wa kufa katika ajali za gari.

Wakati watafiti wengine wanahusisha tofauti hizi na utegemezi wa vipimo vya usalama kwenye magari bandia yaliyoundwa kulingana na vipimo vya miili ya wanaume, wengine wanaamini kuwa aina tofauti za magari yanayoendeshwa na wanaume na wanawake, na mazingira ya ajali yenyewe, inaweza pia kuchangia kuelezea tofauti hii.

Hoja hii inaungwa mkono, kwa kiasi fulani, na matokeo ya utafiti uliofanywa na idara hiyo mwaka 2022, ambao ulihitimisha kuwa pengo la hatari ya vifo kati ya madereva wa kiume na wa kike katika magari ya kisasa limepungua, kutokana na maboresho yaliyofanywa katika muundo wa mifumo ya usalama.

Je, unapima vipi usalama wa gari?

Majaribio ya ajali za magari yameonyesha maendeleo makubwa katika miongo kadhaa iliyopita, katika suala la mbinu na zana zinazotumiwa.

Katika hatua zake za awali, katika miaka ya 1930, 1940 na 1950, watengenezaji wa magari walitumia mbinu zinazochukuliwa kuwa za kushtua hii leo, zikiwemo maiti za binadamu na wanyama, kama vile sokwe, nyani, nguruwe na mbwa. Watu hai waliojitolea pia walishiriki katika majaribio kadhaa ya ajali hizo.

Mnamo 1934, kampuni ya Marekani ya General Motors ilifanya majaribio ya kwanza ya ajali kwa kutumia vizuizi, ikitegemea maiti za wanadamu kusoma athari za ajali kwenye mwili wa binadamu ndani ya gari. Majaribio haya yalichangia uundaji wa vipengele muhimu katika mifumo ya usalama, kama vile dashibodi zenye kinga.

Mili ya binadamu bado hutumiwa, kwa kiasi kidogo, katika baadhi ya utafiti wa ajali za magari ambapo viwango vya maadili vinaruhusu, kwa sababu hutoa data sahihi kuhusu majibu ya viungo vya ndani na tishu za binadamu, vipengele ambavyo miili bandia haiwezi kuiga kikamilifu.

Kinyume chake, watengenezaji wa magari waliacha kutumia wanyama walio hai katika majaribio ya ajali miongo kadhaa iliyopita kutokana na shinikizo la umma, wasiwasi wa maadili, na uaminifu mdogo wa matokeo kwa sababu ya tofauti kubwa za anatomia kati ya wanyama na wanadamu. hatahivyo watengenezaji wengine wakuu waliendelea na mazoezi haya hadi 1993.

Lini tunaweza kutarajia magari salama kwa kila mtu?

Upimaji wa usalama wa gari umekuwa na utata kila wakati. Hata hivyo, mjadala mkubwa zaidi wa kimaadili leo unahusu kufanya magari kuwa salama kwa mamilioni ya wanawake duniani kote, wakati ambapo matatizo yanayohusiana na kutumia wanyama hai au miili ya wafu katika utafiti yamepungua kwa kiasi kikubwa.

Licha ya hatua chanya ya hivi majuzi ya shirikisho nchini Marekani, kupitishwa rasmi na mwisho kwa jaribio jipya la majaribio la wanawake "Thor-05F" katika majaribio ya shirikisho halitarajiwi kabla ya 2027 au 2028.

Hata hivyo, kutekeleza viwango vipya vya watengenezaji magari kunaweza kuchukua muda mrefu zaidi, kwa kuwa baadhi ya watengenezaji na watoa bima wameelezea kutoridhishwa kwao kuhusu ufanisi wa majaribio haya, wakielezea wasiwasi wao kuhusu hatari zinazozidisha au kudhoofisha ufanisi wa mifumo iliyopo ya usalama. Wakati huo huo, watetezi wa mabadiliko wanaendelea kushinikiza mahitaji haya kutekelezwa.

Kuanzishwa kwa mgari bandia mapya kunalenga kuziba pengo la usalama kati ya madereva wa kiume na wa kike, na kusababisha magari salama kwa kila mtu. Swali linabaki: je, ni kweli magari yanakaribia zaidi kutoa ulinzi bora kwa wanawake?