Urusi na Ukraine: Kwa nini Ukraine haijathibitisha au kukanusha kuhusika na mashambulizi ya wazi ya Urusi

Chanzo cha picha, Getty Images
Karibu saa 11:50 subuhi ya April 1, kituo cha mafuta kilishika moto katika mji wa Belgorod nchini Urusi, uliopo kilomita 50 kutoka mpaka wa Ukraine.
Video iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii, amnbayo iliyoangaliwa na BBC, ilionyesha kile kilichoonekana kama kombora likianguka katika kituo hicho huku helikopta mbili zikipita, na kusababisha misururu ya milipuko iliyoishi na moto mkubwa.
Baadhi ya ripoti za vyombo vya habari, zilizotokana na kanda zingine za video zinaashiria, kwamba helikomta mbili zilioonekana kama Mi-8 zili paa juu ya miji mingine ndani ya saa kadhaa za milipuko.
Wizara ya kikanda ya Belgorod, Vyacheslav Gladkov iliilaumu Ukraine kwa kushambuli akituo hicho, na muda mfupi baadaye msemaji wa ulizi wa Urusi alisema helikopta mbili za Ukraine aina ya Mi-24 ziliingia kwenye anga ya Urusi kwa mwinuko wa chini sana.na "kuanzisha shambulio la kombora dhidi ya ghala la mafuta- la kiraia" viungani mwa Belgorod.
Haikuwa mara ya kwanza kwa mashambulio y akutiliwa shaka kutokea katika ardhi ya Urusi tangu Rais Vladimir Putin aanzishe uvamizi dhidi ya Ukraine mnamo Februari 24. Siku chache kabla ya Machi 29, milipuko kadhaa ilirepotiwa kwenye ghala la silaha karibu na Belgorod.
Hata hivyo, wakati huu ulikuwa tofauti kwa sababu, kama mwandishi wa BBC wa ulinzi Jonathan Beale anavyoeleza, ikiwa Kiev ilihusika katika mlipuko huo utathibitishwa, ingekuwa mara ya kwanza kwa ndege ya Ukraine kuvuka eneo la Urusi kutekeleza shambulio.
Lakini licha ya tuhuma za Moscow, Kiev haijathibitisha kuhusika na shambulio hilo. Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Oleksandr Motuzyanyk alisema "uchokozi" wa Urusi ulikuwa unakabiliwa "katika eneo la Ukraine".

Chanzo cha picha, Getty Images
Unaweza pia kusoma
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
Ajali au shambulio?
Tangu wakati huo, visa kadhaa vinavyotiliwa shaka vimeripotiwa katika ardhi ya Urusi.
Mnamo April 25, kwa mfano, mji wa Bryansk, uliopo kilomita t 150 kaskazini mwa mpaka wa Ukraine, uliamkia anga nyeusi kufuatia moto uliokumba bomba kubwa la mafuta. Gavana wa kikanda wa Aleksandr Bogomaz aliripoti poto huo lakini hakuelezea chanzo chake.
Pia kulitokea milipuko karibu na mitambo ya kijeshi ya Urusi na hata katika taasisi ya utafiti wa kijeshi katika jiji la Tver, karibu na Moscow.
Hakuna anayejua idadi kamili ya mashambulio hayo, lakini vyombo vya habari vimeripoti makumi ya matukio kama hayo.
"Yalitokea katika maeneo tofauti ya nchi katika vituo ambavyo kawaida huhusishwa na jeshi na vituo vingine vya uzalishaji wa kimkakati, kwa hivyo inaonekana dhahiri kuwa milipuko hii sio ya bahati mbaya," Matthew Orr, mchambuzi aliyebobea katika Eurasia huko Rane, mshauri wa uchambuzi wa hatari za kijiografia, katika mahojiano na BBC Mundo, Idhaa ya BBC ya lugha ya Kihispania.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wachambuzi wanaamini kuwa baadhi ya matukio haya huenda yalisababishwa na ndege zenye nguvu za Bayraktar zilizotengenezwa Uturuki ambazo Ukraine inazo na kwamba, katika hali nyingine, zinaweza kuwa shughuli za upekuzi za vitengo vya kijasusi vya nchi hiyo ndani ya ardhi ya Urusi.
Hata hivyo, Kiev haijathibitisha wala kukanusha kuhusika kwake katika matukio haya. Kwa nini?
utata wa kimkakati
Maadisa katika serikali ya Volodymyr Zelensky ilikwepa kufafanua wanachojua kuhusu matukio haya, lakini ilionyesha kuridhishwa kwao.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ukraine Anton Gerashchenko pia alirejelea matukio haya, lakini kwa kejeli. Pia kwenye Twitter, alichapisha ujumbe wa "kimajazi" akiambatanisha na picha ya moto wa bohari ya mafuta huko Bryansk.
Hadi sasa, hakuna afisa yeyote wa Ukraine aliyetoa jibu la moja kwa moja kuhusu matukio haya yaliyoangaziwa na Oleksei Arestovych, mshauri wa mkuu wa wafanyakazi wa Zelensky.
"Hatuthibitishi wala kukanusha. baada ya kile kilichotokea, kirasmi hatusemi ndio au la, sawa na Israel," Arestovych alisema katika mahojiano ya hivi karibuni na gazeti la Marekani The New York Times, akimaanisha sera ya "utata wa kimkakati". ambayo Israel imedumisha kwa miongo kadhaa kuhusu mpango wake wa silaha za nyuklia.
Kama Matthew Orr alivyoelezea BBC Mundo, Ukraine inapata faida zaidi kwa kudumisha kutokuwa na uhakika juu ya suala hili.
"Inaweza kudhaniwa kuwa baadhi ya mashambulio haya yanafanywa kwa msaada wa ujasusi wa Ukraine na hawaoni haja ya kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu suala hili kwa sababu hawataki Urusi kutumia mashambulio hayo kuhalalisha vita," anasema.
Orr anafafanua kwamba, kwa mtazamo wa habari, ni muhimu zaidi kwa Waukraine kusema kwamba hii haifanyiki na wao, lakini na watu wa Urusi ambao wanaunga mkono hali ya Kiev na ambao wanataka kuhujumu vita vilivyoanzishwa na Putin.
Mtaalam huyo anaongeza kuwa haishangazi kwamba Ukraine inatekeleza hatua katika eneo la Urusi kwa sababu nchi hiyo imekuwa ikifanya kazi kwa miaka mingi kuwa na akili, vyanzo na uwezo huko. "Itakuwa si busara kwao kutotumia rasilimali hizi sasa."

Chanzo cha picha, Getty Images
Tisho la kuongezeka kwa vita
Kujirudia kwa matukio haya kumeghadhabisha Moscow, ambayo ilitishia kulipiza kisasi.
"Jeshi la Urusi liko tayari kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya vituo vya kufanya maamuzi mjini Kiev kwa kutumia silaha zenye uwezo wa hali ya juu," Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilionya wiki iliyopita, ikiishutumu Uingereza kwa "kuchochea" Ukraine kufanya mashambulizi dhidi ya eneo la Urusi.
Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov alishutumu NATO kwa kuendesha "vita visivyo vya moja kwa moja" dhidi ya Urusi na kuonya kwamba silaha zinazotolewa na nchi Magharibi kwa Ukraine "zinalenga" vikosi vya Urusi.
Maafisa walilaumu nchi za magharibi kwa "kuchochea moto" kwa kuipatia Ukraine silaha na kuongeza kuwa mzozo huo unaweza kusababisha vita vya tatu vya dunia.
Lakini je mashambulio dhidi ya ardhi ya Urusi inaweza kuchochea mzozo zaidi?
Wataalamu kama vile Tatiana Stanovaya, mwanzilishi wa shirika la ushauri la uchambuzi wa kisiasa R. Politik, wanaeleza kuwa mashambulizi katika ardhi ya Urusi yanaweza kuongeza uungwaji mkono kwa vita nchini humo.
"Jamii ya Urusi haiko tayari kwa amani. Jamii ya Urusi inatarajia Ukraine kushindwa. Kila kitu kinachotoka Ukraine, kama vile mashambulizi katika eneo la Urusi, huchochea hisia hizi," Stanovaya aliambia gazeti la Marekani la The Washington Post.

Chanzo cha picha, Getty Images
Matthew Orr, kwa upande wake, haamini kwamba matukio haya ni sababu za kuongezeka, ingawa Kiev inakiri kuwa nyuma ya milipuko hii.
"Sidhani kama itakuwa ya kuamua, lakini inaweza kuwa sehemu ya hoja ambayo Urusi hutumia kuongeza mashambulizi; kwa hali yoyote, ni kipengele kingine," anasema.
"Urusi tayari inatumia makombora ya balestiki kuharibu reli, viwanda, barabara, madaraja na kila aina ya miundombinu nchini Ukraine, hivyo itakuwa sawa na Ukraine kufanya jambo lile lile, lakini kwa utulivu na kwa kiwango kidogo. Kwa hiyo, hii itakuwa tu kuchochea kuongezeka kwa mzozo ikiwa Urusi itaamua kuitumia kama hoja ya kuendeleza mashambulizi yake.












