Katika picha: Jinsi daraja la Gujirat lilivyoporomoka

Takriban wa 141 wamefariki baada ya daraja la kivuko cha watu kuporomoka katika jimbo la Gujarat magharibi mwa India usiku wa Jumapili.

Idadi kubwa ya waliofariki ni wanawake, watoto na wazee.

Daraja la mto Machchulenye urefu wa mita 230-kuvuka hadi mji wa Morbi lilijengwa mwaka1880, wakati wa utawala wa kikoloni wa Uingereza katika karne ya 19.

Daraja hilo lilifunguliwa wiki moja tu iliyopita baada ya kufanyiwa ukarabati.

Mamlaka ziliripoti kwamba kulikuwa na mkanyagano juu ya daraja hilo, jambo ambalo lilisababisha kuporomoka kwake.