Urusi yashambulia miji muhimu ya Ukraine huku uvamizi ukizidi

Wanajeshi wa Urusi wameuvamia mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine.

Moja kwa moja

  1. Tumefika tamati ya matangazo yetu ya moja kwa moja mpaka kesho panapo majaaliwa

  2. Uvamizi wa Ukraine: Vikosi vya Urusi vyadai kuteka mji muhimu wa bandari

    Ukraine

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine uliathiri vibaya raia siku ya Jumatano huku vitongoji vya makazi vikishambuliwa kwa mabomu na miji mikuu ikizingirwa.

    Jeshi la Urusi lilidai kuwa linadhibiti Kherson, mji muhimu wa kimkakati wa bandari karibu na Crimea.

    Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliwataja watu wake kuwa "ishara ya kutoshindwa".

    Jiji la Mariupol, kusini mashariki, imeshambuliwa kwa makombora leo Jumatano, naibu meya wake Sergiy Orlov aliambia BBC.

    "Hali ya Mariupol ni mbaya, tunakaribia kukumbwa na janga la kibinadamu. Tumeshuhudia zaidi ya saa 15 za mashambulizi ya makombora bila kusitishwa," alisema.

    "Jeshi la Urusi linafanyia kazi silaha zake zote hapa - mizinga, mifumo mingi ya kurusha roketi, ndege, roketi za mbinu. Wanajaribu kuharibu jiji."

    Jingo lililoporomoka

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Bw Orlov alisema vikosi vya Urusi viko kilomita kadhaa kutoka mji kwa pande zote, na mashambulio dhidi ya miundombinu muhimu yamekatiza huduma za maji na usambazaji wa umeme katika maeneo ya jiji.

    "Hatuwezi kukadiria idadi ya wahasiriwa huko, lakini tunaamini angalau mamia ya watu wamekufa. Hatuwezi kuingia kuchukua miili," alisema. "Baba yangu anaishi huko, sina uwezo wa kumfikia, sijui yuko hai au amekufa."

    Huduma za dharura za Ukraine zilisema zaidi ya raia 2,000 wameuawa kufikia sasa katika uvamizi wa Urusi, ingawa BBC haikuweza kuthibitisha idadi hiyo. Umoja wa Mataifa ulisema Jumanne kwamba takriban raia 136 wameuawa, ikifikiri kwamba inakadiria kwamba idadi halisi ya watu waliouawa ni kubwa zaidi.

    Rais Zelensky awali alisema kwamba Urusi inajaribu "kufuta" historia ya nchi yake.

    • Urusi na Ukraine: Hujui kinachokuja - Joe Biden amwambia Putin
    • Mzozo wa Ukraine: Mambo matano ambayo hukujua kuhusu uvamizi wa Urusi huko Ukraine
  3. Uvamizi wa Ukraine: Mazungumzo ya amani kurejelewa- Urusi yaripoti

    Wajumbe walifanya mazungumzo katika eneo la Gomel la Belarus siku ya Jumatatu

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Wajumbe walifanya mazungumzo katika eneo la Gomel nchini Belarus siku ya Jumatatu.

    Mazungumzo ya amani kati ya Urusi na Uraine yanatarajiwa kurejelewa Jumatano jioni, kulingana na shirika la habari la Urusi Tass.

    "Ujumbe wetu utakuwa tayari kuendelea na mazungumzo," msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amesema.

    Inafuatia duru ya kwanza ya mazungumzo katika mpaka wa Urusi na Belarus, ambayo hayakufikia azimio lolote

    Msaidizi wa Rais Vladimir Putin Vladimir Medinsky kwa mara nyingine tena atakuwa mpatanishi mkuu wa Urusi, ripoti zinasema.

    "Nadhani mambo yatasalia yalivyokuwa. Hakuna kitakachobadilika. Tutashikilia msimamo wetu. Watu wale wale wanaohusika," mshauri wa rais Olexiy Arestovych aliiambia Suspilne TV.

    Haijabainika mazungumzo hayo yatafanyika wapi.

    • Urusi na Ukraine: Hujui kinachokuja - Joe Biden amwambia Putin
    • Mzozo wa Ukraine: Mambo matano ambayo hukujua kuhusu uvamizi wa Urusi huko Ukraine
    • Papa Francis ataka kwaresma hii ianze kwa kuiombea Ukraine

      m

      Leo hii mamilioni ya wakristo wanaadhimisha siku ya Jumatano ya majivu ambapo wanaanza kwa kupaka majivu.

      Mwaka huu kwaresima imeanza Jumatano ya tarehe 2 Machi na itamalizika Alhamisi ya Aprili 14.

      Siku ya majivu ni siku takatifu kwa baadhi ya wakristo na makanisa huwa yana misa maalum kuadhimisha Jumatano hii ya majivu, Ikiwa ni ishara kuwa tulitoka majivuni na tunarudi majivuni.

      Kwaresima ni kipindi cha majuma sita (siku 40 bila kujumuisha Jumapili) kuelekea Pasaka, hii ni sikukuu muhimu zaidi katika kalenda ya Kikristo.

      Wakristo hutumia siku hizo 40 za kwaresma kwa kufunga, kusali , kutubu na kufanya matendo mema.

      Wakatoliki na baadhi ya makanisa ya kiprotestanti huadhimisha siku hii.

      Aidha, Mwaka huu Papa Francis ametoa wito kwa kutuma ujumbe kwenye kurasa yake ya twitter kuwa watu wasali kwa pamoja na kufunga kwa ajili ya kuiombea amani Ukraine.

    • Kenya: Wasioamini kuwa kuna Mungu wataka kupiga marufuku siku za maombi shuleni

      Wasioamini Mungu Kenya wasema wanaamini katika kuhoji mawazo

      Chanzo cha picha, Getty Images

      Maelezo ya picha, Wasioamini Mungu Kenya wasema wanaamini katika kuhoji mawazo

      Chama cha wasioamini kuwa kuna Mungu nchini Kenya kimeiandikia barua wizara ya elimu kutaka kupigwa marufuku kwa siku za maombi katika shule za umma kabla ya mitihani ya kitaifa.

      Kundi hilo linasema siku za maombi ni kinyume cha haki za wanafunzi.

      Shule za umma zina utamaduni wa kuandaa siku za maombi kabla ya wanafunzi kufanya mitihani ya kitaifa.

      Shule zimewaita wazazi wiki hii kujumuika katika utamaduni huo ili kuombea kipindi kizuri cha mitihani.

      “Wakenya wengi wamepitia mfumo wa elimu ambapo uzingatiaji wa wa desturi za kidini ulikuwa wa lazima," chama cha wasioamini kuwa kuna Mungu kiliandika.

      Kundi hilo linasema watoto wanapaswa kuachwa wafanye maamuzi yao wenyewe bila upendeleo kuhusu dini.

      Pia unaweza kusoma:

      • Illuminati ilianzaje? na ni kwanini kuna mvuto kuhusu wafuasi wake?
      • Wasioamini Mungu yupo walalamika Kenya
      • Vitisho wanavyopokea Wasomali wasioamini kwamba Mungu yuko
      • Wasioamini Mungu yupo wadai kubaguliwa Kenya
    • Habari za hivi punde, Uvamizi wa Ukraine: Zaidi ya raia 2,000 wameuawa Ukraine - ripoti

      Mamlaka nchini Ukraine zinasema kuwa zaidi ya raia 2,000 wameuawa kufikia sasa katika uvamizi wa Urusi, ambao ulianza karibu wiki moja iliopita.

      Waokoaji 10 pia wameuawa, Huduma ya Dharura ilisema.

      Waokoaji wamezima moto zaidi ya 400 uliozuka baada ya makombora ya Urusi kote nchini na kuzima vilipuzi 416.

      "Kufuatia siku saba za vita, Urusi imeharibu mamia ya vituo vya usafiri, majengo ya makazi, hospitali na shule za chekechea," ilisema.

    • Maisha chini ya utawala wa Urusi

      mm

      Niliamka asubuhi ya leo katika nyumba yetu ya chini na kumuona Liana ambaye kwa hakika ni jirani yetu mpya.

      Kwa muda wa siku saba mchana na usiku aliniambia, "Sipaswi kuwa na huzuni, lazima niwe na nguvu."

      Asubuhi ya leo nilikutana naye katika chumba chenye giza chini ya ardhi katika mafuriko ya machozi. Alisikia kutoka kwa baba yake anayeishi nyumbani kwao kaskazini, karibu na mpaka wa Belarusi.

      Wanajeshi wanane wa Kirusi walikuwa wameingia nyumbani mwao, wakitafuta sigara na kuwachukua mateka kwa ufanisi, wakiwaambia: "Usiende juu, usishuke chini, usisogee."

      Mwingine alifanikiwa kutorokea bafuni kumpa ujumbe wa kunong'ona wa kusema "tumezingirwa".

      Liana alishindwa kuyazuia machozi yake.

      Anaogopa kwamba baba yake sasa amechukuliwa mateka.

      m
      m
    • 'Putin sio Urusi - Navalny atoa wito wa maandamano ya kila siku

      Navalny, kama alivyopigwa picha mwaka 2020

      Chanzo cha picha, Reuters

      Maelezo ya picha, Navalny, kama alivyopigwa picha mwaka 2020

      Kiongozi wa upinzani wa Urusi aliyefungwa jela, Alexei Navalny amechapisha jumbe kwenye mtandao wa Twitter wenye maneno makali akitoa wito wa kufanyika kwa maandamano ya kila siku nchini Urusi na kwingineko.

      Navalny amekaa mwaka mmoja gerezani baada ya kunusurika shambulio la sumu ambalo anailaumu Ikulu ya Kremlin.

      Mwezi uliopita alifunguliwa mashtaka mapya ambayo yanaweza kuchangia kifungo chake kuongezwa kwa zaidi ya muongo mmoja.

      "Sisi - Warusi - tunataka kuwa na taifa la amani. Lakini huenda ni watu wachache wanaweza kutuita hivyo sasa," ameandika kutoka gereza lenye ulinzi mkali mashariki mwa Moscow ambako amefungwa.

      Lakini Warusi wanapaswa "angalau wasiwe taifa la watu wasio na hofu" ambao "wanajifanya kuwa hawatambui vita".

      "Ni muongo wa tatu wa Karne ya 21, na tunatazama habari kuhusu watu wanaochomeka kwa mabomu, nyumba zinapigwa mabomu," anasema.

      "Tunatazama vitisho vya kweli vya kuanzisha vita vya nyuklia kwenye TV zetu."

      Ruka X ujumbe
      Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

      Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

      Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

      Mwisho wa X ujumbe

      • Navalny: Maelfu waandamana kupinga kufungwa kwa mpinzani wa Putin
      • Alexei Navalny: Kiongozi wa upinzani na mkosoaji mkuu wa rais Vladimir Putin wa Urusi apata fahamu
    • 'Watatushambulia hadi tubaki majivu'

      m

      Chanzo cha picha, Reuters

      Watu waliopo Kharkiv wameomba msaada wa kimataifa kusaidia kuizuia Urusi kushambulia kaskazini mashariki mwa mji huo.

      Glib Mazepa ambaye anaishi katikati ya jiji hilo anataka Nato kuzuia ndege kuruka kwenye anga ya Ukraine.

      "Tafadhali funga anga kuzuia makombora ya Kirusi na ndege za Kirusi. Kwa sababu Urusi itashambulia mji wote ubaki majivu."

      Mamlaka nchini humo zinasema kuwa watu wanne wameuawa katika mashambulizi ya makombora ya Urusi asubuhi ya leo.

      Mazepa anasema kulikuwa na "mlipuko mkubwa" majira ya usiku kutoka kwa ndege ambayo ilizunguka mara tatu kabla ya kurusha mabomu manne, karibu kilomita 1 (maili 0.6) kutoka nyumbani kwake.

      Alisema nyumba mbili za makazi ziligongwa karibu na kituo cha metro cha Botanichnyi. Na alielezea wakati aliposikia shambulio la jana la roketi kwenye Uwanja wa Uhuru wa Kharkiv. "Kulikuwa na sauti ya mluzi juu ya vichwa vyetu ... kisha boom.

      • Urusi na Ukraine: Hujui kinachokuja - Joe Biden amwambia Putin
      • Mzozo wa Ukraine: Mambo matano ambayo hukujua kuhusu uvamizi wa Urusi huko Ukraine
    • 'Watoto wangu wako Ukraine, siwezi kubaki Zanzibar',

      m

      Baadhi ya raia wa Ukraine wamekwama Zanzibar na wanashindwa kurudi kwao ili kuzisaidia familia zao.

      Julia anasema anajisikia vibaya sana kwasababu watoto wake wako Ukraine, na alikuja Zanzibar kwa ajili ya mapumziko yeye na mume wake.

      Hivyo ni lazima arudi nyumbani kwao.

      "Warusi wanawaua marafiki zetu na familia zetu najisikia vibaya kwa sababu niko hapa wakati huu.

      Tumenunua tiketi mpya ya ndege tunataka kwenda nyumbani tutapitia Quatar kisha Romani.

      Na baada ya hapo sijui tutaendaje kufika Ukraine ila tutajua tu.

      Najisikia vibaya sana nilipopata taarifa za vita kuanza nilitaka kurudi nyumbani haraka nataka kukutana na familia yangu na ndugu zangu."

      mm

      Vilata mwenye umri wa miaka 25 natoka Ukraine na yuko Zanzibar, anasema kinachotokea nchini kwake ni kibaya sana.

      Anaishi Khakiv,mji ambao umeshambuliwa leo.

      Anasema ana hofu juu ya marafiki zake kwemye mahandaki na kwenye vituo vya mabasi kila siku.

      "Warusi wanawashambulia waukraine kwa mabomu sio utani hali ni mbaya nchini Ukraine".

      Mimi na marafiki zangu tulisema tuje kutembea zanzibar ila kinachotoke nyumbani najisikia vibaya najisikia kulia ...kila wakati ila siwezi sababu haita saidia marafiki zangu na familia yangu lazima nijikaze kwaajili yao."

      • Urusi na Ukraine: Zanzibar inashirikiana na ubalozi wa Ukraine kuwasafirisha watalii wake
    • 'Tafadhali Nato, funga anga ya Ukraine'

      Maafa yanayoendelea kushuhudiwa Ukraine

      Chanzo cha picha, Reuters

      Maelezo ya picha, Maafa yanayoendelea kushuhudiwa Ukraine

      Watu wanaoishi katika mji wa kaskazini-mashariki wa Kharkiv wameiambia BBC jinsi inavyokuwa kuishi chini ya mashambulizi ya anga yanayotekelezwa na Urusi.

      Glib Mazepas, ambaye anaishi katikati ya jiji katika mji wa pili wa Ukraine, anasema kumeshudiwa "mlipuko mkubwa" usiku kucha kutoka kwa ndege iliyozunguka mara tatu kabla ya kushambulia kilomita 1 (maili 0.6) kutoka nyumbani kwake.

      Pia alielezea wakati aliposikia shambulio la jana la roketi kwenye Uwanja wa Uhuru wa Kharkiv "Kulikuwa na sauti ya mluzi" iliyosikika ... kisha mlipuko ukafuata. Nakumbuka nyumba yetu haikuwa ikitikisika sana kutoka kushoto kwenda kulia, kwa takriban sekunde tano. likuwa ni hisia ya ajabu sana."

      Anasema kila kelele anazosikia sasa anafikiri inawezekana ilikuwa ni Urusi imefanya mashambulizi.

      "Jana mke wangu alikuwa akipasha moto kitu kwa kutumia ‘microwave’. Na nilishangaa kwa sababu nilifikiri ni aina fulani ya mashambulizi."

      "Unazoea vita haraka sana, niamini. Ni suala la siku moja au mbili. Sikuwahi kufikiria kuwa itakuwa hivi."

      Mazepas anasema anashukuru kwa uungwaji mkono wa kimataifa, lakini anataka Nato iende mbali zaidi kwa kutekeleza ukanda wa kutoruka ndege nchini Ukraine.

      "Tafadhali funga anga kwa sababu ya makombora ya Kirusi na ndege za kivita za Kirusi. Kwa sababu watapiga tu bomu jiji lote kwenye majivu."

      Soma zaidi:

      • Fahamu mataifa 9 yenye uwezo mkubwa wa silaha hatari za nyuklia duniani
      • Uvamizi wa Ukraine: Warusi wahisi makali ya vikwazo
    • Ukraine yadai kuwauwa wanajeshi 5,840 wa Urusi

      Vikosi vya kijeshi vya Ukraine vimesema takwimu za awali zinaonesha vikosi vya kijeshi vya Urusi vimepata hasara kubwa tangu mwanzo wa uvamizi huo.

      BBC haiwezi kuthibitisha madai haya kwa kina, lakini wizara ya ulinzi ya Uingereza inaamini kwamba vikosi vya Moscow vimepata hasara kubwa wakati wa uvamizi wake nchini Ukraine.

      Jumla ya hasara ya Urusi inayodaiwa na Ukraine kufikia sasa ni pamoja na: Wanajeshi 5,840

      - Ndege 30

      -Helikopta 31

      -Mizinga 211

      -Magari 862 ya kivita (APVs)

      - Tangi 60 za mafuta

      -Magari 355

      -Roketi 40 za MLRS (zilizokamatwa)

      Soma zaidi:

      • Ukraine na Urusi: Je Vacuum au thermobaric ni bomu la aina gani?
    • Urusi yadai kuudhibiti mji wa Kherson

      Ukraine

      Chanzo cha picha, Getty Images

      Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema wanajeshi wake sasa wameuteka mji wa kusini mwa Ukraine wa Kherson.

      Ikiwa mji huo umedhibitiwa na Urusi, utakuwa mjini mkubwa zaidi nchini Ukraine kudhibitiwa na vikosi vya Urusi hadi sasa.

      Usiku wa kuamkia leo tuliripoti kuwa wanajeshi wa Urusi walionekana katika mitaa ya mji huo na kwamba meya wake alisema kituo cha treni cha Kherson na bandari vimetekwa.

    • Rais wa Nigeria kuzuru Uingereza kwa uchunguzi wa kimatibabu

      Muhammadu Buhari amekosolewa kwa kutafuta matibabu nje ya nchi

      Chanzo cha picha, AFP

      Maelezo ya picha, Muhammadu Buhari amekosolewa kwa kutafuta matibabu nje ya nchi

      Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari anatarajiwa kusafiri hadi London kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake kwa takriban wiki mbili, vyombo vya habari vya nchini vinaripoti.

      Rais amekosolewa kwa kukosa kukabidhi mamlaka kwa naibu wake kwa muda ambao hatakuepo kama inavyotarajiwa kikatiba.

      Bw Buhari pia amekosolewa vikali kwa kutafuta matibabu nje ya nchi huku mfumo wa afya wa Nigeria ukikumbwa na usimamizi mbovu.

      Rais wa Nigeria aliwasili nchini Kenya siku ya Jumanne kuhudhuria Bunge la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEA) kuadhimisha miaka 50 ya Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa.

      Anatarajiwa kuondoka Kenya na kuelekea London moja kwa moja.

    • Mtu mmoja afariki dunia baada ya kunywa kafeni sawa na vikombe 200 vya kahawa

      Mwanaume afariki dunia baada ya kuzidisha kafeini ya kahawa

      Chanzo cha picha, Getty Images

      Maelezo ya picha, Afariki dunia baada ya kuzidisha kafeini ya kahawa

      Mkufunzi wa kibinafsi amefariki dunia baada ya kunywa kafeini ambayo ni sawa na vikombe 200 vya kahawa, uchunguzi umeeleza.

      Baba wa watoto wawili Tom Mansfield alikuwa ametumia kimakosa kiasi cha unga alichotakiwa kutumia kwenye mizani ya jikoni.

      Uchunguzi huko Ruthin umebaini kwamba kijana mwenye umri wa miaka 29 kutoka Colwyn Bay aliugua moja kwa moja baada ya kunywa mchanganyiko huo tarehe 5 Januari 2021.

      Akifikia hitimisho la tukio hilo lisilo la kawaida, daktari wa John Gittins alisema chanzo cha kifo kilikuwa sumu ya kafeini.

      Kafeini hutumiwa na baadhi ya washiriki wa mazoezi ya viungo, huku tovuti zingine za mazoezi ya mwili zikipendekeza kuwa unywaji wa kafeni kwa ajili ya kuboresha utendaji wa michezo katika viwango fulani.

      Hata hivyo, wataalam wameonya kwamba wakati wa kunywa kafeni, kuna hatari ya kunywa zaidi ya kiasi kilichopendekezwa.

      Uzito wa chini kabisa uliopimwa kwa kipimo cha Bwana Mansfield ulikuwa zaidi ya mara sita ya kiwango cha juu kilichopendekezwa

      Chanzo cha picha, Getty Images

      Maelezo ya picha, Uzito wa chini kabisa uliopimwa kwa kipimo cha Bwana Mansfield ulikuwa zaidi ya mara sita ya kiwango cha juu kilichopendekezwa

      Siku ya Jumanne uchunguzi ulionesha Bw Mansfield alianza kufunga kifua na kulalamika moyo wake unapiga haraka baada ya kuteketeza bidhaa hiyo.

      Dakika chache baada ya kwenda kujilala alianza kutokwa na povu mdomoni.

      Mkewe Suzannah aliwaomba majirani na familia, na kuitisha ambulensi. Hapo ndipo wahudumu wa afya walipoanza kujaribu kumuamsha muda wa dakika 45 lakini baadaye alitangazwa kuwa amefariki katika Hospitali ya Glan Clwyd huko Bodelwyddan, Denbighshire.

      Pia unaweza kusoma:

    • Zimbabwe yawahamisha wanafunzi 118 kutoka Ukraine

      Serikali ya Zimbabwe imefanikiwa kuwahamisha wanafunzi 118 kutoka Ukraine hadi nchi jirani, tovuti inayomilikiwa na serikali ya Herald inaripoti.

      Wanafunzi hao wamehamishiwa Romania (28), Hungary (15), Slovakia (26) na Poland (49).

      Aidha watapewa tiketi za ndege kurejea nyumbani, waziri wa habari amenukuliwa akisema.

      Balozi wa nchini Urusi na balozi wa Ujerumani wanashughulikia uhamishaji huo.

      Waziri huyo aliwataka wanafunzi wa Zimbabwe ambao bado wako Ukraine kutafuta njia ya kuelekea Poland ambako watapata msaada wa serikali.

    • Ni maeneo gani ya Ukraine yanayodhibitiwa na Urusi?

      Ramani
      Maelezo ya picha, Maeneo yenye rangi ya waridi yako chini ya udhibiti wa Urusi

      Unaweza pia kusoma:

      • Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
      • Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
      • Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • Jeshi la Urusi laushambulia mji wa Kharkiv

      m

      Shirika la habari la UNIAN linaripoti kuwa shambulio la roketi huko Kharkiv limepiga jengo la idara ya polisi ya mkoa katika mji huo.

      Video iliyotumwa kwenye chaneli ya Telegram ya mshauri wa serikali ya Ukraine inaonesha jengo likiwa limeteketea kwa moto.

      Anton Geraschenko, mshauri wa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ukraine, amesema jengo la Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Karazin pia linateketea kufuatia shambulio hilo.

      BBC bado haijaweza kuthibitisha video hiyo kwa uhuru.

      Takriban watu 21 wameuawa katika shambulizi la makombora Kharkiv

      Mwanajeshi wa Kikosi cha Ulinzi cha Jimbo la Ukraine akiwa amesimama ndani ya jengo la serikali lililoharibiwa baada ya shambulio la makombora mjini Kharkiv.

      Chanzo cha picha, EPA

      Maelezo ya picha, Mwanajeshi wa Kikosi cha Ulinzi cha Jimbo la Ukraine akiwa amesimama ndani ya jengo la serikali lililoharibiwa baada ya shambulio la makombora mjini Kharkiv.

      Takriban watu 21 waliuawa na 112 kujeruhiwa katika shambulio la makombora katika mji wa pili kwa idadi ya watu nchini Ukraine Kharkiv, meya wa jiji hilo amesema.

      Hata hivyo, gavana wa Tawala za Jimbo la Kharkiv alisema mashambulizi yote ya Urusi "yalikabiliwa", na maeneo kushikiliwa licha ya mashambulizi makubwa ya Kharkiv siku ya Jumanne na usiku.

      Gavana Oleh Synegubov alisema "adui wa Urusi alipata hasara kubwa".

      Inafahamika kuwa wanajeshi wa Urusi waliingia katika maeneo ya kaskazini-mashariki na kaskazini mwa mji huo huku Kharkiv walikabiliwa kwa ndege zenye kutumia sialaha kutoka kwenye anga.

      Soma zaidi:

      • Mlipuko karibu na mnara wa TV mjini Kyiv
      • Mzozo wa Ukraine: Urusi ina silaha ngapi za nyuklia?
    • Makumi ya wanafunzi wa Kenya waondolewa Ukraine

      m

      Wanafunzi 79 wa Kenya hadi sasa wameondolewa Ukraine kufuatia uvamizi wa Urusi.

      Serikali ya Kenya inasema mwanafunzi mmoja tayari ameshawasili Kenya, wengine 74 wako Poland, wawili wako Romania na wawili wako Hungary.

      Mamlaka zinaendelea kuratibu uhamishaji wa wanafunzi wengine wengi kutoka miji mbalimbali nchini Ukraine ili kuwaondoa.

      Wanafunzi wanne wa Kenya wameelezea nia yao ya kutoondoka Ukraine, wakitaja kwa sababu za kibinafsi.

      Wanafunzi kutoka Afrika wameungana na raia wa Ukraine kuondoka nchini humo baada ya uvamizi wa Urusi.

      Kulikuwa na wasiwasi wa ubaguzi wa rangi katika vituo vya mpakani na Umoja wa Afrika umezitaka nchi kuheshimu sheria za kimataifa na kuwasaidia wale wote wanaokimbia vita.

    • Nini ilichofanya Marekani hadi sasa nchini Ukraine?

      erritorial defence reservists across Ukraine have been preparing for a possible Russian invasion

      Chanzo cha picha, reuters

      Maelezo ya picha, Walinzi wa kieneo wa ziada Ukraine

      Rais Biden alianza hotuba yake kwa taifakwa sera nzito ya kigeni, akipongeza hatua zake - na mataifa mengine - kuunga mkono Ukraine katika siku saba zilizopita.

      Hiki ndicho Marekani ilichokifanya hadi sasa:

      Kutoa dola milioni silaha za thamani ya dola milioni 350 (£263m) kwa Ukraine

      Kusambaza misaada ya kibinadamu ya thamani yadola milioni 54 (£41m)

      Kuondoa benki kadhaa za Urusi kutoka kwenye mfumo wa dunia wa Swift

      Kuzuwia benki kuu ya Urusi kuilinda sarafu ya taifa hilo rouble

      Kujiunga na kikosi kazi chaeneo la Atlantiki kufuja na kuchukua mali za ‘oligarchs'

      Kufunga anga ya safari za ndege zinazomilikiwa na Urusi na ndege za Urusi

      Ikulu yaWhite House pia imeliomba baraza la Congress liongeze usaidizi wa ziada wa dola bilioni 6.4 (£4.8bn) za msaada wa dharura kwa kipindi cha miezi michache ijayo.

      Hatahivyo, Biden amesisitiza tena kwamba haitatuma vikosi kukabiliana na Warusi ndani ya Ukraine.

      Unaweza pia kusoma:

      • Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
      • Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
      • Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?