Wadudu wa Kombe la Dunia: Maadui wapya ambao hawakutarajiwa

Mwandishi wa BBC Michezo akikabiliana na wadudu katika uwnaja wa dimba la dunia Urusi
Maelezo ya picha, Mwandishi wa BBC Michezo akikabiliana na wadudu katika uwnaja wa dimba la dunia Urusi

Waandalizi wamekuwa wakiweka dawa za kuwazuia wadudu hao bila mafanikio.

Ingawa mashabiki na wachezaji wa Uingereza walikuwa na wasiwasi kuhusu masuala tofauti kabla ya Kombe la dunia, wamekutana na maadui wapya wasiowatarajia - wadudu.

Uingereza itachuana na Tunisia kwenye mechi yao ya kwanza Kombe la Dunia baadaye leo katika jiji la magharibi la Volgograd.

Wadudu hao wamezua usumbufu kwa mashabiki wa Uingereza, wenyeji, na waandishi.

Kikosi cha Uingereza kimeanza kutumia dawa za kuwazuia wadudu hao kabla ya kufanya mazoezi katika uwanja huo.

"Unawakuta usoni, wanakwama mdomoni, kuingia kwenye masikio pua n ahata kwenye nywele," alisema mwandishi wa michezo wa BBC Natalie Pirks.

'Wanafika hata bilioni'

"Kama hali itasalia kuwa jinsi ilivyoshuhudiwa Jumapili, basi wadudu hawa watasababisha usumbufu zaidi," alisema mtangazaji wa Radio 5 live, John Murray.

"Tumetahadharishwa dhidi ya mambo mengi kabla ya kuja Urusi kwa dimba hili, lakini hili halikuwepo."

Uwanja wa Volgograd Arena upo katika kingo za mto Volga ambapo wadudu hao wanatoka

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Uwanja wa Volgograd Arena upo katika kingo za mto Volga ambapo wadudu hao wanatoka

Uga wa Volgograd Arena

Wadudu hawa wametoka kando kando ya mto Volga ambao ndio asili ya wadudu hao.

Msimu wa wadudu kakutana na msimu wa Soka?

Msimu huu wa mwezi Juni unafahamika kuwa msimu wa wadudu hao kuzaana na kukua kwa haraka.

Baadaye wadudu hao huondoka na kuingia mjini ambapo wanasababisha uharibifu.

Profesa Adam Hart wa chuo kikuu cha Gloucestershire anasema huenda mbu wakachanganyika na wadudu hao wanaoitwa chironomidae. Wadudu wenyewe hawana madhara makubwa.

Organisers said the flies are a "typical phenomenon for Volgograd in June due to the local climate" and claim the "insignificant amount of flying insects will not disrupt any of the scheduled events in Volgograd".

Mamlaka zimewajibika vipi?

There are four group games in Volgograd itaandaa mechi nne na waandilizi wanasema wamekuwa wakipuliza madawa kweneye maeneo ya michuano kutumia dawa za kuwafukuza wadudu.

"Tumeweka mikakati ya kuwapunguza wadudu hao na tumefaulu," ofisi ya mawasiliano Volgograd imesema.

Profesa Hart anasema hilo halitasaidia kwani mamlaka haziwezi kuweka dawa kwneye uwanja mzima wenye mashabiki.

Mashabiki wameruhusiwa kuingia na madawa ya kuwazuia wadudu hao uwanjani.

"Shirikisho la soka limesema kuwa daktari wa timu amearifiwa nba wachezaji wataingia uwanjani wakiwa wamejipaka dawa za kuwazuia wadudu hao. Kuna wasiwasi kuwa huenda Kipa akaathirika Zaidi kwnai ndio watakaokuwa wamesimama muda mrefu tofauti na wachezaji wengine watakaokuwa wakikimbia uwanjani."