Jeff Bezos: Mtu tajiri zaidi duniani ni mtu wa aina gani?

Jeff Bezos: Mtu tajiri zaidi duniani

Utajiri wa Jeff Bezos ambaye ndiye mmiliki wa kampuni ya mauzo ya bidhaa ya mtandao ya Amazon unakadiriwa kuwa ni takribani dola bilioni $171bn (£137bn), ambapo ameweza kutengeneza mabilioni ya pesa wakati wa janga la Covid-19 .

Jeff Bezos hata anamipango ya kukipeleka kizazi cha binadamu katika anga za mbali.

Yafuatayo ni mambo 5 unayofaa kuyajua kuhusu Jeff Bezos;

Jeff Bezos

Chanzo cha picha, Getty Images

1/Akiwa mtoto

Akiwa na umri wa miaka mitatu tu, alianza kupata uwezo usio wa kawaida kwa watoto. Moja ya mambo ya ajabu aliyoyafanya ilikua ni kutengenisha kitanda ambacho wazazi wake walimnunulia na kukifanya kuwa sawa na kitanda cha mtu mzima .

Alikua na ujyzi wa kiuhandizi akiwa na umri mdogo, ambapo alitengeneza alamu iliyowazuwia ndugu zake wadogo kuingia chumbani kwake.

Mashine hiyo ilimuwezesha kutambua pale wadogo zake walipoingia chumbani kwake.

Jambo moja ambalo hatalisahau ni jinsi alipomwambia mama bibi (nyanya) yake miaka aliyoipoteza katika maisha yake kwa kuvuta sigara. Bezos alikua na umri wa miaka 10 tu wakati huo

Baadae hilo lilimtia hofu kwasababu ilimfanya bibi yake alie kwa huzuni.

Bezos anasema babu yake alimvuta pembeni akamwambia, ''siku moja utatambua kwamba ni vigumu kuwa mkaribu kuliko kuwa na busara yako ."

Umma unamtambua Bezos kama mtu anayejali akili kuliko ukarimu.

2/Bezos anapenda hesabu kujua faida anayoipata

Anapotaka kuwaajiri wafanyakazi huyo wa Amazon huwauliza maswali ya watahiniwa wanaotafuta kazi katika kampuni yake, ni alama gani wangepata na kuendelea kuongeza kiwango cha alama za mtihani wa kazi.

Huku vipaji katika Amazon vikiongezeka, wanaopata alama za chini hufutwa kazi.

Katika kampuni ya Amazon, wafanyakazi wamekua wakilalamika juu ya muda wanaotumia kutembea kwenda msalani na kituo cha shughuli za kielektroniki wakidai wanachunguzwa.

Pia kuna vijfaa vya utambuzi vinavyopima kiwango cha kazi ambacho kila muajiriwa amekitumia kufanya kazi kwa siku nzima.

3/ Hufanya mambo kwa namna yake ya kipekee

Zamani kabla hajawa mtu maarufu, Bwana Bezos alikua na biashara yake ya kibinafsi ambayo aliiendesha kwa mtindo ambao watu wengine waliuona kuwa sio wa kawaida.

Mwaka 1994, alifungua duka la kwanza la vitabu kwenye gereji ya nyumbani kwao.

Na sasa ameainisha baadhi ya mipango yake ya kuendesha biashra yake binafsi

Hupenda kuandika waraka mrefu uliofaa taarifa kabla ya kufanya mkutano na wafanyakazi wake.

Ana tabia na anayoiita "kuwadhibiti wateja wate". Inafahamika vyema kwamba yeyote mwenye malalamiko miongoni mwa wafanyakazi wake kumuhusu Bezos anaweza kumueleza kwa kumtumia barua pepe moja kwa moja

"Anwani yangu ya barua pepe ni [email protected], inafahamika , na sijawahi kuificha kamwe ."

Wakati Bezos anapoona malalamiko yaliyotumwa na mtu fulani, hutuma barua pep kwa mmoja wa wafanyakazi wake, ambapo huweka alama ya kuuliza.

Hii inamaanisha kwamba mfanyakazi wake anayehusika na jambo hilo ataweka kila kitu kando na kutatua tatizo lililoelezewa katika barua pepe.

Jeff Bezos akiwa na mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman

Chanzo cha picha, Getty Images

4/ Benzos na siasa

Mwaka 2018, Rais Donald Trump alimshutumu Jeff Bezos kwa uhalifu kama ukwepaji wa kodi na kujaribu kufanya vitendo ambavyo ni kinyume na ushindani wa kibiashara.

Hii ilisababisha kuanguka kwa hisa za biashara yake kwa takriban 9%, na kushuka kwa pato lake kwa kiwango cha dola bilioni $10, lakini baadae biashara yake ikaendelea kunawiri .

Senata Bernie Sanders pia alipitisha muswada wa sheria dhidi ya Amazon uliojulikana kama sheria ya "Stop the Bezos"

Senata Sanders alimkosoa Bwana Bezos kwa namna anavyoendesha biashara, akisema kwamba wafanyakazi wa Amazon ni maskini sana hawawezi kutengeneza faida.

Matokeo yake Bwana Bezos ameongeza mshahara wafanyakazi wa Amazoni hadi kufikia dola $ 15 kwa kila saa.

Jeff Bezos na Elon Musk

5/Bezos ana mipango mikubwa kwa ajili ya anga za mbali

Bezos anawekeza mabilioni ya dola kila mwaka katika kampuni Blue Origin ambayo inapanga kupeleka binadamu katika anga za mbali na hata sayari nyingine .

" Hii ni kazi muhimu zaidi ambayo nimewahi kuifanya .Nilipokua na umri wa miaka mitano mwanaanga Neil Armstrong alitua mwezini, na tangu wakati huo nilipanga mawazo yangu kwamba lazima nivumbue anga na hata niende huko," alisema.

Tangu alipokua shule ya sekondari Bezos alianza kufikiria ni jinsi gani anaweza kubadili maisha ya binadamu katika dunia hii na maeneo yanayoizunguka.