Virusi vya corona: Zijue habari njema kuhusu corona mwaka mmoja baada ya janga

Ignacio López-Goñi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Janga la Covid-19 pia lilileta habari njema, kulingana na mtaalamu wa vimelea Ignacio López-Goñi.

Mwaka mmoja uliopita niliandika makala juu ya vipengele 10 ambavyo ni taarifa njema juu ya virusi vya corona lengo likiwa ni kuonesha sayansi, ufahamu wa janga hili na ushirikiano ni muhimu katika kukabiliana nalo.

Hatujui kitakachotokea miezi ijayo na virusi vipya ni moja ya sababu ya kutia hofu lakini mwaka mmoja baadaye, ujumbe bado ni ule ule:

1. Kuna makala zaidi ya virusi vya SARS-CoV-2 na Covid-19 kuliko hata ugonjwa wa malaria

Mwaka mmoja uliopita, tulifurahishwa na taarifa kwamba zaidi ya mwezi mmoja tu tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya corona, tayari kulikuwa na majarida 164 ya sayansi yanayoweza kufikiwa na watu kuhusu virusi vipya vya corona.

Leo hii idadi hiyo imeongezeka zaidi ya mara 600 na machapisho hayo sasa hivi yanapita makala 100,000, ikilinganishwa na ya ugonjwa wa "malaria", kwa mfano. Zaidi ya utafiti 4,800 sasa hivi unaendelea juu ya tiba na chanjo ambao umesajiliwa.

2. Kuna chanjo mpya zaidi ya 200

Mwaka mmoja uliopita ilisemekana kwamba kuna majaribio mapya manane ya virusi na chanjo dhidi ya ugonjwa wa virusi vya SARS-CoV-2.

Kulingana na tovuti ya bioRENDER, sasa hivi kuna zaidi ya chanjo 195 huku 71 tayari zikiwa zinafanyiwa majaribio.

Kuna takriban miradi 200 ya chanjo dhidi ya covid-19.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuna takriban miradi 200 ya chanjo dhidi ya covid-19.

Hakujawahi kuwekezwa pesa nyingi kama kipind hiki, ushirikiano wa hali ya juu katika uvumbuzi wa chanjo kati ya mashirika ya umma na serikali, vituo vya utaafiti, vyuo vikuu, makampuni ya kutengeneza dawa na mashirika yasiyo ya serikali.

Baadhi ya majaribio yamefutiliwa mbali lakini kuna yale ambayo yameendelezwa na WHO: Pfizer / BioNTech na Moderna na teknolojia ya mRNA, AstraZeneca / Oxford na Sputnik V teknolojia ya virusi na Sinopharm ya China zikiwa zinaendeleza utafiti wake.

Takriban chanjo 20 tayari zimeingia katika awamu ya tatu ya majaribio na huenda zikaidhinishwa wiki au miezi michache ijayo, ikiwa matokeo yake yatakuwa ya kutosheleza.

3. Chanjo za mRNA ni salama

Moja ya athari kubwa kwa chanjo ni kuweka maisha hatarini kitu ambacho hutokea muda mfupi baada ya mtu kupewa chanjo.

Takwimu za mwezi wa kwanza zinaonesha chanjo zimetathminiwa nchini Marekani ambapo zaidi ya dozi milioni 17.5 zimetolewa.

Na hadi kufikia sasa ni visa kidogo sana ambavyo vimejitokeza dhidi ya chanjo hizo.

Hii inawakilisha chini ya visa 4 kwa dozi milioni ya chanjo zote zilizotathminiwa. Pia hakuna kifo ambacho kimeripotiwa kutokana na chanjo hizo.

Kuna uelewa mkubwa wa kisayansi wa Covid kuliko Malaria

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuna uelewa mkubwa wa kisayansi wa Covid kuliko Malaria

Ikiwa italinganishwa na idadi ya visa vya ugonjwa wa Covid-19 na vifo vilivyotokea, faida ya itakonayo kwa kupata chanjo inakuwa ya juu kuliko ya athari zake.

4. Chanjo zina ufanisi

Israel ni nchi yenye idadi kubwa ya watu ambayo tayari imetoa chanjo. Mapema Februari na tangu kuanza kwa kampeni mnamo mwezi Desemba, zaidi ya watu milioni 3.67 wa Israel wamepokea dozi ya kwanza ya chanjo ya Pfizer / BioNTech mRNA.

Utafiti wa awali unaonesha kuwa chanjo hiyo ina ufanisi.

5. Imani kwa chanjo hizo inazidi kuongezeka

Baada ya dozi zaidi ya milioni 160 ya chanjo dhidi ya virusi vya Covid-19 kutolewa, imani ya watu katika chanjo hizo imeendelea kuongezeka.

Kwa mfano, utafiti uliofanyiwa watu 13,500 kutoka nchi 15 za Ulaya, Asia na Australia ulifanyika kati ya Novemba 2020 na Januari 2021.

Novemba, kabla ya mataifa kuanza kuidhinisha matumizi ya chanjo, asilimia 40 pekee ya waliofanyiwa utafiti ndio wangependa kupata chanjo ya virusi vya corona na zaidi ya asilimia 50 walikuwa na wasiwasi wa athari ya chanjo hizo.

Lakini kufikia Januari, zaidi ya idadi nusu walitaka kupata chanjo na idadi ya watu waliokuwa na wasiwasi wa athari inayoweza kutokea ilikuwa imepungua.

Ongezeko la idadi ya watu inategemea chanjo chidi ya covid-19.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ongezeko la idadi ya watu inategemea chanjo chidi ya covid-19.

6. Kinga dhidi ya virusi unadumu kwa angalau miezi minane

Majaribio ya mfumo wa kinga dhidi ya virusi vya SARS-CoV-2 hayaoneshi uwezo kamili, muda na kumbukumbu ya mfumo wa kinga dhidi ya virusi.

Kujua namna mfumo wa kinga unavyofanyakazi baada ya kupata virusi ni muhimu kutathmini uwezo wa kujilinda dhidi ya maambukizi kwa mara nyingine.

7. Tiba mpya kwa visa vingine ambavyo ni hatari zaidi

Tayari tunajua kwamba ugonjwa wa virusi vya corona ni zaidi ya pneumonia.

Kuna mengi yanayofahamika juu ya ugonjwa huo na ingawa sasa hivi hakuna dawa za kukabiliana na virusi hivyo, kuna machanganyiko wa tiba ambao unaweza kuudhibiti kwa kiasi kikubwa na kupunguza idadi ya wanaofariki dunia.

8. Hakuna mafua

Kulikuwa na wasiwasi mkubwa juu ya ugonjwa wa virusi vya SARS-CoV-2 ukiingiliana na magonjwa mengine ya kupumua.

Hata hivyo ilibainika kwamba ugonjwa wa SARS-CoV-2 unaambatana kwa karibu na magonjwa mengine ya virusi kama vile mafua na matatizo ya kupumua ambayo yanasababisha pneumonia na ndio sababu ya wengi kulazwa hospitali na vifo kwa kundi la watu walio katika hatari ya kupata maambukizi.

Watu waliovaa barakoa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuwajali watu, kwa matumizi ya barakoa na kukaa umbali, imesababisha virusi vingine kama vya mafua kupungua

Athari za virusi vipya vya ugonjwa wa corona huenda visiwe na chanjo makhususi.

Kwasababu mabadiliko ya kijenetiki huenda yakaathiri namna virusi vinavyojiendesha na hivyo basi ni muhimu kufuatiliwa.

Taarifa njema ni kwamba hilo linaweza kufanyika na kujua mabadiliko yanayotokea kwenye virusi husika.

Tunaweza kufuatilia mabadiliko ya ugonjwa huo moja kwa moja

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Tunaweza kufuatilia mabadiliko ya ugonjwa huo moja kwa moja

10. Janga la corona linaendelea kupungua

Hatujui namna janga hilo litakavyoendelea siku zijazo.

Hasa ukizingatia madhara yake siku za hivi karibuni, kuna uwezekano mkubwa kukawa na mawimbi mapya ya virusi hivyo lakini yasiyokuwa na nguvu.

Idadi ya watu wenye virusi vya corona inapungua kote dunian

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Idadi ya watu wenye virusi vya corona inapungua kote duniani

Lakini taarifa njema ni kwamba kiwango cha athari zake kimataifa, zimepungua.

Taarifa zaidi kuhusiana na virusi vya corona:

Maelezo ya video, Barakoa mbili: Je tunapaswa kuzitumia?