Uvamizi wa Ukraine: Urusi yaonya kuwa itashambulia maeneo maalum mjini Kyiv

Wizara ya ulinzi ya Urusi imeonya kwamba inajiandaa kushambulia maeneo maalum katika mji mkuu wa Ukraine.

Moja kwa moja

  1. Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo haya ya moja kwa moja. Hadi kesho kwaheri

  2. Ajali ya ndege Comoro: Hakuna miili uliopatikana

    Ndege

    Chanzo cha picha, Flay Zanzibar

    Serikali ya Comoro imesema bado hakuna mwili wowote uliopatikana baada ya kuanguka kwa ndege inayofanya safari zake visiwani humo.

    Ajali hiyo imetokea wakati ndege hiyo ya Tanzania inayomilikiwa na kampuni ya Fly Zanzibar ilipokuwa inatoka makao makuu ya visiwa vya Comoro, Moroni kwenda kisiwa cha Mwali juma lililopita.

    Kwa mujibu wa mkurugenzi wa mawasiliano wa viwanja vya ndege Comoro Mohamed Said, Ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria 12 raia wa Comoro na marubani wawili raia wa Tanzania na inaaminika ilianguka baada ya kukumbana na hali mbaya ya hewa wakati ikikaribia kutua.

    Serikali ya Comoro kwa kushirikiana na kampuni ya wapiga mbizi ya ufaransa bado inaendelea kusaka miili ya watu hao 14, lakini mpaka sasa ni mabegi ya abiria na baadhi ya mabaki ya ndege ndivyo vitu pekee vilivyo patikana.

    Mmiliki wa Ndege hiyo Rubani Mohamed Mazrui amesema kuwa ndege nyingine ya kampuni hiyo inaendelea na shughuli za kusaka watu hao na ishara yoyote inayoashiria kuwepo kwa kitu chochote kinachohusiana na ajali hiyo.

    Ameongeza kuwa shughuli za uokoaji zinaendelea lakini mpaka sasa hakuna mwili wowote uliopatikana wala kisanduku cha kunakili data a safari ya ndege 'blackbox'.

  3. Mlipuko karibu na mnara wa TV mjini Kyiv

    Moshi mkubwa umeshuhudiwa

    Chanzo cha picha, Reuters

    Tunaona picha za moshi mkubwa karibu na mnara wa Televisheni huko Kyiv.

    BBC imethibitisha picha hizo lakini haijafahamika iwapo mnara huo uligongwa moja kwa moja.

    Picha nyingine zinaonesha mlipuko katika eneo hilo.

    Hapo awali wizara ya ulinzi ya Urusi ilionya wakaazi wa Kyiv kwamba inajiandaa kulenga maeneno maalumu katika mji mkuu.

  4. Habari za hivi punde, Uvamizi wa Ukraine: Urusi yaonya kuwa itashambulia maeneo maalum mjini Kyiv

    Wizara ya ulinzi ya Urusi imetoa onyo kwa wakazi wa Kyiv kwamba inajiandaa kushambulia maeneo maalum katika mji mkuu wa Ukraine.

    Katika taarifa iliyotolewa leo mchana, maafisa wa Urusi walisema vikosi vyao vinajiandaa kufanya "mashambulizi ya uhakika na ya hali ya juu" dhidi ya "vituo vya kiteknolojia vya Huduma ya Usalama ya Ukraine na kituo kikuu cha 72 cha PsyOps huko Kyiv".

    "Tunawahimiza raia wa Ukraine ambao wanatumiwa na watu wa kitaifa kutekeleza uchochezi dhidi ya Urusi, pamoja na wakaazi wa Kyiv wanaoishi karibu na vituo vya hivyo kuondoka nyumbani kwao," iliongeza taarifa hiyo.

    Maafisa walidai mashambuli hilo linafanywa ili "kuzuia mashambulizi ya mawasiliano dhidi ya Urusi".

    Huku hayo yakijiri Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Oleksiy Reznikov ameonya kuhusu uwezekano wa Urusi kufanya "shambulio la kisaikolojia".

    Bw. Reznikov alidai kwenye mtandao wake wa Facebook kuwa Urusi ikwanza inapanga kuvuruga mawasiliano.

    "Baada ya hapo, kutakuwa na usambazaji mkubwa wa taarifa ghushi kuhusu uongozi wa kijeshi na kisiasa wa Ukraine," aliandika.

  5. Nini kipya kutoka Ukraine?

    Huku dunia ikishuhudia siku ya sita ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, fahamu yaliyojitokeza hivi karibuni zaidi:

    • Katika Kharkiv - mji wa pili wa Ukraine - takriban watu 10 wameuawa na 20 kujeruhiwa katika mlipuko mkubwa wakati kombora la Urusi lilipopiga makao makuu ya serikali ya mkoa
    • Rais wa Ukraine anakiita kitendo hicho "ugaidi dhidi ya serikali" na anaishutumu Urusi kwa uhalifu wa kivita kwasababu hata makazi na raia pia wanashambuliwa, ikiwa ni pamoja na kuuawa kwa watoto 16
    • Katika hotuba yake kwa kikao maalum cha bunge la Umoja wa Ulaya, anaomba uwanachama wa muungano huo, akisema itakuwa na nguvu zaidi na Ukraine ndani yake.
    • Katika mji wa kaskazini-mashariki wa Okhtyrka, hadi wanajeshi 70 wa Ukraine wameripotiwa kuuawa katika katika shambulio lililotekelezwa na Urusi.
    • Wakati huo huo, msafara mkubwa wa magari ya kivita ya Urusi yanasonga mbele kuelekea mji mkuu wa Ukraine Kyiv
    • Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov, ameonekana kutoa uhalali mpya wa uvamizi wa Urusi - akiuambia mkutano wa Umoja wa Mataifa kuwa ni kuzuia Ukraine kupata silaha za nyuklia
    • Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anaishutumu Urusi kwa mashambulizi ya "kinyama na ya kiholela" na inasema iko tayari kuzidisha vikwazo vya kiuchumi kwa Urusi kwa muda wote itakavyokuwa.
  6. Watu 10 wauawa katika shambulio la kombora Kharkiv

    Takriban watu 10 wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa baada ya shambulio la kombora kupiga kwenye mji wa pili kwa ukubwa Kharkiv mashariki mwa Ukraine.

    Dazeni wengine waliokolewa kutoka chini ya vifusi.

    Chanzo chetu ni Huduma ya Dharura ya Serikali, kama ilivyonukuliwa na shirika la habari la Interfax-Ukraine.

  7. Mtoto wa Museveni anaunga mkono uvamizi wa Urusi nchini Ukraine

    Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba ndiye afisa mkuu wa kwanza wa kijeshi barani Afrika kujitokeza kuunga mkono Urusi

    Mtoto mwenye nguvu kiutawala wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ameelezea kuunga mkono uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

    Jenerali Kainerugaba - ambaye ni kamanda wa majeshi ya nchi kavu ya Uganda – aliweka ujumbe kwenye mtandao wa Twitter, kwamba " "binadamu wengi (ambao si wazungu) wanaunga mkono msimamo wa Urusi nchini Ukraine".

    "Putin yuko sahihi kabisa!" aliongeza.

    "Wakati USSR ilipoweka makombora yenye silaha za nyuklia nchini Cuba mwaka 1962, nchi za Magharibi zilikuwa tayari kulipua ulimwengu juu yake. Sasa Nato ikifanya hivyo wanatarajia Urusi kufanya tofauti."

    Jenerali Kainerugaba ndiye afisa mkuu wa kwanza wa kijeshi barani Afrika kuunga mkono hadharani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

    Anasemekana kuwa anaweza kuwa mrithi wa babake mwenye umri wa miaka 77, ambaye amekuwa madarakani tangu 1986.

    Umoja wa kanda ya Afrika Magharibi Ecowas umelaani uvamizi wa Urusi, huku Umoja wa Afrika ukiitaka Moscow kuheshimu "eneo la uadilifu.

    Wizara ya mambo ya nje ya Afrika Kusini imetoa wito wa kuondolewa kwa wanajeshi wa Urusi kutoka Ukraine.

    Jenerali Kainerugaba pia alimtuma tena ujumbe wa mwanahabari mashuhuri wa Uganda Andrew Mwenda, ambaye alisema kwamba hata "mgeni katika siasa za kimataifa anaweza kuona kwamba Moscow haiwezi kamwe kuruhusu Ukraine kujitosa kwa Nato, EU, kwa sababu inaleta tishio kwa Urusi!

    Soma zaidi:

  8. Ukraine na Urusi:Shambulio la pili lapiga mji wa pili kwa ukubwa Kharkiv

    Moto mkubwa

    Kharkiv imekumbwa na shambulio la Urusi. Shambulio hilo la asubuhi lilionekana kulenga ofisi za serikali katika eneo la Freedom Square katikati mwa jiji.

    Maafisa wa dharura wa eneo hilo waliandika kwenye mtandao wa Facebook kwamba raia sita walijeruhiwa wakati wa shambulio la makombora katika ofisi ya utawala wa serikali, akiwemo mtoto mmoja.

    Makombora ya Urusi yamegonga kitovu cha kitamaduni cha mji wa pili wa Ukraine katika kile maafisa walisema ni shambulio baya na la "kinyama".

    Jumba la opera, ukumbi wa tamasha na ofisi za serikali zilipigwa katika Freedom Square, katikati mwa jiji la kaskazini-mashariki, Kharkiv. Takriban watu 20, ikiwa ni pamoja na mtoto walijeruhiwa, lakini mamlaka bado wanajaribu kubaini kama mtu yeyote aliuawa.

    Shambulio hilo limetokea huku rais wa Ukraine akisema Urusi ilikuwa ikifanya uhalifu wa kivita.

    " Hivi ndivyo asubuhi yetu inavyoonekana, watu wa Ukraine," Rais Volodymyr Zelensky alisema. "Huu ni ugaidi dhidi ya Ukraine.

    Hakukuwa na malengo ya kijeshi katika uwanja huo - wala hawako katika maeneo ya makazi ya Kharkiv ambayo yanapigwa na makombora," aliongeza.

    Picha za video zilionesha kombora likipiga jengo la serikali ya mtaa na kulipuka, na kusababisha moto mkubwa. Kharkiv imekuwa imeshambuliwa kwa mabomu kwa siku kadhaa sasa.

    Serikali ya Ukraine inaishutumu Urusi kwa kujaribu kuizingira Kharkiv na miji mingine, ukiwemo mji mkuu wa Kyiv, ambako msafara mkubwa wa kivita wa Urusi unakaribia.

  9. Hofu yatanda baada ya msafara huu kuonekana

    m

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mbinu ya msafara huu mkubwa wa wanajeshi wa Urusi umetoa maana mpya ya kutisha kwa mtazamo wa ulimwengu.

    Kila mtu duniani anaweza kuona kwamba msafara huu uko njiani, kuna hata ripoti kwamba unaimarisha kabla ya kufika jijini.

    Kuongeza hofu hii ni ripoti zinazokuja kutoka sehemu nyingine za Ukraine, kwamba Urusi inazingira maeneo yenye watu wengi kwa kutumia "mbinu za enzi za kati", maeneo yanayozunguka na kuwanyima chakula, maji na vifaa muhimu.

    Wakati uvamizi huu ulipoanza, kulikuwa na matarajio kwamba ingekuwa ni suala la siku tu, hata suala la saa kadhaa kabla ya jeshi kubwa la Urusi kuingia Kyiv.

    Ni siku sita sasa na Ukraine bado imesimama - imesimama kwa sababu ya upinzani uliowekwa na jeshi la Ukraine, kwa kutumia silaha na risasi za Magharibi, lakini pia inalindwa na wananchi ambao wanachukua bunduki, kusaini kwa vikosi vya ulinzi vya jirani na kwenda hadi mistari ya mbele.

    Lakini hakuna ubishi kwamba msafara huu, hata kama unazidi kukaribia na milipuko inazidi kukaribia.

    Walikuwa hasa kwenye ukingo wa jiji, jana usiku palikuwa karibu sana hivi kwamba jengo letu wenyewe lilitikisika.

  10. Mzozo Ukraine: Kundi la kwanza la wanafunzi wawasili Ghana

    m

    Ghana imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuwahamisha raia wake wanaokimbia mzozo wa Ukraine kufuatia uvamizi wa Urusi.

    Kundi la kwanza la wanafunzi 17 waliwasili Jumanne asubuhi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kotoka, katika mji mkuu, Accra.

    Wizara ya mambo ya nje ya Ghana hapo awali ilisema wanafunzi 460 walikuwa wakielekea Poland, Hungary, Romania, Slovakia na Jamhuri ya Czech.

    Wanatarajiwa kurejea nyumbani siku zijazo.

    Idadi kamili ya raia wa Ghana wanaoishi nchini Ukraine haijulikani na kwa sasa, serikali inakutana na wazazi na walezi ili kuwaandikisha wanafunzi wote nchini humo.

    Inakadiriwa kuwa zaidi ya raia 1,000 wa Ghana kwa sasa wanasoma au kufanya kazi nchini Ukrainia.

    • Uvamizi Ukraine: Ghadhabu zazuka baada ya Waafrika kubaguliwa Ukraine
    • Urusi na Ukraine: Zijue athari za vita ya Ukraine kwa Afrika
  11. AU yakemea unyanyasaji wa Waafrika maeneo ya mpaka wa Ukraine

    mm

    Chanzo cha picha, Reuters

    Umoja wa Afrika umepinga unyanyasaji wa Waafrika wanaojaribu kutoka Ukraine na kuvuka kuelekea katika nchi jirani.

    Taarifa kutoka umoja wa bara hilo ilisema mapema Jumatatu kwamba Waafrika wakitengwa kutakuwa na ubaguzi wa rangi na ukiukaji wa sheria za kimataifa.

    Iliongeza kuwa watu wote wana haki sawa ya kuvuka mipaka ya kimataifa kutokana na migogoro, bila kujali utaifa wao au utambulisho wa rangi.

    Tangu Urusi ilipoivamia Ukraine wiki iliyopita, Waafrika na watu wengine wa rangi mbalimbali wameripoti kutendewa vibaya na maafisa wa mpaka wa Ukraine, huku baadhi wakidai kuwa walizuiliwa kupanda treni na mabasi yanayokimbia miji wakishambuliwa au waliambiwa tu wasubiri kwenye maeneo ya mpakani huku wengine waliruhusiwa.

    Baadhi ya wanafunzi wa Kiafrika waliripoti kuzuiwa kuingia hotelini na kulala barabarani.

    Katika siku chache zilizopita, maelfu ya Waafrika, wengi wao wakiwa wanafunzi, wamevuka mipaka hadi Poland, Romania, Hungary na mataifa mengine katika eneo hilo, huku wengine wakijaribu kurejea katika nchi zao.

  12. Ukraine: Shambulio la Kharkiv lilikuwa la uhalifu wa kivita, asema Rais Zelensky

    mm

    Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

    Rais wa Ukraine ameelezea shambulizi la bomu la Kharkiv, ambalo liliua makumi ya raia, kama uhalifu wa kivita.

    Volodymyr Zelensky amesema kulikuwa na mashuhuda walioona raia wakilengwa kwa makusudi wakati wa shambulizi la Jumatatu kwenye mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine.

    Mashirika ya kutetea haki za binadamu pia yalisema uhalifu wa kivita unaweza kutokea wakati wa uvamizi wa Urusi.

    Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinai (ICC) inatarajia kuanzisha uchunguzi wake yenyewe kuhusu madai hayo.

    Kuna "msingi wa kuridhisha" kuamini uhalifu wa kivita au uhalifu dhidi ya binadamu umetendwa nchini Ukraine, mwendesha mashtaka mkuu Karim Khan alisema Jumatatu jioni.

    Siku chache baada ya kuanzisha uvamizi wake, Urusi inaishambulia Ukraine katika nyanja kadhaa, lakini kasi yake imepunguzwa baada ya kupata upinzani kutoka kwa Ukraine.

    Vingora vya mashambulizi ya anga vilisikika tena katika mji mkuu, Kyiv, huku picha za satelaiti zikionyesha msafara wa wanajeshi wa Urusi wenye umbali wa maili 40 (kilomita 64) ukitokea kaskazini mwa mji huo.

    Msafara huo unajumuisha magari ya kivita, vifaru, mizinga na magari ya vifaa vingine, na uko umbali wa chini ya maili 18 (30km) kutoka Kyiv, kulingana na Maxar Technologies, ambayo ilitoa picha hizo.

  13. Asilimia 75 ya wanajeshi wa Urusi wako ndani ya Ukraine

    mm

    Chanzo cha picha, bbc

    Urusi imeongeza idadi ya wanajeshi wake nchini Ukraine kutoka 40% hadi karibu 75%, msomi wa kijeshi anasema.

    Idadi hiyo ya 75% pia imetajwa na afisa mkuu wa ulinzi wa Marekani.

    Dk Jack Watling ni mtafiti katika vita vya ardhini na sayansi ya kijeshi katika Taasisi ya Royal United Services.

    Aliambia kipindi cha BBC Radio 4 cha Today programme, kuwa kundi kubwa la wanajeshi wa Urusi wanasonga mbele kutoka Belarus na kuanza kuweka masharti ya kuwawezesha kufanya shambulizi huko Kyiv.

    Alipoulizwa kuhusu pendekezo kwamba Urusi imetumia makombora kwenye maeneo ya makazi huko Kharkiv, anaelezea silaha hizi kama mifumo mingi ya kurusha roketi ambayo inalipua idadi kubwa ya makombora yasiyoongozwa kwenye eneo.

    Anasema pia kuna ushahidi kwamba baadhi ya hizi nyingi zina vilipuzi vingi.

    "Ukweli ni kwamba hayaongozwi na munaweka kiasi kikubwa cha vilipuzi kwenye eneo lenye wakazi wengi," anasema.

    Jeshi la UKraine halifanyi kazi tena katika miundo ya kijeshi, lakini sasa lipo zaidi katika nafasi ya kujilinda sawa na kuwa zaidi na zaidi sehemu ya ulinzi wa eneo na kujitolea, anasema.

    • UrusUkraine: Ni zipi hatari za shambulio la kinyuklia?
  14. Wanajeshi 70 wa Ukraine wauawa huko Okhtyrka kaskazini-mashariki

    Mashambulizi ya Urusi yalipiga kambi moja ya wanajeshi na kuwaua wanajeshi 70 wa Ukraine Jumapili

    Chanzo cha picha, Dmytro Zhyvytskyi/ Telegram

    Maelezo ya picha, Mashambulizi ya Urusi yalipiga kambi moja ya wanajeshi na kuwaua

    Maafisa wa Ukraine wamethibitisha kuwa wanajeshi wasiopungua 70 waliuawa katika shambulio la makombora ya Urusi katika kambi yao ya kijeshi siku ya Jumapili.

    Shambulio hilo lilitokea Okhtyrka, katika eneo la Sumy ambalo kwa sasa limezingirwa na majeshi ya Urusi. Siku ya Jumatatu, wafanyikazi wa dharura walikuwa bado wakipekua vifusi kujaribu kutafuta manusura.

    Bunge la Ukraine limeandika hivi punde tu kuwaenzi wanajeshi, likisema "Utukufu wa milele kwa mashujaa wa Ukraine". Bunge lilisema waliuawa na makombora ya Grad.

  15. Uhalifu wa kivita utafunguliwa mashtaka - Uingereza

    TSN CHANNEL

    Chanzo cha picha, TSN CHANNEL

    Urusi itatumia "mbinu kubwa zaidi" nchini Ukraine na uhalifu wowote wa kivita utachukuliwa hatua, naibu waziri mkuu wa Uingereza amesema.

    Dominic Raab anasema: "Hatua zote tunazochukua pia tunaunga mkono juhudi za kuhakikisha kwamba ushahidi wa uhalifu wa kivita unahifadhiwa.

    " Aliiambia BBC kuwa jumuiya ya kimataifa haiko tayari kuweka ukanda wa kutoruka ndege katika Ukraine kwa sababu itahusisha nia ya kutungua ndege za Urusi jambo ambalo "ni hali ya hatari".

    Badala yake, Uingereza ilikuwa inaweka juhudi zake zote katika vikwazo vya kiuchumi ambavyo vilikuwa vinafadhaisha mfumo wa kifedha wa Putin.

    Hawa pia walikuwa wanahitaji kupata mfumo wa kimataifa na ambao watatumia shinikizo kwa Putin, anasema.

    Alipoulizwa iwapo nchi za magharibi zinapaswa kwenda mbele zaidi katika suala la usambazaji wa mafuta na gesi, Raab anasema: "Ndiyo nadhani tutaliangalia hilo kwa makini sana... Tunapochukua hatua ya kufa njaa jeshi la Urusi, hakuna kitu ambacho nje ya meza."

    • Mzozo wa Ukraine: Fahamu uhusiano wa kihistoria kati ya Ukraine na Urusi
    • Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
  16. Ukraine yaomba usaidizi wa mmiliki wa Chelsea

    m

    Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich ameombwa na Ukraine kusaidia juhudi zao za kufikia "azimio la amani" na Urusi, msemaji wa bilionea huyo anasema.

    Waliongeza Abramovich aliwasiliana na maafisa wa Ukraine na "amekuwa akijaribu kusaidia tangu wakati huo".

    Ukraine imetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano kabla ya mazungumzo ya amani nchini Belarus.

    Rais wa Urusi Vladimir Putin alianzisha uvamizi wa kijeshi katika nchi jirani ya Ukraine siku ya Alhamisi.

    Wizara ya afya ya Ukraine ilisema Jumapili kwamba raia 352, wakiwemo watoto 14, wameuawa tangu uvamizi wa Urusi uanze.

    Abramovich alitangaza Jumamosi kwamba "usimamizi na utunzaji"wa kilabu ulikuwa ukitolewa kwa wadhamini wa wakfu wa hisani wa Chelsea.

    Abramovich - ambaye anasalia kuwa mmiliki wa Chelsea kwa mkopo wa £1.5bn - hakurejelea uvamizi wa Urusi kwa Ukraine katika taarifa yake.

    Mzee huyo mwenye umri wa miaka 55 ni mmoja wa watu tajiri zaidi nchini Urusi na anaaminika kuwa karibu na Rais wa Urusi Putin.

    Msemaji huyo aliongeza: "kwa kuzingatia kile kilicho hatarini, tungeuliza ufahamu wako kwa nini hatujazungumza juu ya hali kama hiyo au ushiriki wake."

    Mkurugenzi wa filamu wa Ukraine na mtayarishaji Alexander Rodnyansky alithibitisha kuhusika kwa mmiliki wa Chelsea katika majaribio ya kufikia azimio la amani, lakini akaongeza kuwa hana uhakika na athari itakayotokana nayo.

    • Roman Abramovich akabidhi usimamizi wa Chelsea kwa bodi ya wadhamini
  17. Pele: Mchezaji bora wa Brazil aruhusiwa kutoka hospitali

    mm

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Gwiji wa Brazil Pele ameruhusiwa kutoka hospitalini baada ya kupata matibabu ya uvimbe na maambukizi ya mfumo wa mkojo.

    Mshindi huyo Kombe la Dunia kwa mara tatu, mwenye umri wa miaka 81, alilazwa katika Hospitali ya Sao Paulo Albert Einstein tarehe 13 Februari, kwa ajili ya matibabu ya uvimbe wa utumbo mpana.

    Siku nane baada ya kulazwa, madaktari waligundua ugonjwa wa mfumo wa mkojo, ambao uliongeza muda wake wa kukaa hospitalini.

    Hata hivyo, hospitali hiyo ilisema Pele yuko katika "hali nzuri ya kiafya".

    Ataendelea na matibabu ya uvimbe huo ambao uligunduliwa kwa mara ya kwanza katika vipimo vya kawaida mwezi Septemba.

    Pele alifanyiwa upasuaji wa tezi dume mwaka 2015 baada ya kulazwa hospitalini kwa mara ya pili ndani ya miezi sita, na alirejea tena kwa ajili ya maambukizi ya mkojo mwaka wa 2019.

    Alirudishwa tena Disemba kwa matibabu ya uvimbe huo lakini aliruhusiwa kabla ya Krismasi.

    Mfungaji bora wa muda wote wa Brazil akiwa na mabao 77 katika michezo 92, mshambuliaji huyo wa zamani ni miongoni mwa wachezaji wanne pekee waliofunga katika michuano minne ya Kombe la Dunia.

    • Pele: Mchezaji maarufu wa soka nchini Brazil asema hali yake afya ni jambo la kawaida kwa watu wenye umri kama wake
    • Pele: Aliyekuwa mchezaji soka maarufu Brazil anahisi aibu kutoka nyumbani kutokana na hali mbaya ya kiafya
  18. Rigobert Song kuifunza timu ya taifa ya Cameroon

    Rigobert song

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Rigobrt song

    Mchezaji wa zamani wa Liverpool Rigobert Song anatarajiwa kutangazwa kuwa mkufunzi mpya wa timu ya Cameroon kutokana na agizo la rais wa taifa hilo.

    Song mwenye umri wa miaka 45 atachukua mahala pake Toni Conceicao , ambaye aliiongoza timu hiyo ya taifakatika michuano ya kombe la Afrika mnamo mwezi Januari

    Song ndiye mchezaji wa zamani wa taifa hilo aliyeshiriki mechi nyingi zaidi akiwachezea Indomitable Lions, mara 137.

    Taarifa ilisema Cameroon inahitaji ‘hewa safi’

    ‘’Kutokana na agizo la rais, mkufunzi wa timu ya taifa ya wanaume , bwana Antonio Conceicao amefutwa kazi na badala yake nafasi yake ikachukuliwa na Rigobert Song’’ , alisema waziri wa michezo wa Cameroon Narcisse Mouelle Kombi.

    "Shirikisho la Soka la Cameroon (Fecafoot) limeagizwa kuchukua hatua zinazohitajika kutekeleza kwa haraka na usawa wa maagizo ya rais"

    Uteuzi huo hautakuwa wa kawaida kwa sababu sheria za Fifa zinahitaji chama chochote mwanachama kuwa huru na kuepuka aina yoyote ya kuingiliwa kisiasa.

    Conceicao alikuwa ameiongoza Cameroon kufuzu katika raundi ya muondoano wa kufuzu kwa Kombe la Dunia na watacheza na Algeria katika mikondo miwili mwezi Machi ili kufuzu kwa Qatar 2022.

    • Rigobert Song asafirishwa Ufaransa
  19. Mamia ya wanafunzi wa Ghana wameondoka Ukraine

    Takriban wanafunzi 460 wa Ghana wameondoka Ukraine wakielekea Poland, Hungary, Romania, Slovakia na Jamhuri ya Czech kufuatia uvamizi wa Urusi, Waziri wa Mambo ya Nje Shirley Ayorkor Botchwey amesema.

    Wanafunzi hao watapokelewa na maafisa kutoka balozi za nchi hizo na maafisa wa vyama vya wanafunzi wa Ghana.

    Wanatarajiwa kurejea Ghana katika siku zijazo.

    Wazazi na walezi wa wanafunzi hao wamealikwa na serikali katika mkutano katika mji mkuu wa, Accra, siku ya Jumanne.

    Awali serikali ilikuwa imewataka wanafunzi wa Ghana nchini Ukraine kutafuta makazi katika nyumba zao au katika maeneo yaliyotengwa na serikali.

    Zaidi ya raia 1,000 wa Ghana kwa sasa wanasoma au kufanya kazi nchini Ukraine.

    Baadhi ya Waafrika walikuwa wamelalamikia ubaguzi wa rangi katika mpaka wa Ukraine na Poland.

    • Uvamizi Ukraine: Ghadhabu zazuka baada ya Waafrika kubaguliwa Ukraine
  20. Hali ya Ukraine mpaka sasa

    Takriban wanajeshi 70 wameuawa katika shambulio la mizinga la Urusi, maafisa wa Ukraine wamethibitisha.

    Wafanyakazi wa dharura wanajaribu kutafuta manusura katika Kituo cha kikanda cha Kherson ambacho sasa kimezingirwa na wanajeshi wa Urusi, zinasema ripoti, huku wanajeshi na vifaa vya kijeshi vimeripotiwa kuwepo "pande zote".

    Jeshi la Urusi linaendelea kusonga mbele kwa kasi huko Kyiv, na picha za satelaiti zinazoonyesha msafara wa kivita ambao una urefu wa maili 40 (65km.

    Makumi ya raia waliuawa mapema Jumatatu katika shambulio la makombora la Urusi kwenye mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine, Kharkiv.

    Serikali ya Ukraine imesema inapanga kuuza hati za kivita ili kulipia vikosi vyake vya kijeshi

    m

    Chanzo cha picha, Getty Images