Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi: Arsenal yawasilisha ombi la kumsajili Liam Delap

Muda wa kusoma: Dakika 2

Arsenal imewasilisha ofa kwa wawakilishi wa mshambuliaji wa Ipswich na Muingereza Liam Delap, 22, huku wakitafuta njia ya kusajili mshambuliaji pamoja na chaguo la uzoefu zaidi na lililothibitishwa. (Football Transfers)

The Gunners pia wameongeza juhudi katika mazungumzo ya kuongeza mkataba wa beki wa Ufaransa William Saliba, ambaye amekuwa akihusishwa tetesi za kuelekea na Real Madrid. (L'Equipe, via Get French Football News)

Mustakabali wa mlinda lango wa Argentina Emiliano Martinez, 32, katika klabu ya Aston Villa uko shakani, huku klabu hiyo ya Midlands ikipania kumsajili kipa mpya katika usajili la majira ya kiangazi. (Mail)

Liverpool iko tayari kumuuza beki wa Ugiriki Kostas Tsimikas, 28, msimu huu. (Football Insider)

Klabu za Arsenal, Manchester United na Chelsea ziko mbioni ya kumnunua mshambuliaji wa Bayer Leverkusen kutoka Jamhuri ya Czech Patrik Schick, 29, msimu huu wa kiangazi. (Caught Offside)

Chelsea na Liverpool zinaongoza katika mbio za kumsajili beki wa Bournemouth na Uhispania Dean Huijsen, 20. (Teamtalk)

Al-Hilal inasubiri jibu kutoka kwa kocha wa Inter Milan Simone Inzaghi kuhusu Muitaliano huyo kuwa meneja wao mpya na, klabu hiyo ya Saudi Pro huenda ikamsajili Marco Silva wa Fulham wakimkosa Simone. (Talksport)

Beki wa Uingereza Lloyd Kelly, 26, amefikia idadi inayohitajika ya mechi kubadilisha uhamisho wake wa mkopo kutoka Newcastle United kwenda Juventus kuwa wa kudumu. (Calciomercato - kwa Kiitaliano), nje

Mmiliki wa Napoli Aurelio de Laurentiis amekuwa akiwasiliana na kocha wa zamani wa Juventus na AC Milan Massimiliano Allegri kwa lengo la kumsajili endapo Antonio Conte ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu. (Tutomercatoweb - kwa Kiitaliano)

Manchester United inamfuatilia mchezaji wa Italy mwenye umri wa miaka 25 na mshambuliaji wa Fiorentina Moise Kean. (Footmercato - kwa Kiitaliano)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi