Tetesi za soka Ulaya Jumapili 08.09.2024

Erling Haaland

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Mshambuliaji wa Manchester City Erling Haaland, 24, anakaribia kukubaliana na mkataba mpya ambao utamfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi. (Marca)

Mkataba mpya wa Haaland unatarajiwa kuwa na kipengele cha kutolewa ambacho kinaweza kufikiwa na Real Madrid ikiwa wanataka kumsajili katika siku zijazo. (Mail)

Real Madrid wanalenga kumnunua mlinzi wa kati wa Arsenal na Ufaransa William Saliba, 23. (Fichajes)

Meneja wa Newcastle United, Eddie Howe anafikiria kumnunua winga wa Manchester United na Brazil Antony, 24, ikiwa dili la mshambuliaji wa Nottingham Forest na Uswidi Anthony Elanga, 22, halitatimia. (Caught Offside)

Newcastle itajaribu kumsajili mlinzi wa Crystal Palace Marc Guehi, 24, katika mkataba wa bei nafuu mwezi Januari wakati atakuwa amebakiza miezi 18 katika mkataba wake, lakini The Eagles wataendelea kushikilia hesabu yao ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza. (Football Insider)

Marc Guehi

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambuliaji wa Bayern Munich, Jamal Musiala, ambaye anaivutia Manchester City, hajakataa kuhamia Ligi ya Premia. Mkataba wa sasa wa winga huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 21 utakamilika Juni 2026. (Welt Am Sonntag, via Goal)

Beki wa Ujerumani Jonathan Tah, 28, anasema hataongeza mkataba wake wa Bayer Leverkusen ambao utaendelea hadi msimu wa joto wa 2025, na anathibitisha kuwa Bayern Munich walikuwa miongoni mwa vilabu vilivyotaka kupata saini yake msimu wa joto. (90 min)

Jonathan Tah

Chanzo cha picha, Getty Images

Leverkusen huenda ikalazimika kumuuza Tah kwa bei iliyopunguzwa wakati wa usajili wa majira ya baridi ili kumzuia beki huyo wa kati kuondoka bure mkataba wake utakapokamilika msimu ujao wa joto. (Fichajes ), nje

Kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot ni mchezaji huru baada ya kuondoka Juventus, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 hana nia ya kuhamia katika klabu moja nchini Uturuki. (Fabrizio Romano)

 Adrien Rabiot

Chanzo cha picha, Getty Images

Leverkusen huenda ikalazimika kumuuza Tah kwa bei iliyopunguzwa wakati wa usajili wa majira ya baridi ili kumzuia beki huyo wa kati kuondoka bure mkataba wake utakapokamilika msimu ujao wa joto. (Fichajes )

Kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot ni mchezaji huru baada ya kuondoka Juventus, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 hana nia ya kuhamia katika klabu moja nchini Uturuki. (Fabrizio Romano)