Mazungumzo ya ‘Uaminifu’ huku Ukraine ikiisukuma Ujerumani kutuma Leopards Ukraine

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vifaru vya Leopards vimemeundwa kushindana na vifaru vya Urusi vinavyotumiwa katika uvamizi nchini Ukraine

Waziri wa ulinzi wa Ukraine amesema kwamba alikuwa na "mazungumzo ya uaminifu" na mwenzake wa Ujerumani kuhusu vifaru vya Ujerumani vinavyofahamika kama German Leopard 2, ambavyo Ukraine umeviomba kwa Ujerumani kwa dharura ili kukabiliana na vile vya Urusi.

Bado Ujerumani haijaamua iwapo itatuma vifaru hivyo nchini Ukraine, au itaruhusu nchi nyingine kutoa msaada wao, licha ya shinikizo kwa utawala wa Ujerumani kuchukua hatua ya kutuma vifaru hivyo.

"Tulikuwa na mazungumzo ya uaminifu kuhusu Leopards 2, yayakayoendelea," Oleksii Reznikov alisema baada ya mkutano wa washirika wa Magharibi.

Kyiv inapata silaha nyingine nyingi za Nato.

Mkutano huo uliofanyika katika ngome ya kijeshi ya Ujerumani -Ramstein AirBase ulifikia makubalino ya kutuma magari mengine zaidi ya kijeshi, mifumo ya ulinzi wa mashambulio ya anga na silaha nyingine.

 Lakini Leopard 2 inaonekana kuwa italeta mabadiliko makubwa kwa Ukraine, kwani ni silaha iliyo rahisi kwa matunzo na imeundwa hususan kwa ajili ya kushindana na vifaru vya Urusi vinavyofahamika kama T-90 , ambavyo vinatumiwa katika mashambulizi ya Urusi ndani ya Ukraine.

Waziri wa usalama Boris Pistorius alisema kuwa maoni yameendelea kuwa ya mgawanyiko khusu kupelekwa kwa vya Leopards, na akakanusha kuwa Ujerumani inaweka pingamizi ya kupelekwa Ukraine kwa silaha hizo.

Chini ya sheria ya kuuza silaha nje ya Ujerumani, nchi nyingine zinazotaka kupeleka msaada wa Leopards – kama viole Poland na Finland – haziwezi kufanya hivyo mpaka ziruhusiwe na utawala wa Berlin.

'Uamuzi lazima ufanyika'

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliwasifu washirika wa Nato kwa msaada wao wa kijeshi, lakini akasema " bado tutapigania kupata vifaru vya kisasa".

"kila siku tunavyosonga mbele inaonekana dhahiri kwamba hakuna mbadala mwingine , kwamba uamuzi kuhusu vifaru vya kijeshi lazima uchukuliwa."

Vifaru vingi vya Ukraine vinavyotumiwa kwa sasa ni vya miundo ya zamani ya enzi ya Muungano wa Usovieti, mara nyingi huwa vichache na kuzidiwa nguvu na vifaru vya Urusi.

Zaidi ya vifaru aina ya Leopards 2,000 viko katika maghala ya silaha kote Ulaya. Rais Zelensky anaamini kuwa vifaru 300 kati ya hivyo vinaweza kuwasaidia kuishinda Urusi

Bw Pistorius- alisema kuwa Berlin inajhiandaa kuchukua uamuzi haraka iwapo kutakuwa na maafikiano miongoni mwa washirika, ingawa hakusema ni lini uamuzi kuhusu vifaru hivyo unaweza kuchukuliwa.

Mkwamo wa ujerumani

g

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Waziri wa ulinzi wa Ukraine Minister Oleksii Reznikov (Kulia) akiwa pamoja na washirika wake wa Kyiv na ujerumani mjini with Ramstein
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ujerumani umejipata katika mkwamo huu kutikana na mambokadhaa mkiwemo diplomasia ya kimataifa na urithi wake katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Ilikuwa na sera ya kututoma silaha kwenye maeneo ya vita, lakini hilo lilibadilika mwezi Februari mwaka jana baada ya uvamizi wa Urusi.

 Mwishoni mwa mwaka jana , Mkuu wa Nato Jens Stoltenberg alisema kuwa Ujerumani sasa "ni miongoni mwa washirika wanaotoa silaha zaidi , fedha na msaada wa kibinadamu kwa Ukraine", kwa kutuma huko makombora, mifumo ya ulinzi ya ang ana magari ya kijeshi ya mapigano.

Lakini ujerumani inasita kutuma vifaru vya Leopards mpaka zijumuishwe na sehemu ya silaha zinazotumwa na Nato ambazo zitajumuisha vifaru vyenye nguvu zaidi vya Marekani vinavyofahamika kama M1 Abrams.

 Marekani imekataa hili, ikisema kuwa vifaru vya Abrams haviwezi kutumwa kwa vikosi vya Ukraine kwasababu ni vigumu kutumiwa na na ni ghali kuvikarabati.

Hatahivyo, kumekuwa na shinikizo kutoka kwa baadhi kuitaka Marekani kutuma vifaru vyake , ili kuiwezesha pia Ujerumani kufanya hivyo.

 Waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin alikanusha kuwa Ujerumani ilikuwa inasubiri marekani kwanza ichukue hatua. "Haya mawazo ya kuanza kwanza – katika fikra zangu sio tatizo," alisema baada ya mkutano wa Ijumaa wa nchi 54 katika ngome ya vikosi vya anga vya Ujerumani -Ramstein Air Base.

 Ujerumani bado inakabiliwa na jinamizi la maasi yaliyofanyika enzi ya wanazi katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia, na Kansela Olaf Scholz anaaminiwa kuwa mwangalifu katika kufanya kitu chochote kinachoweza kuifanya hali nchini Ukraine kuwa mbaya zaidi.

 Mwanasiasa wa Chama cha upinzani kinachoongoza nchini Ujerumani cha Christian Democrat (CDU), Johann Wadephul, alilaani sera ya serikali "ya kukataa" kupelekwa Ukraine kwa vifaru vya Leopards, akisema kuwa itaathiri hadhi ya Ujerumani kimataifa. ‘’Ni nini Scholz anachosubiri?" aliuliza.

 Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Zbigniew Rau pia alikosoa kusita kwa Ujerumani.