Warusi wanapeleka wanajeshi na silaha zaidi huko Bakhmut. Je, hali ikoje kwenye uwanja wa vita?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mfumo wa salvo wa roketi ya Kirusi wenye roketi za thermobaric

Taasisi ya Utafiti wa Vita (ISW) inasema Warusi walileta mifumo ya silaha ambayo inakisiwa kuwa na nguvu ikifahamika kama thermobaric Sontsepek katika ngome ya mji wa Bakhmut, na wanajeshi wa kawaida wa Urusi wamewasili kuimarisha vikosi vya mamluki kwa jina wagner .

Bakhmut inaendelea kuwa sehemu ya mbele katika vita.

Vyombo vya habari vya Urusi vinaandika tena kwamba Vikosi vya Jeshi la Ukraine vinaondoka mjini ili kuepuka kuzingirwa. Lakini upande wa Ukraine unahakikishia kwamba jeshi bado linashikilia ulinzi katika mji huo na Bakhmut haiko chini ya udhibiti wa Urusi.

Uimarishaji wa Urusi

Kulingana na ISW, vikosi vya Urusi vimekuwa vikitumia silaha aina ya TOS-1A ("Sontsepek") pia mifumo ya silaha za thermobaric katika eneo la Bakhmut. Katika taarifa yao ya kila siku, wataalamu walizingatia sana uchambuzi wa hali katika mji huu mashariki mwa Ukraine.

Kulingana na ISW, mifumo ya silaha za thermobaric ya TOS-1A huenda ilipokelewa na vikosi vya anga vya Urusi, haswa, Idara za 76 na 106 za Walinzi wa Ndege.

Vikosi vya Jeshi la Ukraine havikuweza kuthibitisha habari hii, lakini vilifafanua kuwa data kama hizo zinaweza kupatikana na watalaam kupitia njia za ziada za ufuatiliaji, hasa, picha za setilaiti. Wakati huo huo, uimarishaji wa vikosi vya Urusi huko Bakhmut na askari wa doria kwa kweli unafanyika.

"Warusi wanaimarisha vikosi vyao huko Bakhmut peke yao. PMC "Wagner" ilijaribu kutumia nguvu ya ukiritimba katika mwelekeo huu, hata ilijaribu kuunda vitengo vyao vya hewa na silaha. Hata hivyo, kutokana na hasara kubwa, tumegundua katika wiki za hivi karibuni kwamba wanaimarisha vikosi vyao na vikosi vya jeshi la kawaida la Urusi, ikiwa ni pamoja na wanajeshi wa angani," Serhiy Cherevatyi, msemaji wa Kundi la Vikosi vya Mashariki, aliiambia BBC Ukraine.

Warusi wanasonga mbele

Kulingana na ISW, video za kijiolojia zinathibitisha kuwa wanajeshi wa Urusi wamesonga mbele kaskazini mwa Bakhmut - kaskazini mwa kijiji cha Khromovo, kilomita 2 kutoka mji huo, na kaskazini mashariki mwa Orikhovo-Vasylivka, umbali wa kilomita 11.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Picha nyingine zinaonyesha vikosi vya Ukraine vikisonga mbele kwenye maeneo ya magharibi mwa Novobakhmutivka, kaskazini mwa Avdiivka. Hata hivyo, bado haijulikani ikiwa Vikosi vya Jeshi la Ukraine vinashikilia nafasi ya ukubwa upi katika maeneo haya.

Vyombo vya habari vya Urusi hatahivyo vinaandika kwamba wanajeshi wa Ukraine wanaondoka katika mji huo ili kuepuka kuzingirwa. Wanaripoti kuwa mamluki wa PMC Wagner walitekanyara jengo la shule magharibi mwa uwanja wa Metalurh katikati mwa Bakhmut.

Upande wa Ukraine unatoa maoni machache tu juu ya hali ya Bakhmut kwa muda mfupi, bila maelezo zaidi. Maoni ya Wizara ya Ulinzi yanashiria mambo kadha wa kadha - hali katika mji huo ni ngumu, Vikosi vya Jeshi la Ukraine vinavyoshikilia maeneo, vinahitaji silaha zaidi za Magharibi.

Wakati wa ziara ya Warsaw mnamo Aprili 5, Volodymyr Zelenskyy alipendekeza uwezekano wa kuondoka Bakhmut ili kuepuka kuzingirwa. Walakini, hadi sasa, amri kutoka Ukraine ni kuwa inaamini kwa uwezekano wa kujiondoa bado.

"Bila shaka, ikiwa kuna wakati wa matukio ya hatari zaidi na tukiona tunaweza kupoteza wafanyakazi kwa sababu ya mazingira, bila shaka, maamuzi sahihi ya Jenerali (Kamanda wa Vikosi vya Ardhini vya Jeshi la Ukraine Oleksandr Syrsky) yatakuwa sahihi. - .) papo hapo. Nina uhakika na hili," alisema, akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu uwezekano wa kuondoa wanajeshi wa Ukraine kutoka Bakhmut iwapo watazidiwa nguvu.

Zelensky alisisitiza kwamba jambo kuu ni kuhifadhi jeshi la Ukraine.

Jinsi silaha za aina ya thermobaric zinavyofanya kazi

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jeshi la Marekani lilitumia mabomu ya thermobaric dhidi ya al-Qaeda nchini Afghanistan

Jeshi la Ukraine limekuwa likiripoti mara kwa mara uharibifu wa mifumo mizito ya silaha za nzito za Warusi. Mnamo Februari, Wafanyakazi Wakuu waliripoti kwamba tangu kuanza kwa uvamizi kamili, Vikosi vya Jeshi la Ukraine vilikuwa vimeharibu mifumo 9 ya TOS-1 "Pinocchio" na TOS-1A "Sontsepek".

Wizara ya Ulinzi ya Urusi haifichi ukweli kwamba inatumia mifumo hii katika vita dhidi ya Ukraine. Walijigamba mara kwa mara juu ya nguvu na ufanisi wa mifumo ya moto na kusisitiza kwamba Vikosi vya Jeshi la Ukraine vimepanga "uwindaji makhsusi " wa silaha hizi.

Sontsepek ni mfumo wa ngazi ya kijeshi lakini matumizi yake, kulingana na shirika la watalamu wa vita (ISW), hayatawapatia wanajeshi wa Urusi faida kubwa.

Silaha za thermobaric, pia hujulikana kama mabomu ya utupu au vilipuzi vya hewa ya mafuta, zinajumuisha kontena lenye tenki mbili tofauti za mlipuko.

Inaweza kurushwa kama roketi au kudondoshwa kutoka kwenye ndege kama bomu. Wakati wa kulenga shabaha , hatua ya kwanza ya mabomu hayo hufungua chombo na kutawanya moto kama vile mfumo wa wingu.

Wingu hili la moto linaweza kupenya sehemu yoyote kwa mfano majengo au ng'ome ambazo hazijadhibitiwa kabisa . Mbinu ya pili ni kulipua wingu hilo la moto , na kusababisha moto mkubwa, na kuwa wimbi kubwa la mlipuko, hivyo basi kufyonzwa hewa yote ya oksijeni inayozingira eneo hilo .

Pia wanaweza kushambulia malengo mbalimbali na yanayokuja kwa ukubwa tofauti, kama vile mabomu ya kurusha kwa mkono(GRENEDI) na vifaa vya kurusha roketi vinavyoshikiliwa kwa mkono ambavyo askari wanaweza kutumia.

Urusi ilitumia zana hizi katika vita vya Chechnya mwaka 1999 na kulaaniwa na shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch .