Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumanne: Manchester United yatangaza bei ya Garnacho
Manchester United imeiambia Chelsea kwamba italazimika kulipa pauni milioni 65 ili kumsajili winga wa Argentina mwenye umri wa miaka 20 Alejandro Garnacho msimu huu wa kiangazi. (Star)
Klabu za Everton na Wolves zina nia ya kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Nicolas Pepe, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 29 akitarajiwa kukamilisha mkataba wake na klabu ya Villarreal msimu wa kiangazi. (Foot Mercato - in French)
Winga wa Ujerumani Leroy Sane, 29, amebadilisha wakala wake, jambo ambalo limeibua swali kuhusu mustakabali wake katika klabu ya Bayern Munich na kuongeza mkataba ambao ulikaribia kuafikiwa. (Sky Sports in Germanty)
Beki wa Liverpool anayeondoka Trent Alexander-Arnold yuko tayari kusaini mkataba wa miaka sita na Real Madrid ambao utaanza kutekelezwa Julai mosi. (Atheletic- Usajili unahitajika)
Alexander-Arnold, 26, alikataa ofa ya nyongeza ya mshahara ili kusalia na Liverpool hadi mwisho wa msimu huu. (ESPN)
Liverpool inatazamiwa kutumia fedha nyingi msimu huu wa kiangazi huku Reds wakiwa mbioni kuwasaka mabeki wapya wa safu ya kushoto na kati pamoja na mshambuliaji. (Sport)
Chelsea inatarajiwa kufanya mazungumzo na kiungo wa Ecuador Moises Caicedo, 23, kuhusu kandarasi mpya msimu huu kama zawadi kwa uchezaji wake mzuri msimu huu. (Telegraph - usajili unahitajika)
Mlinda lango wa Southampton na England Aaron Ramsdale, 26, anawaniwa na klabu za Manchester United na West Ham. (Mirror)
Aston Villa inamfuatilia mlinda lango wa Real Madrid na Ukraine Andriy Lunin, 26, huku mlinda lango wa Argentina Emiliano Martinez, 32, akiendelea kuhusishwa na tetesi za uhamisho wa majira ya kiangazi. (Birmingham Mail)
Meneja wa Fulham Marco Silva na mkufunzi wa Nottingham Forest Nuno Espirito Santo ni miongoni mwa wagombea wanaowaniwa na klabu ya Saudi Pro League Al-Hilal. (Sport )
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi na kuhaririwa na Ambia Hirsi