Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kutana na wanasoka bibi vikongwe wanavyotishia soka la Afrika
Huenda wasiwe na ujuzi wa Lionel Messi au Cristiano Ronaldo, lakini hilo haliwazuii bibi vikongwe hawa ama maajuza wa Kiafrika kufanya mazoezi ya kufunga bao na kukaba kwa ustadi.
Rebecca Ntsanwisi mwenye umri wa miaka 57 kutoka Afrika Kusini ameanzisha timu za Soka kwa ajili ya bibi wazee ama Maajuza (Football Grannies) katika bara zima la Afrika katika jitihada za kuboresha afya ya akili na kimwili za wanawake wazee.
Timu tano kutoka Afrika kwa sasa zinashiriki katika mashindano ya Kombe la Dunia la Football Grannies huko Limpopo, zambia ambapo mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi ana zaidi ya miaka 80.