Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumatano: Al-Hilal inavutiwa na Bruno Fernandes
Klabu ya Al-Hilal ya Saudia inajiandaa kuwasilisha dau la kumnunua nahodha wa Manchester United Bruno Fernandes, lakini Mashetani hao wekundu hawana mpango wa kumuuza kiungo huyo wa kati wa Ureno mwenye umri wa miaka 30. (Mail)
Newcastle inamfuatilia mlinzi wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Jonathan Tah, 29, ambaye anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo mkataba wake utakapokamilika msimu wa kiangazi. (Sun)
Kiungo wa Liverpool Muingereza Harvey Elliott, 22, anawaniwa na vilabu kadhaa vya Ligi ya Premia, ikiwa ni pamoja na Wolves. (Talksport)
Real Madrid haina mpango wa kumsajili kiungo wa Real Sociedad Martin Zubimendi. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania, ana kipengele cha kumuachia cha €60m . (OK Diario - kwa Kihispania)
Kiungo wa Italia Jorginho, 33, amepiga hatua katika mpango wa kujiungana klabu ya Brazil Flamengo bila malipo mkataba wake na Arsenal utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu. (Mail)
Arsenal inafikiria kuwasilisha ofa nyingine ya kumsajili kiungo wa Paris St-Germain Lee Kang-in, 24, baada ya kumkosa mchezaji huyo wa kimataifa wa Korea Kusini mwezi Januari. (Sun)
Kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Florian Wirtz, 22, anatazamiwa kuzima nia ya Manchester City na Real Madrid ili kujiunga na Bayern Munich. (Bild - kwa Kijerumani), nje
Kipengele cha kuachiliwa kwa mshambuliaji wa RB Leipzig Benjamin Sesko ni zaidi ya pauni milioni 80 lakini vilabu vinaweza kumsajili kwa bei nafuu vikiwasilisha ofa inayofaa kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Slovenia mwenye umri wa miaka 21. (Sky Sports Ujerumani)
Arsenal imefufua nia ya kumsajili winga wa West Ham na timu ya taifa ya Ghana Mohammed Kudus, 24. (Talksport)
Federico Chiesa, 27, huenda yuko njiani kuondoka Liverpool msimu huu wa kiangazi huku klabu za AC Milan na Napoli zikimtaka winga huyo wa Italia. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)
Manchester United imemjumuisha kipa wa Torino Mserbia Vanja Milinkovic-Savic mwenye umri wa miaka 28 kwenye orodha yao fupi ya uhamisho wa majira ya kiangazi. (Givemesport)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi