Virusi vya corona: Marekani yabaini dozi moja ya Chanjo ya Johnson and Johnson inatosha

Vaccine

Chanzo cha picha, Getty Images

Taasisi ya udhibiti wa viwango vya dawa na chanjo nchini Marekani inasema dozi moja ya chanjo ya Johnson and Johnson ni salama

Hii inatoa njia kwa chanjo hiyo kuwa ya tatu ya Covid-19 kuidhinishwa nchini Marekani, huku kukiwa na uwezekano wa chanjo hiyo kuanza kutumiwa katika siku za hivi karibuni.

Chanjo hiyo itakuwa na bei nzuri ikilinganishwa na chanjo za Pfizer na Moderna na inaweza kutunzwa katika friji ya kawaida badala ya kutunzwa ndani ya friji za barafu.

Majaribio ya chanjo hiyo yamebaini kuwa inazuia kuugua sana lakini ilikuwa na ufanisi wa ujumla wa 66% wakati wagonjwa wanaogua kiasi walipojumuishwa.

Kampuni imekubali kutoa dozi milioni 100 kwa Marekani kufikia mwishoni mwa mwezi Juni. Uingereza, Muungano wa Ulaya na Canada zimekwisha agiza dozi milioni 500 kupitia mpango wa Covax kwa ajili ya kusamabaza chanjo hiyo kwa mataifa masikini zaidi.

Data za majaribio ya chanjo hii zinaeleza nini ?

Waraka wa maelezo uliochapishwa na taasisi ya Matekani ya udhibiti wa viwango vya dawa na chakula FDA, unatoa maelezo ya kina zaidi ya data yaliyowasilishwa na Janssen, kitengo cha kampuni ya madawa ya Johnson & Johnson, kwa wasimamizi wa viwango. FDA ilisema kuwa chanjo ya Johnson & Johnson ina "faida zinazojulikana " katika kupunguza virusi visivyosababisha mtu kuugua pamoja na vile vinavyomsababishia muathiriwa kuugua sana

Hii inakuja baada ya kampuni hiyo kutangaza data za majaribio yake ya chanjo mwezi uliopita.

Matokeo yalitokana na majaribio yalifanywa matika mataifa ya Marekani, Afrika Kusini na Brazil ambapo yalibaini kuwa chanjo hiyo ina ufanisi dhidi ya matokeo mabaya ya virusi vya corona "ambayo ni ya hali ya juu " lakini kwa ujumla kinga ilikuwa ya chini katika nchi za Afrika Kusini na Brazil, ambako aina mpya za virusi zimejitokeza kwa wingi.

Data zinaonesha kuwa ina uwezekano wa zaidi ya 85% ya ufanisi katika kuzuia ujgonjwa, lakini kwa ujumla ina ufanisi wa 66% wakati visa vya ugonjwa wa kadri vinapojumuishwa, kwa kuzingati pale hivyo vinapodumu kwa muda wa walau siku 28 baada ya chanjo.

Kilichobainika ni kwamba hakuna vifo vilivyojitokeza miongoni mwa washiriki wa jaribio la chanjo hiyo ambao waliipokea na hakuna aliyelazwa siku 28 baada ya kupewa chanjo hiyo.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video, Covax vaccine scheme: What is it and how will it work?

Nini kinakachotokea sasa?

Kamati ya ndani ya wataalamu itakutana siku ya Ijumaa kushauri juu ya ikiwa FDA inapaswa kuishinisha chanjo, na huenda ikaongezwa kwenye chanjo zinazotolewa nchini Marekani .Marekani itakuwa ni nchi ya kwanza duniani kuidhinisha chanjo hiyo.

Afisa wa Ikulu ya White House alisema kuwa utawala wa nchi hiyo unapanga kugawa walau dzi milioni tatu za chanjo ya Johnson & Johnson wiki ijayo, iwapo itapokea idhinisho kutoka kwa FDA.

Kampuni hiyo inasema kuwa inapanga kusambaza dozi milioni 20 kwa jumla ifikapo mwezi Machi, kulingana na makubaliano ya kusambaza chanjo hiyo Marekani itatoa dozi milioni 100 kufikia mwezi Juni.

Sio tu kwamba chanjo hiyo itahitaji dozi chache tu kuliko ile ya Pfizer and Moderna inayohitaji mtu kupewa dozi mbili, Johnson and Johnson itawawezesha wanaochanjwa kwenda hospitali mara chache, wahudumu wa chanjo watakuwa ni wachache wa kutoa huduma ya chanjo.

Ni akina nani wengine walioagiza dozi ya Johnson & Johnson jab?

  • Uingereza - dozi milioni 30
  • Muungano wa Ulaya - dozi milioni 200
  • Canada - dozi milioni38 millioni
  • Mataifa ya Covax - dozi milioni 500

Maelezo ya video, Barakoa mbili: Je tunapaswa kuzitumia?