Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tazama: Je, Rais wa Ufaransa amezabwa na kofi au ni mahaba
Kanda ya video inayoonyesha wakati Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kisukumwa usoni na mke wake wakati walipotua uwanja wa ndege wa Hanoi, Huko Vietnam Jumapili jioni imezua gumzo mtandaoni.
Katika kanda hiyo, Brigitte Macron hakuonekana vizuri, lakini mkono wake ulionekana ukimsukuma Macron usoni kwa nguvu.
Macron ambaye mwanzoni alionekana kuchanganikiwa ajituliza haraka na kuwapungia mkono wapiga picha.
Vyanzo vya Ikulu ya Ufaransa vilivyonukuliwa na vyombo vya habari vya Ufaransa vinasema kuwa tukio hilo lilinaswa ''wakati ambapo rais na mke wakoe walikuwa wakitaniana kabla ya kuanza kwa ziara yao", huku Macron akisema "tulikuwa tunafanya utani kama kawaida".