Mambo 9 usiyoyafahamu kuhusu nyoka

Snake

Chanzo cha picha, Getty Images

Nyoka ni mojawapo ya viumbe wa zamani zaidi wanaoishi duniani kwa mamilioni ya miaka. Mwezi Julai kila mwaka (Julai 16) huadhimishwa kama Siku ya Nyoka Duniani.

Je! ni simulizi gani tunazo kuhusu nyoka? Je! una ukweli gani kuhusu viumbe hivi? Je, ni kweli nyoka hucheza wanaposikia sauti fulani? Je, nyoka huuma? Nini cha kufanya ikiwa nyoka amekuuma?

Pamoja na yote haya ni mambo tisa muhimu kuyafahamu kuhusu nyoka.

Nyoka anasikiaje?

Snake

Chanzo cha picha, Getty Images

Kuna kauli kwamba mtu anayeweza kusikia sauti ndogo za chini inasemekana ana masikio ya nyoka. Hii haina maana kwamba nyoka wana masikio. Kwa kweli, nyoka hawana masikio yanayoonekana kwa nje. Lakini utafiti umeonyesha kuwa kuna mifumo inayohusiana na masikio katika miili yao.

Lakini kwa kuwa hawana masikio kama ya wanadamu, hawawezi kusikia sauti moja kwa moja.

Ngozi ya nyoka inapogusa ardhi wakati anatambaa, muundo wa mfupa wa kochlear huchukua mawimbi ya sauti yanayosafiri ardhini na kufikia sikio. na hapo ndipo anaposikia.

Kama hawasikii moja kwa moja, wanawezaje kucheza?

Snake

Chanzo cha picha, Inpho

Maelezo ya picha, Nyoka wakichezeshwa ngoma India

"Ukweli ni kwamba kupitia mitetemo ardhini sauti zinafikia kwenye mwili wa nyoka, hivyo anaitikia na kufanya alichofundishwa ( kwa wale nyoka wanaocheza ngoma)," anasema mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Andhra, India Manjulata, alipozungumza na BBC.

Wananusa kwa kutumia ulimi

Nyoka wanatumia ulimi kunusa... Nyoka wanaweza kuona rangi mbili tu kwa macho yao. Lakini nyoka hawapepesi macho. Kwa sababu hawana kope. Lakini wana safu inayofanana na lenzi inayoitwa 'eyecap'.

Wakati nyoka anapozaa, safu hii juu ya macho yote pia hutoka na kuja mpya. Wanyama hawa wenye damu baridi, wana ulimi unaowasaidia kugundua uelekeo na harufu ya chakula.

Nyoka wanakasirika?

Snake

Chanzo cha picha, Getty Images

Watu wengi wanafikiri kwamba nyoka wana hasira. Filamu nyingi zimetengenezwa kuakisi hilo.

Ukweli ni kwamba nyoka hana kumbukumbu nzuri. Hana uwezo wa kuhifadhi kumbukumbu. Hajaumbwa kuuma binadamu, mashambulizi mengi ya nyoka ya kumuuma mtu yanatokea kama akihisi tu hayuko salama, anahisi maisha yake yako hatarini.

Nyoka hatafuni

Nyoka hawawezi kutafuna chakula chao. Na wanaweza pia kumeza wanyama wakubwa kuliko vichwa vyao. Muundo wa taya zao unafaa kwa hilo.

Nyoka wote wanang'ata

Pinjeri

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha, Pinjeri hupatikana katika nchi nyingi hasa Afrika na Asia

Nyoka wote wanauma. Lakini sio nyoka wote wanaouma wana sumu. Wakati mwingine nyoka wenye sumu huuma lakini wasitoe sumu. Nyoka wapo wakundi mawili. Aina mojawapo ni ile yenye sumu kali kama neurotoxic inayoathiri mfumo wa neva na mfumo wa kupumua.

Aina nyingine ya nyoka wasio na sumu. Wanatumia meno yao kuwinda na kushambulia. Aina hii ya sumu ya nyoka kawaida huharibu tishu za ngozi na kusababisha kutokwa na damu kwa ndani.

Nyoka hatari zaidi duniani ni hawa

Cobra

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Cobra ni miongoni mwa nyoka hatari na wenye sumu duniani

Wako nyoka ambao wakikung'ata wanaua, Pinjari mwenye sura ndogo (nyoka mwenye msumeno) ni mojawapo ya nyoka hatari zaidi. Wanapatikana katika sehemu nyingi duniani kuanzia Afrika Magharibi hadi bara Hindi. Huuma zaidi gizani.

Wengine ni Katla pamu: Nyoka huyu huonekana mkali wakati wa mchana na hushambulia kwa fujo sana usiku.

Damu Cage (Russell's Viper): Huyu ni nyoka mwenye ukali wa kawaida. Anapatikana kote India na Asia ya Kusini. Cobra / Cobra (Indian Cobra) : Cobra hupatikana karibu duniani kote katika bara Hindi.

Wanashambulia zaidi gizani. Husababisha damu kuganda kwa ndani. King Cobra / Rachanagu / Kalinda: Ni nyoka mrefu kuliko wote. anaweza kufikia urefu wa hadi futi 20.

Miongoni mwa nyoka wenye sumu duniani, nyoka huyu ndiye anayetema sumu nyingi zaidi anapokuuma mara moja. Anatema sumu ujazo wa 10mil hadi 20 ml ya sumu anapokung'ata mara moja. Sumu yake ina athari kali kwenye mfumo wa neva.

Nini kitatokea nyoka wakitoweka duniani?

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Kutoweka kwa nyoka kutasumbua usawa wa maisha wa viumbe. Tayari nyoka wanawindwa kwa ajili ya chakula na biashara katika nchi nyingi. Bidhaa zilizotengenezwa kwa ngozi ya nyoka zinahitajika sana.

Huko India Kusini, watu wa kabila la Ilaru mara nyingi hukamata nyoka na kuuza ngozi zao.

Huko Tamil Nadu, shirika linalofanya kazi za uhifadhi wa nyoka, linaloongozwa na mtaalamu wa heptologist aitwaye Dk. Romulus Whitkar, linaendesha programu za uhamasishaji kwa ajili yao. Watu wanaokamata nyoka hulipwa, sumu huvunjwa kutoka kwa nyoka na kurudishwa tena porini. Hivi ndivyo wanavyolindwa.

Mambo gani ya kufanya uking'atwa na nyoka?

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Nini cha kufanya na nini usifanye ikiwa nyoka akikuuma? vitu vya kufanya Wataalam wa matibabu wanapendekeza kutafuta matibabu mara moja.

Usijajiribu kukamata nyoka kama huna utaalamu huo kwa sababu nyoka wengi hawapendi kubugudhiwa.