Yafahamu mashindano haya ya kuua nyoka na njia rahisi ya kumuua

Chanzo cha picha, GLADES BOYS
Katika muongo mmoja tangu Florida ilipoanzisha shindano lake la kwanza la mauaji ya nyoka wa Burma, maelfu ya watu kutoka Marekani na duniani kote wameshiriki katika kuua nyoka.
Jake Waleri, mwenye umri wa miaka 22, ana mpango mmoja tu mkubwa kwenye likizo yake, nao ni kuwinda nyoka.
Kijana huyu kutoka mji wa Naples katika jimbo la Florida alisema kuwa huwa anafuatilia masuala ya wanyamapori na tatizo wanalokuwa nalo kwenye mazingira ya asili ya Florida.
Alivutiwa na uwindaji wa nyoka baada ya kuwatazama kwenye televisheni wataalam wa kuwinda nyoka wakikamata nyoka.
Alianza kuwinda nyoka miaka miwili iliyopita. Mwaka jana, aliingia katika Mpango unaojulikana kama Florida Python Challenge - shindano la kila mwaka la uwindaji wa chatu - lakini alishindwa kuendelea kwa sababu alikuwa chini ya viwango kwa mujibu wa tathmini.
"Mwaka huu nataka kushinda," alisema.
Mamia ya watu katika jimbo la Florida hushiriki kila mwaka katika shindano la kitaalamu la kutega nyoka.
Baadhi ya washiriki wanatoka Canada, Ubelgiji na Latvia, na wote walivutiwa na zawadi nono ya dola $30,000.
Miongoni mwa washindi wa hivi karibuni wa shindano hili ni mwalimu wa sayansi katika shule ya 'walemavu wasiosikia' ambaye alimshika nyoka mwenye urefu wa futi 16 kwa mikono yake na kujishindia dola $10,000.
Wahifadhi wa ndani wanasema mashindano haya ni muhimu ili kupunguza tishio la nyoka Florida.
Sasa, watu wanaruhusiwa kuua nyoka wakati wowote na mahali popote wanapoona nyoka, na hauhitaji kibali cha kumuua nyoka.

Chanzo cha picha, FLORIDA FISH & WILDLIFE
Sheria ya Uwindaji wa Jabisada
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Sheria ya kushiriki Shindano ni kwamba, washiriki lazima walipe dola $25 na kushiriki programu ya mafunzo ya dakika 30, ambayo inalenga kuwafundisha jinsi ya kutambua kwa usahihi nyoka na kuwaua kwa haraka.
Kwa kuwa ni kinyume cha sheria kusafirisha nyoka akiwa hai bila kibali maalum, wawindaji wengi wa nyoka lazima wawaue nyoka wanaowaona kabla ya kuwafikisha kwenye kituo rasmi cha kuwapima.
Njia ya kuua ambayo wataalamu wanapendekeza inaitwa "double-pithing" na hufanyika kwa kumpiga nyoka kichwani, kwenye uti wa mgongo na kuharibu ubongo. Pia inaruhusiwa katika baadhi ya maeneo kumuua nyoka kwa kutumia risasi.
Kutambua nyoka kwa usahihi ni muhimu. Kuwaua nyoka wengine mbali na chatu kutasababisha ushindwe shindano hilo, alisema Bi Segelson, mmoja wa waandaji wa shindano hilo.
"Kwa upande mwingine, ni marufuku kuua nyoka jike ambaye anaweza kutaga takriban mayai 100 kwa mwaka.
Haijulikani ni athari gani ya mauaji haya yaliyoidhinishwa na serikali yameleta kwenye mfumo wa ikolojia wa Everglades kwa sababu wataalam wanasema haiwezekani kujua ni wangapi waliosalia.
Lengo la shindano hili ni kupunguza idadi ya nyoka hao katika jimbo la Florida.
Wanyamapori kama vile mbweha na wanyama wengine ambao walikuwa wengi katika eneo la Everglades kusini mwa Florida sasa wamepungua.
Chatu janga Florida

Chanzo cha picha, Getty Image
Chatu waliokomaa katika eneo hilo huwa na urefu wa kati ya futi 6 na 9, maafisa wa wanyamapori wanasema, lakini baadhi yao ni wakubwa zaidi.
Jake Waleri, mwenye umri wa miaka 22, aliweka rekodi ya chatu mkubwa zaidi wa Kiburma aliyekamatwa Florida mapema katika msimu wa joto. Alimshika nyoka huyo mwenye urefu wa futi 19 na uzito wa kilo 57 katika Hifadhi ya Big Cypress National Preserve mnamo Julai 10 na kupambana naye alipojaribu kumng'ata.
Mwaka jana, mwindaji wa chatu Marcia Carlson Pack alimshika chatu mwenye urefu wa futi 15 akiwa amemeza mamba tumboni mwenye futi 5, aliambia BBC.
Pack ni mwanachama wa kundi la uwindaji la wanawake wote la Everglades Avenger Team, na huwawinda nyoka hao mwaka mzima, lakini hashiriki katika shindano hilo.
Mashindano ya mwaka huu yameanza Agosti 4 na yatamalizika Agosti 13, 2023 na mshindi ni yule atakayekamata nyoka wengi na atajizolea dola $10,000 wa pili dola $7,500.
Mwaka jana, shindano hilo lilivutia washiriki zaidi ya 1,000 kutoka majimbo 32, Canada na Latvia, Lisa Thompson, msemaji wa Tume ya Uhifadhi wa Samaki na Wanyamapori ya Florida, alisema katika barua pepe kwenda kwa CBS News.
Jumla ya chatu 231 ambayo ni rekodi walinaswa katika mashindano ya mwaka jana.














