Viongozi waliochanjwa chanzo ya corona moja kwa moja kwenye televisheni

Picha za viongozi wa Afrika

Rais Ghana Ghana Nana Akufo-Addo amepokea dozi ya kwanza ya chanjo ya Covid-19 ya kwanza nchini humo Jumatatu, kama ishara kwa umma ya kuwathibitishia raia kwamba chanjo ni salama.

Inaaminiwa kuwa, viongozi wanapata chanjo hiyo wazi mbele ya umma kuonesha uongozi na jukumu la uwajibikaji katika kueneza imani katika chanjo ni jukumu lao.

Ingawa WHO inasisitiza kuwa njia fupi zimetumiwa katika kutengenezwa na kuidhinishwa kwa chanjo, hii haijatosha kuwashawishi baadhi ambao wanasema chanjo zimeharakishwa, kwahiyo si salama.

Akufo-Addo amepuuzilia mbali uvumi wa propaganda uliotolewa na baadhi ya Waghana kuwa chanjo hizo zinawea kubadili vinasaba (DNA) binafsi vya mtu ; wengine wanahofia kuwa dozi hiyo ilitengenezwa kwa ajili ya kuwamaliza Waafrika , ripori ya Modern Ghana inasema.

Nana Akufo-Ado

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nana Akufo-Ado amepokea chanjo ya Covid -19 Jumatatu

Tarehe 21 Disemba 2020, hata kabla ya urais wake kuwa rasmi, rais wa mteule wa Marekni wakati huo, Joe Biden, alipokea chanjo ya Corona moja kwa moja kwenye kipindi cha televisheni kumuonyesha kila mtu kwamba alikuwa pale na "hakuna la kuhofia".

Na viongozi wengine muda mfupi walifuata nyayo-kama vile Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahuna Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman.

Haikuchukua muda kabla viongozi wa Afrika kuanza kupewa chanjo kupitia 'televisheni moja kwa moja'

Hebu tuangalie wale ambayo tayari wamefuata njia hii :

Ushelisheli

Rais Wavel Ramkalawan alikua kiongozi wa kwanza wa Afrika kupokea chanjo ya corona

Chanzo cha picha, STATE HOUSE SEYCHELLES/FACEBOOK

Maelezo ya picha, Rais Wavel Ramkalawan alikua kiongozi wa kwanza wa Afrika kupokea chanjo ya corona

Rais Wavel Ramkalawan aliandika historia tarehe 10 Januari mwaka 2021 wakati alipokuwa kiongozi wa kwanza wa Afrika kuchanjwa huku watu wakimtazama wakati huo huo.

Rais wa Uselisheli alichukua chanjo iliyotengenezwa nchini Uchina-Sinopharm kuanzisha mwanzo wa mpango wa nchi hiyo wa chanjo.

Afrika Kusini

Katika moja ya miji masikini zaidi nchini humo, tarehe 17 Februari, Rais Cyril Ramaphosa alipokea chanjo yake katika hospitali ya Khayelitsha - hospitali ya umma - akionyeshwa moja kwa moja kwenye televisheni.

Rais Cyril Ramaphosa alipokea chanjo yake katika hospitali ya umma

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Rais Cyril Ramaphosa alipokea chanjo yake katika hospitali ya umma

Kwa njia ile, rais alitumia jiwe moja kuwauwa ndege wawili: Kuonyesha kwamba chanjo ya virusi vya corona ya Johnson & Johnson ni salama na kwamba ni sawa kwenda katika hospitali ya umma kupokea chanjo ya corona.

Baadae Ramaphosa alituma ujumbe wa Twitter kusema "ulikua wa haraka, rahisi na usioumiza ".

Zimbabwe

Sio rais kwanza, Mr Emmerson Mnangagwa tarehe 18 Februari alisema "ninakushukuru'' Makamu wa rais Constantino Chiwenga ambaye alipewa chanjo ya kwanza ya corona nchini akionyeshwa moja kwa moja kwenye televisheni.

Haijawa wazi ni kwanini Rais Mnangagwa alitoa jukumu la kitendo muhimu cha kupata chanjo kwa Makamu wake, lakini labda ni kwasababu ya majukumu mawili aliyonayo Bw Chiwenga kama waziri wa afya na kwa hiyo alikuwa na jukumu la kufanya hivyo.

Senegal

Magharibi mwa Afrika, Rais Macky Sall alipokea chanjo ya Sinopharm, iliyotengenezwa na Uchina katika kasri la rais tarehe 25 Februari.

Macky Sall

Chanzo cha picha, MACKY SALL / TWITTER

Hakuwa mtu wa kwanza kuipokea nchini mwake, hatahivyo, wakati kampeni rasmi ya chanjo ilianza siku kumi mapema huku watu zaidi ya 4000 wanachanjwa, yeye ndiye anayekuwraia wa kwanza wa Senegal.

Taarifa zaidi kuhusu virusi vya corona:

Morocco

Nfalme Mohammed wa VI alizindua mpango wa chanjo Februari 28 akiwa mtu wa kwanza nchini humo kupatiwa chanjo ya Covid-19 katika kasri la ufalme.

Morocco, ni moja ya mataifa yenye mpango mkubwa zaidi wa kitaifa wa chanjo

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Morocco, ni moja ya mataifa yenye mpango mkubwa zaidi wa kitaifa wa chanjo

Wizara ya afya ilikuwa imeeleza bayana kuwa wahudumu wa afya, usalama, na waalimu pamoja na watu wenye umri wa kuanzia miaka 75, watafuatia kupokea chanjo hiyo .

Nchini Nigeria, ilitarajiwa kwa kiasi kikubwa kwamba Rais Mahammadu Buhari, pia atakuwa mgtu wa kwanza kupata dozi ya chanjo ya Covid-19 ambayo itawasili nchini humo Jumanne tarehe 2 Machi.

Dkt Faisal Shuaib, ambaye ni mkuruhgenzi mkuu wa shirika la maendeleo ya huduma za kimsingi za afya (NPHCDA) alisema kuwa rais ana mpango wa kupata chanjo yake huku akionekana moja kwa moja kwenye televisheni kama njia ya kuwatia moyo Wanaigeria kupata chanjo hiyo.

Chanjo hiyo ina patikana chini ya mpango wa COVAX, ambao pia umesambaza chanjo kwa matiafa ya Ivory Coast na Ghana.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video, Covax vaccine scheme: What is it and how will it work?