Nini cha kufanya kwanza unapoumwa na nyoka, ili kuokoa maisha?

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Karibu 300% ya nyoka wote duniani wana sumu, na katika 50% ya visa vya nyoka wanaowauma binadamu huwa hawaachi sumu mwilini
Muda wa kusoma: Dakika 4

Karibu 300% ya nyoka wote duniani wana sumu, na 50% ya visa vya nyoka wanaowauma binadamu huwa hawaachi sumu ndani ya mwili wakati wa wanapomuuma binadamu. Kwa hivyo ni karibu visa 15 kati ya 100 ya nyoka ambapo muathiriwa huhitaji matibabu.

Unaweza pia kusoma:

Nini cha kufanya ukiumwa na nyoka ili kuokoa maisha?

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Unapoumwa na nyoka mwenye sumu, matibabu ya haraka na sahihi ni muhimu ili kuokoa maisha ya mtu

Kulingana na Shirika la Afya Duniani, kuumwa na nyoka wenye sumu kunaweza kusababisha kupooza, kupumua kwa shida, na wakati mwingine kukatwa kiungo ni hatua muhimu ikiwa sumu itaenea sana.

Mbali na hili, iwapo sumu ya nyoka itaenea zaidi mwilini na iwapo myu aliyeumwa na nyoka hatapoea matibabu anaweza pia kufariki , kwahiyo hatua zingine zinapaswa kuchukuliwa mara moja wakati unapoumwa na nyoka.

Nini cha kufanya wakati unaumwa na nyoka?

  • Unapoumwa na nyoka, kwanza hakikisha kuwa mtu aliyeumwa na nyoka na anayempatia huduma yuko mbali na nyoka. Usijaribu kumkamata nyoka.
  • Mtazame kwa mbali nyoka na ujaribu kukumbuka anakaaje, hii itasaidia kuwa rahisi kutibiwa wakati wa kupelekwa hospitali.
  • Ikiwa umevaa mapambo, saa, mkufu au vitu vingine kulipokuwa eneo la ulipoumwa na nyoka, ondoa.
  • Usikimbie baada ya kuumwa na nyoka, kaa kimya iwezekanavyo na ikiwezekana usimruhusu aliyeumwa kutembea.
  • Ita gari ikupeleke kwenda hospitali mara moja bila kupoteza muda, ili maisha ya mtu yaweze kuokolewa.
  • Kama inawezekana, kumbuka wakati tukio la kuumwa na nyoka lilipotokea na dalili gani zilifuata.
  • Unapofika hospitalini, kwanza mpe daktari maelezo ya jinsi nyoka alivyoonekana na kilichotokea.

Nini isichotakiwa kufanya wakati wa kuumwa na nyoka?

  • Usiweke bandage kwa nguvu sana wakati umeumwa na nyoka. Hata kama bandage imefungwa, inapaswa kulegezwa kidogo.
  • Ikiwa bandeji imefungwa kwa nguvu sana, sumu inaweza kuenea hadi sehemu ambayo nyoka amekuuma, na sehemu hiyo ya mwili inaweza kukatwa.
  • Baada ya kuumwa na nyoka, songa kidogo iwezekanavyo. Harakati nyingi zinaweza kusababisha sumu kuenea haraka katika mwili.
  • Usimpatie dawa yoyote ya mitishamba au dawa nyingine isiyojulikana mtu ambaye ameumwa na nyoka.
  • Usimpe kinywaji cha aina yoyote muathirika wa nyoka.
  • Mtu akianza kutokwa na damu, na kuongezeka kwa kiasi cha mkojo, akipata uvimbe kwenye eneo alipoumwa na nyoka, ukushindwa kupumua, maumivu ya kifua na dalili za kupooza, mpeleke hospitali mara moja.

Je, kuua nyoka au kutumia barafu kunaondoa sumu?

Wakati unaumwa na nyoka mwenye sumu, matibabu ya wakati na sahihi ni muhimu ili kuokoa maisha ya mtu.

Katika hali nyingi, kifo au uharibifu wa kudumu wa kimwili unaweza kutokea ikiwa hautibiwi mara moja au ikiwa hautapata matibabu sahihi. Kwa hivyo usisikie au kutumia njia zingine za matibabu ya kuua nyoka, kutumia barafu au hata mbinu nyingine za kijadi zinazopendekezwa.

Nini cha kuzingatia zaidi unapoumwa na nyoka?

f

Chanzo cha picha, Getty Images

  • Usijaribu kunyonya sumu kutoka kwa mtu aliyeumwa na nyoka
  • Usikate sehemu ya mwili iliyoumwa na nyoka ili kutoa sumu
  • Usiende kwa mganga wa kienyeji
  • Usimpe kamwe dawa za nyumbani mgonjwa aliyeumwa na nyoka
  • Usijifunge nyoka kujiuma yenyewe
  • Usisafishe wala kupaka barafu kwenye sehemu iliyoumwa na nyoka
  • Usijaribu kumshika au kumuua nyoka, kumuua nyoka hakuondoi sumu

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, watu wanaofanya kazi katika kilimo na watoto ni waathirika wakubwa wa nyoka. Watoto ndio walioathirika zaidi na sumu ya nyoka.

Visa vya nyoka kwa ujumla hupatikana duniani kote, lakini kiwango cha vifo katika visa kama hivyo ni kikubwa katika nchi za Kusini-Mashariki mwa Asia ikiwa ni pamoja na India.

Kulingana na ripoti ya serikali ya India, matukio ya nyoka ni ya kawaida zaidi katika vijiji na maeneo ya miji. Katika India, Bihar, Jharkhand, Bengal Magharibi, Madhya Pradesh, Odisha, Uttar Pradesh, Andhra Pradesh, Telangana, Rajasthan na Gujarat ni zaidi ya kukabiliwa na nyoka.

Kuna aina zaidi ya 250 za nyoka nchini India, kati ya hizo nyoka 52 ni nyoka wenye sumu. Nyoka wenye sumu wanaopatikana nchini India ni wa aina nne: krait na cobra, viper, na nyoka wa baharini .

Kati ya spishi 60 hadi 62 zinazopatikana Gujarat, ni aina nne tu za nyoka ambao ni hatari kwa binadamu. Nyoka wanne , nag ( cobra ya India), karnataro (krait ya India), khadchitalo (Russell's viper) na furso (saw scale viper), ndio wanaohusika na vifo vingi vya nyoka nchini India.

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi na kuhaririwa na Ambia Hirsi