Urusi na Ukraine: Ipi sababu ya Ujerumani kusita kuipatia Ukraine vifaru vya Leopard?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kifaru cha leopard cha Ujerumani

Ripoti zilionyesha kuwa Ujerumani itatuma vifaru Ukraine ikiwa tu Marekani itafanya vivyo hivyo.

Kansela Olaf Schultz yuko chini ya shinikizo linaloongezeka la kimataifa na la ndani ili kuipatia Kyiv vifaru vya Leopard 2 vinavyotengenezwa Ujerumani, au angalau kukubali kuwasilishwa Ukraine na nchi nyengine.

Poland na Finland ziliahidi kutuma Vifaru vya Leopard huko Kyiv, lakini zilihitaji kibali cha Ujerumani kufanya hivyo.

Lakini Berlin bado inafanya mazungumzo na Marekani kabla ya kufafanua msimamo wake rasmi.

Zelensky anakosoa kusita kwa Ujerumani kutuma vifaru vyake nchini mwake huku akiahidi kuikomboa Crimea.

Wengi wanatarajia tangazo baada ya washirika wa magharibi wa Ukraine kukutana katika kambi ya kijeshi ya Marekani ya Rammstein kusini magharibi mwa Ujerumani.

Ripoti zinaonyesha kuwa Schultz hatoipatia Ukraine Vifaru vyake hadi pale Rais wa Marekani Joe Biden atakubali kuipatia Ukraine vifaru vya Abrahams vya Marekani .

Mshauri mkuu wa usalama wa Pentagon, Colin Kahl, alisema jioni siku ya Alhamisi kwamba Marekani haiko tayari kukidhi matakwa ya Kyiv kuipatia vifaru vya Abrahams.

"Kifaru cha Abrahms ni kipande cha vifaa vigumu sana," Kahl alisema. "Ni ghali. Ni vigumu kufanya mazoezi navyo. Ni turbojet."

Chanzo kikuu cha serikali ya Ujerumani kiliiambia BBC kwamba ripoti za mzozo kati ya Berlin na Washington kuhusu vifaru hivyo zilitiwa chumvi, lakini zilikuwa zikizua wasiwasi miongoni mwa washirika wa magharibi wa Ukraine.

Utoaji wa vifaru vya Magharibi, kwa idadi ya kutosha, unaonekana kuwa muhimu sana ikiwa Ukraine inataka kuishinda Urusi au, angalau, ijilinde dhidi ya shambulio linalotarajiwa na Rais wa Urusi Vladimir Putin katika msimu wa kuchipua.

Hadi sasa, Uingereza ndiyo nchi pekee ambayo imeahidi kusambaza vifaru kwa Ukraine. Nchi nyingine, ikiwa ni pamoja na Ujerumani, Ufaransa na Marekani, zimetuma au kujitolea kutuma magari ya kivita, mifumo ya ulinzi wa anga na vifaa vingine vizito.

Je ni kwanini Waziri mkuu wa Ujerumani anasita sita

Dalili zote zinaonyesha kuwa Schultz hataruhusu watu wengine kusambaza vifaru vyya Leopard kwa Ukraine, Makamu wa Kansela wa Ujerumani Robert Habeck alisema wiki moja iliyopita.

Lakini Schultz bado hajajitolea kuhusika na suala hilo, na tahadhari yake inatokana na sababu kadhaa, ikiwa ni pamoja na wasiwasi juu ya kusambaa kwa vita, na majibu ya Rais wa Urusi Vladimir Putin kuhusu mataifa ya magharibi kuipatia silaha Ukraine suala ambalo wataalamu wengi wanaamini kuwa halifai.

.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Ujerumani imekuwa ikisita kuipatia silaha Ukraine
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Matarajio ya vifaru vya Ujerumani kwenye ardhi ya Ukreni bado haijapokelewa vyema mjini Berlin, ambapo historia ya Vita vya Kidunia vya pili ni wingu ambalo bado limetanda juu ya taifa hilo.

Schultz anafuatilia kura za ndani, ambazo zinaonyesha kuwa umma kwa ujumla umeridhika na majibu yake kwa Ukraine, tofauti na sera na utendaji wake katika maeneo mengine mengi.

Kura ya maoni ya hivi majuzi ya redio ya taifa iligundua kuwa asilimia 41 ya wananchi wanadhani Ujerumani inaipatia Ukraine kiasi kinachofaa cha silaha, asilimia 26 wanaamini kuwa inaunga mkono kwa kiasi kikubwa mno, na asilimia 25 ya Wajerumani wanafikiri kuwa nchi hiyo haijatuma silaha za kutosha.

Schultz aliahidi kwamba Ujerumani itachukua nafasi kubwa zaidi ya kijeshi katika jukwaa la dunia, lakini miaka mingi ya uwekezaji duni imeacha vikosi vyake vya kijeshi katika hali ya duni.

Hata iwapo mshauri atatoa idhini ya kupeleka vifaru, mtengenezaji wa silaha Rheinmetall ameonya kuwa urekebishaji na mahitaji ya maandalizi yatachelewesha uwasilishaji kwa miezi.

Schultz hakutaka kuonekana kwamba amefanya uamuzi huo peke yake, kwa hivyo alitaka uratibu na washirika, haswa Marekani . Ndiyo maana kuna uwezekano kwamba kutakuwa na tangazo kabla ya mkutano wa Rammstein kesho.

Hata hivyo, msimamo wake ulizusha mfadhaiko na kulaaniwa katika duru za kimataifa za kisiasa na kiusalama.

Jumuiya ya usalama ya kimataifa inasema Ujerumani lazima itimize majukumu yake ya kijeshi