Gautam Adani: Kutoka kuacha masomo hadi kuwa mtu tajiri zaidi wa Asia

Chanzo cha picha, Getty Images
Usiku wa tarehe 26 Novemba 2008,Gautam Adani, wakatii ule akiwa mtu wa 10 tajiri zaidi nchini India, alikuwa akila chakula cha jioni katika mgahawa wa kifahari wa hoteli ya Mumbai -Taj Mahal Hotel wakati alipowakuwa na watu wenye silaha wakiingia kwa nguvu na kufyatua risasi kila upande na kulipua grunedi.
Wanajeshi kumi waliokuwa wamejihami kwa silaha nzito, wote rai awa Pakistan , walikuwa wamewasili kwa njia ya bahari, wakajigawa katika makundi, wakateka magari na kushambulia maeneo, ziliwemo hoteli za kifahari.
Mashambulio hayo yaliyodumu kwa musa was aa 60 yaliwauwa watu 166 na kuharibu uhusiano baina ya India na Pakistan.
Bwana Adani baadaye aliliambia jarida la India - India Today kwamba mhudumu wa hoteli alikuwa mhudumu wa hoteli alikuwa amepeleka haraka chakula katika eneo la chini ya jengo kwa saa kadhaa, na akawahamishia kwenye ukumbi kwenye gorofa la juu wakati makabiliano yalipokuwa yakiendelea nje ya hoteli.
Kulikuwa na wageni 100 waliokuwa wamejaa katika ukumbi - "baadhi wamejificha chini ya vitu vya sofa, na wengine wakiwa wamejikunja" – wakiomba kwa ajili ya maisha yao.
Bw Adani alielezea kwamba alikuwa ameketi kwenye kiti cha sofa, akiwaambia wageni waliokuwa wamekwamba kuwa "Imani kwa Mungu", na alipiga simu kwa familia yake iliyokuwa na wasi wasi katika mji wa kwao wa Ahmedabad, zaidi ya kilomita 500 (maili 310) mbali , huku dereva wake na mlinzi wake wakimsubiri nje ya gari.
Baada ya kukaa kwa usiku mzima ndani ya ukumbu huo wa hoteli, Bw Adani na mateka wengine waliondolewa nje kupitia lango la nadra baada ya makomandoo kuizingira hoteli asubuhi iliyofuata." Niliona kifo kwa umbali wa futi 15 pekee ," aliwaambia waandishi wa habari baada ya kurekea Ahmedabad kwa ndege yake ya kibinafsi.

Chanzo cha picha, Google
Miaka 14 baadaye, Bw Adani mwenye umri wa miaka 60, ni mtu wa tatu tajiri zaidi duniani – baada ya Elon Musk na Jeff Bezos. Anaendesha biashara ya mkusanyiko wa bandari za nishati na ma makampuni yanayoendesha biashara kwa , wafanyakazi 23,000 employees na soko lenye hisa ya thamani ya zaidi ya dola bilioni 230 (£190bn).
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Amekuwa katika taarifa za habari wiki hii kwasanany anakaribia kununua shirika la habari linaloheshimika sana nchini India la NDTV, katika kile kinachoonekana kama ni uwekezaji mkubwa katika sekta ya habari.
Muda mrefu kabla ya kukatiza masomo yake alipokuwa shule ya sekondari awe mfanyabiashara, alikuwa bilionea ambaye alikuwa na mwenye hamu ya mabadiliko kwa njia hatari.
Januari 1998, yeye na mshirika wake waliripotiwa kutekwa nyara kwa kikombozi kutoka kwenye gari lake na kikundi cha watu katika Ahmedabad.
Washukiwa wawili waliachiliwa huru katika mwaka 2018 baada ya mfanyabiashara na mshirika wake "kushindwa kujitokeza kwa ajili ya kuhojiwa licha ya kuitwa mara mbili na mahakama". Bw Adani huwa hazunguzi kuhusu matukio haya sana.
Baada ya kukatiza masomo alipokuwa na umri wa miaka 16, Bw Adan alihamia mjini Mumbai kujaribi kufanya biashara, akiuza almasi katika wilaya yenye shughuli nyingi za biashara.
Kuingia kwake mapema katika biashara hakukudumu kwa muda mrefu: miaka miwili baadaye alirudi Gujarat, jimbo la kwao, kuendesha kiwanda cha usindikaji kilichokuwa cha kaka yake.

Chanzo cha picha, AFP
Bw Adani, ambaye anatoka katika familia ya kipato cha kati ya wafanyabiashara wa nguo, hakuwahi kamwe kurudi nyuma baada ya kuanzisha kiwanda chake mwaka 1998, akiuza bidhaa.
Kwa zaidi ya miaka 24 baadaye, makampuni yake yaliyoimarishwa na madeni yaligeuzwa kuwa ya bandari, madini, leri, miundo mbinu, paw ana makazi na kumfanya kuwa mtu ambaye alielezewa kama "labda mtu mwenye bidi zaidi katika kizazi kipya cha matajiri wa India".
Leo, bila shaka , Bw Adani ni tajiri wa miundo mbinu nchini India. Anamiliki kampuni ya saruji ya pili ukubwa zaidi nchini India, bandari 13 – ikiwemo bandari kubwa zaidi iliyopo kwenye mwambao wa magharibi ya mji wa Mundra – na anamiliki viwanja saba vya ndege. Anajenga leri ndefu zaidi ya mwendo kasi baina ya Delhi na Mumbai, mji mkuu wa nchi .
Akiwa na viwanda sita vya nishati ya makaa ya mawe, Bw Adan ni mtu binafsi wa pili anayemiliki sehemu kubwa ya nishati ya India.
Wakati huo huo, ameahidi kuwekeza dola bilioni 50 katika nishati ya kijani hydrogen na kutengeneza bomba la gesi asilia lenye urefu wa kilomita 8,000. Pia alinunua mgodi wa makaa yam awe katika nchi za Indonesia na Australia. Analenga kuwa mmiliki mkuu wa nishati mbadala duniani kufikia mwaka 2030.
Kasi na kiwango cha kupanuka kwa utajiri wa Bw Adani kulilinganishwa na makampuni makubwa ya viwanda katika enzi zilizopita, aliandika James Crabtree, mchambuzi wa sera katika kitabu chake The Billionaire Raj:

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika safari yake ya utajiri, Bw Adani alikabiliwa na utata. Uhusiano wake wa karibu na Waziri Mkuu Narendra Modi, kwanza wakati wa muhula wake kama waziri kiongozi wa Gujarat na sasa kama waziri mkuu wa India, uliwafanya wakosoaji kuiita himaya ya biashara yake kama mfano wa ubepari wa uliotokana na kujuana na viongozi wa serikali.
Mgodi wa makaa yam awe unaomilikiwa na Adani katika Queensland ulikuwa gumzo kuu kwa wanaounga mkono na na wanaopinga makaa yam awe na alilazimika kusubiri kwa muda wa miaka kadhaa kuundesha kusubiri idhini za wanamazingira kabla ya ujenzi wake kuanza mwaka 2019.
Mwaka 2012, mkaguzi wa mali ya serikali wa India alimshutumu Bw Modi, aliyekuwa waziri kiongozi wa Gujarat wakati huo , kwa kutoa maguta ya bei ya chini kutoka kwenye kampuni inayoendeshwa na taifa kwa Bw Adani na wafanyabiashara wengine.
Mwandishi wa habari aliandika msururu wa taarifa katika mwaka 2017 akisema kampuni za Bw Adani zilipendelewa huku Bw Modi akitazama bila kuchukua hatua, Kampuni za Bw Adani na serikali ya Bw Modi walikanusha madai hayo mara kwa mara.
RN Bhaskar, mwandishi kuhusu maisha ya Bw Adani, anasema "uwezo wake wa kujenga na kuimarisha mahusiano" ulisaidia katika ukuaji wa biashara zake. Ni rafiki na "viongozi na wanasiasa" wengi wa matabaka mbali mbali.
Mradi wa Bw adani wa bandari katika Kerala auliidhinishwa wakati chama kikuu cha upinzani cha Congress pkilipokuwa madarakani na Wakomunisti, ambao sasa wanaongoza taifa, wameuunga mkono.
Bw Bhaskar anasema kile kinachomfanya Bw Adani ajitokeze miongoni mwa watu wengine wanaofanya biashara saw ana zake ni "utashi wake wa kuongeza fedha kwa kuwekeza katika shughuli za umma ".
La muhimu zaidi, aliongeza, Bw Adani anaamini kwamba ukuaji unauhakika wakati mtu anapoweka maslahi ya kundi la biashara "yanapokaribiana na maslahi ya kiaifa". Hili halishangazi , falsafa ya kampuni zake , kama ilivyoainishwa kwenye wavuti , ni kwamba "Ujenzi wa Taifa" unaochochewa na "Ukuaji wa Wema ".















