Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi

Bandera y escudo de Ucrania

Chanzo cha picha, Getty Images

Mzozo ambao umekuwa kati ya Urusi na Ukraine kwa miaka minane iliyopita unaendelea kuweka mashakani sio tu raia wao bali pia jumuiya ya kimataifa.

Kama mataifa mengine jirani, nchi hizi mbili zina historia inayoziunganisha kuliko vile inaweza kuzitenganisha.

Ilianzia karne ya 9 wakati Kiev, mji mkuu wa sasa wa Ukraine, ulikuwa kitovu cha jimbo la kwanza la Slavic, lililoundwa na kikundi cha Waskandinavia waliojiita Rus.

Jimbo hilo kuu la enzi za kati, ambalo wanahistoria wanaliita Kyvan Rus, lilikuwa chimbuko la Ukraine na Urusi.

Moscow ilianzishwa katika karne ya 12, kwenye ule uliokuwa mpaka mrefu wa kaskazini-mashariki.

Imani iliyodai ilikuwa ya Orthodox Christian, iliyokubaliwa mwaka 988 na Vladimir I wa Kiev au Mtakatifu Vladimir Svyatoslavich "The Great", ambaye aliunganisha ufalme wa Rus kutoka Belarus ya sasa, Urusi na Ukraine hadi Bahari ya Baltic.

Kutoka kwa idadi kubwa ya lahaja za Slavic Mashariki zilizozungumzwa katika eneo hilo, lugha za Kiukreni, Kibelarusi na Kirusi hatimaye zilikuzwa.

Ramani ya Ruscelli ya Urusi, Muscovy na Ukraine, 1574.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ramani ya Ruscelli ya Urusi, Muscovy na Ukraine, 1574.

Historia hiyo inayoingiliana inaonekana kuthibitisha kauli ya Rais wa Urusi Vladimir Putin, ambaye hivi karibuni alitangaza kwamba "Warusi na Waukraine ni watu wamoja."

Urusi yaishambulia Ukraine: Mengi zaidi

Lakini wataalam wanasema kwamba, licha ya asili hii moja, wakati wa karne tisa zilizopita uzoefu wa Waukraine umekuwa tofauti, kwani hatima yao iliamriwa na mamlaka tofauti ambazo ziliigawanya nchi.

Fumbo

Rompecabezas de la bandera de Ucrania

Chanzo cha picha, Getty Images

Katikati ya karne ya 13, shirikisho la Rus lilishindwa na Milki ya Mongol.

Mwishoni mwa karne ya 14, kwa kutumia fursa ya kupungua kwa nguvu ya Mongol, Utawala Mkuu wa Moscow na Grand Duchy ya Lithuania (ambayo baadaye ilijiunga na Poland) iligawanya ardhi ya Urusi ya zamani.

Wakazi wake wengi si Waorthodoksi wa Urusi, bali ni wa Kanisa la Umoja au Makanisa Katoliki ya Mashariki, ambayo hufanya ibada yake kwa Kiukreni na kumtambua Papa kama mkuu wake wa kidini.

Sehemu nyingine ya Ukraine ya leo yenye historia tofauti sana ni Crimea, yenye mahusiano yake ya Kigiriki na Kitatari, pamoja na vipindi chini ya utawala wa Ottoman na Urusi.

Pwani mbili

Moonlit Night on the Dnieper by Arkhip Kuindzhi, 1882
Maelezo ya picha, Usiku wa Mwezi kwenye Dnieper na Arkhip Kuindzhi, 1882

Katika karne ya 17, vita kati ya Jumuiya ya Madola ya Poland-Lithuania na Tsardom ya Urusi ilileta ardhi ya mashariki ya Mto Dnieper chini ya udhibiti wa Kifalme wa Urusi. Mkoa huo ulijulikana kama "Left Bank" Ukraine

Katika karne hiyo hiyo, jimbo la Cossack la Kiukreni lilikuwepo katika maeneo ya kati na kaskazini-magharibi ya Ukraine ya leo, lakini mnamo 1764, kiongozi wa Urusi Catherine the Great aliikomesha, na akaendelea kupata maeneo makubwa ya ardhi ya Kiukreni ambayo yalithibitiwa na Poland.

Katika miaka iliyofuata, sera iliyojulikana kama Russification ilipiga marufuku matumizi na kusoma lugha ya Kiukreni, na watu walilazimishwa kubadili imani ya Othodoksi ya Kirusi, ili kuunganisha moja ya "makabila madogo" ya watu wa Urusi. .

Wakati huo huo, uzalendo ulikita mizizi katika nchi za magharibi zaidi, ambazo zilitoka kutoka Poland hadi Milki ya Austria, ambapo wengi walianza kujiita 'WaUkraine' ili kujitofautisha na Warusi.

Lakini pamoja na karne ya 20 yalikuja mapinduzi ya Urusi na kuundwa kwa Umoja wa Kisovieti, ambao ulifanya upangaji wake upya wa fumbo la Ukraine.

Kuchukuliwa na USSR

Rompecabezas banderas rusa y ucraniana

Chanzo cha picha, Getty Images

Ukraine Magharibi hatimaye ilichukuliwa na kiongozi wa Soviet Joseph Stalin kutoka Poland mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia.

Crimea ilihamishwa na Moscow hadi Jamhuri ya Ukraine ndani ya USSR katika miaka ya 1950, lakini inahifadhi uhusiano mkubwa na Urusi, iliyoonyeshwa na Meli katika Bahari Nyeusi huko Sevastopol.

Na serikali ya Kisovyeti iliifunga Ukraine zaidi kuliko awali kwa ushawishi wa Urusi, mara nyingi kwa gharama kubwa.

Mamilioni ya Waukraine ambao tayari walikuwa sehemu ya USSR katika miaka ya 1930 walikufa katika njaa iliyochochewa na Stalin ili kuwalazimisha wakulima kujiunga na mashamba ya pamoja.

Baadaye Stalin aliingiza idadi kubwa ya raia wa Sovieti, wengi bila uwezo wa kuzungumza Kiukreni na wenye uhusiano mdogo na eneo hilo, kusaidia kujaza watu tena mashariki.

Ingawa Kirusi kilikuwa lugha kuu, watoto katika shule ya msingi walijifunza Kiukreni, vitabu vingi vilichapishwa katika lugha hiyo, na katika nusu ya pili ya karne ya 20, "harakati yenye nguvu ya kitaifa ya Kiukreni ilikua katika Muungano wa Sovieti wa watu ambao walikuwa na Elimu ya Kiukreni.

Makosa makubwa

Kiev ya zamani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kiev ya zamani... yenye maana tofauti.

Mnamo 1991 Muungano wa Sovieti ulianguka, na mnamo 1997, mkataba kati ya Urusi na Ukraine ulithibitisha uadilifu wa mipaka ya Ukraine.

Lakini urithi tofauti katika mikoa tofauti ya nchi umeacha dosari ambazo mara nyingi huonekana kama pengo.

Kuna tofauti katika kila upande wa Mto Dnieper, unaofahamika na urefu wa utawala wa Kirusi.

Kwa upande wa mashariki, mahusiano na Moscow yana nguvu zaidi, na wakazi wake huwa wa Orthodox zaidi na kuzungumza Kirusi.

Eneo la Magharibi, karne kadhaa chini ya utawala wa serikali za Ulaya, kama vile Poland na Milki ya Austria na Hungary, huwafanya wakaazi wake kuwa Wakatoliki zaidi na kuzungumza lugha yao wenyewe.

Kila mtu huota ndoto yake mwenyewe, wengine wanatamani kurudi kwenye kile wanachokiona kama nchi yao ya asili huku wengine wanatamani kufuata mkonndo huru wa maisha.