Urusi na Ukraine: Ni zipi hatari za shambulio la kinyuklia?

Russia's Poseidon nuclear-armed underwater vehicle

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Video ya gari la mtambo wa nyuklia wa Urusi ulio chini ya maji wenye silaha za nyuklia lenye uweze wa kujiendesha kufanya mashambulio unaofahamika kama Poseidon nuclear -armed underwater vehicle - ilichukuliwa na Tass, Shirika la habari la taifa la Urusi.

Jumapili, Rais Putin aliagiza jeshi lake kuhamisha " vikosi vya kudhibiti" - ambavyo vinajumuisha silaha za nyuklia ''kufanya jukumu la mapambano maalumu''. Lakini hilo linamaaninisha nini hasa?

Haiko wazi kabisa, wanasema wachambuzi wa Magharibi wanasema,. Maafisa wa uingereza wanasema kwamba lugha iliyotumiwa na Putin haiendani na uelewa wao wa viwango vya tahadhari kwa silaha za nyuklia za Urusi.

Baadhi wachambuzi wanafikiria Puti alikuwa anaamrisha hatua ya chini abisa ya tahadhari , "mara kwa mara", kuelekea hatua inayofuata ya juu , "ya juu zaidi", (yenye ''hatari ya kijeshi'' na "kamili " bado ni ya juu) lakini hilo lilikuwa isio ya kuaminika . Kila hatua inaongeza utayari kwa ajili ya matumizi ya silaha.

Wengi hatahivyo wamefasili hatua hiyo kimsingi kama aina ya kutoa kiashiria kwa umma, kuliko kuonyesha lengo halisi la kutumia aina hizo za silaha, ambazo Putin anafahamu kuwa zitaleta ulipizaji kisasi wa Magharibi. Waziri wa ulinzi wa Uingereza Ben Wallace amedokeza kuwa anaamini kuwa kimsingi tangazo la Putin lilikuwa ni kwa lengo la ''kuvutia ushawishi''

Hilo halimaanishi kwamba hakuna hatari na huenda hali ikahitaji kufuatiliwa kwa karibu.

Je lilikuwa ni onyo la kwanza?

Wiki iliyopita, Putin alionya kwa lugha ya mafumbo zaidi kwamba kama nchi nyingine zitaingilia mipango ya Urusi zitakabuiliwa na athari "jambo ambalo halijaonekana kabisa ". Hilo lilitafsiriwa kama onyo kwa Nato la kutohusika moja kwa moja kijeshi katika nchini Ukraine.

Nato kila mara imekuwa wazi haitafanya hilo, ikifahamu kuwa inaweza kusababisha mzozo wa moja kwa moja na Urusi ambao unaweza kuchochea vita vya nyuklia. Onyo la Jumapili lilikuwa la moja kwa moja zaidi na la umma.

TH

Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi

TH

Putin alisema hatua hiyo ilikuwa ni kujibu "kauli za uchokozi". Jumatatu, Kremlin alisema hii ilimaanisha kauli zilizotolewa na maafisa wa Magharibi ,ikiwa ni pamoja na kauli iliyotolewa na Waziri wa mambo ya nje wa Liz Truss, kuhusu uwezekano wa migongano na makabiliano na Nato.

Maafisa wa magharibi pia wanaamini kuwa onyo jipya limekuja kwasababu Putin hakuelewa uwezo wa kijeshi wa Ukraine.

Huenda alidhani kiwango cha upinzani wa kijeshi atakaokabiliana nao kutoka Ukraine ni wa kiwango cha chini. Na alifikiri kiwango cha kuungana kwa mataifa cha magharibi katika kuweka vikwazo vigumu ni cha chini. Hilo lilimfanya hana la kufanya ila kuongea kwa ukali na kuchukua hatua mpya.

"Hii ni dalili ya hasira, kukanganyikiwa na kukata tamaa," Jenerali wa Ulingereza aliyestaafu hivi karibuni alisema.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa mataifa Linda Thomas-Greenfield alisema lugha hii ni sehemu ya juhudi za Putin za kuhalalisha vita katika Ukraine kwa kudai sio ya mchokozi bali inakabiliwa na tisho na kwa hiyo inataka kujiinda.

Ikiangaliwa hivi, tahadhari ya nyuklia ni njia ya kusisitiza ujumbe huu kwa watu. Njia nyingine ya kuliangalia hili ni kwamba Putin ana wasi wasi juu ya mipango ya Magharibi ya kutoa usaidizi wa kijeshi kwa Waukraine na anataka kuwaonya juu ya kutofanya hilo sana.

Sababu nyingine ni kwamba anaogopa vikwazo, ambavyo alivielea katika tangazo lake, kama vilivyobuniwa kwa ajili ya kusababisha mzozo na kupindua serikali yake. Lakini kwa ujumla ujumbe unaonekana kuwa ni onyo kwa Nato kwamba kama itahusika moja kwa moja matukio yanaweza kuwa mabaya.

Unaweza pia kusoma:

line

Hatari ni zipi ?

Hata kama tisho la Putin ni onyo kuliko kuashiria utasi wa kutumia silaha, kila mara kuna hatari ya kutoelewana baina ya pande husika iwapo upande mmoja hautaelewa kile upande mwingine unachokimaanisha au matukio kutoweza kudhibitiwa.

Hofu ni kwamba Putin ametengwa na hawezi kuguswa, huku washauri wake wachache wakitaka kumwambia ukweli. Baadhi wanaogopa iwapo hatawaelewa.

Baadhi wanatumaini hatahivyo kwamba iwapo atakwenda mbali, wengine hata wanasema kuwa huenda maafisa wake wasikubali kutekeleza amri zake. Hatari ya mzozo wowote wa nyuklia inaweza kuwa imepanda juu kidogo lakini bado imesalia kuwa ya kiwango cha chini.

Nchi za Magharibu zimejibu vipi ?

Hadi sasa, serikali za magharibi zimekuwa makini wa kuzuwia hali kuwa mbaya zaidi iwe kwa matamshi makali au kwa hatua. Jeshi la Marekani liko tayari kwa hali ya tahadhari zake zake za kijeshi inayofahamika kama Defcon, na leo waziri wa habari wa Ikulu ya White House Jen Psaki alisema "hakuna sababu ya kubadili" viwango vya tahadhari yake ya nyuklia kwa sasa. Uingereza ina manowari za nyuklia na huenda isiseme lolote wazi.

Huu kwa sasa sio mzozo wa nyuklia na haupaswi kuwa mzozo huo, Maafisa wa imagharibi wanasema.

Je nchi za Magharibi zitafahamu inachofanya Urusi?

Waziri wa ulinzi wa Uingereza Ben Wallace aliiambia BBC kwamba Uingereza haijaona bado mabadiliko yoyote katika muundo wa silaha za nyuklia wa Urusi . Hilo litaangaliwa kwa karibu, vyanzo vya ujasusi vimethibitisha.

Wakati wa Vita baridi, machine kubwa za ujasusi zilibuniwa katika nchi za Magaharibi, kufuatilia kwa karibu mtambo wa nyuklia wa Moscow. Setilaiti, mifumo ya kuingilia mawasiliano na vyanzo vingine vilitathminiwa kuangalia dalili za mabadiliko ya tabia-kama vile maandalizi ya silaha na majeshi kwa ajili ya vilipuzi - hilo lingetoa onyo.

Mengi ya hayo bado yanafanyika na nchi za Magharibi yatakuwa yanaiangalia Urusi kuangalia iwapo kuwa kuna kitu ambacho kitaleta mabadiliko makubwa ya kitabia. Hakuna dalili kwa sasa za matumizi ya nyuklia.