Iran: 'Tulinunua mfumo wa rada kutoka nchi rafiki, lakini hawakuuwasilisha'

.

Chanzo cha picha, screenshot

Maelezo ya picha, Bw. Hajizadeh alisema: “Hatuwezi kusubiri matakwa ya wageni
Muda wa kusoma: Dakika 3

Amir Ali Hajizadeh, kamanda wa Kikosi cha Wanaanga cha IRGC nchini Iran , alisimulia habari katika kipindi cha Televisheni ya Iran, ambapo moja ya nchi rafiki za Iran ilikataa kuwasilisha rada ilizoiuzia Iran.

Bw. Hajizadeh alisema: "Tulipokuwa hatuna rada, tuliamua kununua rada kutoka kwa moja ya nchi zinazozalisha rada, ambayo ni rafiki wa Iran." Kama kamanda wa ulinzi, nilinunua mifumo saba ya rada kutoka kwao."

Akibainisha kuwa muuzaji alikataa kupeleka mifumo iliyonunuliwa kwa hatua tofauti kwa sababu mbalimbali, alisema: “Hatimaye, baada ya majadiliano ya siku nyingi, nchi hiyo rafiki haikutuletea mfumo wa rada, licha ya kupata malipo ya mapema. "

Katika hotuba yake, kamanda huyu wa IRGC hakutaja jina la "Nchi Rafiki" na historia ya tukio hili, lakini alisema baada ya kutembelea mitambo ya kiwanda hicho nchini humo, walifanikiwa kujenga mfumo wenyewe kwa kutumia “picha”.

Bwana Hajizadeh alisema katika kipindi hiki kilichorushwa hewani na idhaa ya Khabar: "Hatuwezi kuwa chini ya sera za watu wengine. Hatuwezi kusubiri matakwa ya wageni. Yaani ikiwa utashi wao umeegemezwa juu ya hili, watatufanyia kitu sisi, na ikiwa sivyo, hawatafanya hivyo."

Maneno yake yaliwakumbusha wengi habari kuhusu ununuzi wa mfumo wa kulinda anga wa Urusi wa S-300; Tukio ambalo lilisababisha ukosoaji mwingi wa sera ya kigeni ya Iran kwa Urusi

Pia unaweza kusoma
..

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mwaka 2009, Urusi ilisitisha kuwasilisha mifumo iliyonunuliwa ya S-300 kwa Iran kwa sababu ya vikwazo vya kimataifa

Mwaka 2007, mkataba wa dola milioni 800 ulitiwa saini kati ya Iran na Urusi, ambapo Urusi ilipaswa kuwasilisha mfumo wa hali ya juu wa kuzuia makombora ya angani (S-300) kwa Iran.

Lakini Urusi ilisitisha utoaji wa mifumo iliyonunuliwa mwaka 2010 kutokana na vikwazo vya kimataifa dhidi ya Iran.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Lakini mwaka huo huo, mfumo unaofanana sana na mfumo wa S-300 ulionyeshwa kwenye gwaride la jeshi la Iran.

Wakati huo huo, baadhi ya vyombo vya habari vya Kiarabu viliripoti kwamba Iran ina mfumo wa kiasili sawa na mfumo wa S-300.

Farzad Esmaili, kamanda wa wakati huo wa Kituo cha Ulinzi wa Anga cha Khatam al-Anbiya alitangaza jina la mfumo huu wa kiasili kama "Imani ya 373".

Baada ya makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na nchi za Magharibi, Rais wa Urusi Vladimir Putin aliondoa marufuku ya uwasilishaji wa mfumo wa makombora ya S-300 mnamo Machi 2015.

Hatimaye, mnamo Oktoba 2015, shirika la habari la Sputnik la Urusi, likitoa mfano wa tangazo la Shirika la Usafirishaji wa Silaha la Jimbo la Urusi, lilitangaza kwamba Moscow imekamilisha mchakato wa kuwasilisha mifumo ya makombora ya ulinzi wa anga ya S-300 kwa Tehran kulingana na mkataba.

Amir Ali Hajizadeh anahesabiwa kuwa mmoja wa makamanda wakuu wa kijeshi wa Iran kutokana na hatua za mpango wa makombora wa Iran, na licha ya mabadiliko ya amri ya Walinzi wa Mapinduzi, ameshikilia msimamo wake tangu 2007.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Seif Abdalla