Katika picha: Jinsi daraja la Gujirat lilivyoporomoka

Morbi

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Daraja hilo lilikuwa limejaa wakati wa ajali, watu waliyokuwa wakisherehekea sikukuu ya Diwali.

Takriban wa 141 wamefariki baada ya daraja la kivuko cha watu kuporomoka katika jimbo la Gujarat magharibi mwa India usiku wa Jumapili.

Idadi kubwa ya waliofariki ni wanawake, watoto na wazee.

Daraja la mto Machchulenye urefu wa mita 230-kuvuka hadi mji wa Morbi lilijengwa mwaka1880, wakati wa utawala wa kikoloni wa Uingereza katika karne ya 19.

Daraja hilo lilifunguliwa wiki moja tu iliyopita baada ya kufanyiwa ukarabati.

Kundi la waokoaji lilitwa pamoja katika juhudi za uokoaji ulioendelea usiku kucha

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Kundi la waokoaji lilitwa pamoja katika juhudi za uokoaji ulioendelea usiku kucha

Mamlaka ziliripoti kwamba kulikuwa na mkanyagano juu ya daraja hilo, jambo ambalo lilisababisha kuporomoka kwake.

Zaidi ya watu 177 wameokolewa, kulingana na mamlaka.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Zaidi ya watu 177 wameokolewa, kulingana na mamlaka.
Daraja hilo lilikuwa limefanyiwa ukarabati

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Daraja hilo lilikuwa limefanyiwa ukarabati
Wengi wa walioathiriwa a wanawake watoto na wazee

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wengi wa walioathiriwa a wanawake watoto na wazee
Shughuli ya kuwatafuta manusura iliendelea hadi Jumatatu.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Shughuli ya kuwatafuta manusura iliendelea hadi Jumatatu.
Mazishi mjini Morbi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mzishi ya baadhi ya waliofariki ilifanyika mjini Morbi mchana wa Jumatatu
line