Urusi na Ukraine: 'Vita visivyo moja kwa moja' ni nini na kwanini Moscow inaishtuhumu NATO kuanzisha

Nato imepatia Ukraine mfumo huu wa kupambana na vifaru

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nchi za NATO zimeipatia Ukraine silaha za hali ya juu kama vile mfumo huu wa kupambana na vifaru

Vilikuwa ni "vita moto" vya "Vita Baridi".

Kwa zaidi ya miongo minne, Muungano wa Sovieti na Marekani zilikuwa zikishindana vikali katika nyanja za ushawishi kote duniani bila kukabiliana katika vita vya silaha.

Hiyo haimaanishi kwamba katika nusu karne hiyo hapakuwa na vita kati yao, bali vilitokea kwa ukatili na uharibifu mkubwa, lakini katika maeneo mengine na kupitia wahusika wengine.

Viliitwa "vita visivyo vya moja kwa moja au kwa kimombo proxy wars.

Wiki iliyopita, Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergey Lavrov aliishtumu NATO kwa kuendeleza vita kama hivyo dhidi ya Moscow.

Lavrov alionya kwamba silaha za hali ya juu ambazo nchi za Magharibi zinaikabidhi kwa serikali ya Ukraine zitakuwa shabaha halali kwa vikosi vya Urusi vinavyofanya "oparesheni maalum ya kijeshi," neno linalotumiwa na Moscow katika uvamizi wake dhidi ya Ukraine.

"Mabohari katika maeneo ya magharibi mwa Ukraine yamevamiwa zaidi ya mara moja [na vikosi vya Urusi]. Inawezaje kuwa vingine? NATO, kimsingi, inahusika katika vita dhidi ya Urusi kupitia (mtu wa tatu) na inampa mtu huyo silaha. Vita ni vita," Lavrov alisema katika mahojiano ya televisheni.

Lakini ''vita visivyo moja kwa moja'' ni nini hasa na inamaanisha nini wakati Urusi inapoishtumu NATO kwa kuendeleza vita hivyo?

Mzozo usio wa moja kwa moja

"Vita visivyo moja kwa mija hutokea wakati nchi inapopigana na nchi nyingine, lakini badala ya kutumia wanajeshi wake, inatumia mtu mwingine, inaweza kuwa nchi nyingine, wanamgambo au wababe wa kivita," Daniel Byman, Mhadhiri wa Sera ya Kigeni katika Chuo Kikuu cha Georgetown (USA) na mchambuzi mkuu wa Mashariki ya Kati katika Taasisi ya Brookings aliambia BBC Mundo.

Sergei Lavrov

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lavrov alionya kuwa shehena za silaha za nchi za Magharibi zinazowasili Ukraine ni shabaha halali za vikosi vya Urusi.

Kumbuka migogoro ya aina hii ilikuwa ikitokea mara kwa mara kati ya Marekani na Muungano wa Sovieti katika mfumo wa Vita Baridi wakati, kwa mfano, kulikuwa na wapinzani katika vita vya wenyewe kwa wenyewe katika maeneo kama Somalia au Ethiopia na kila mamlaka kuu iliunga mkono moja wa vita, ili washindane kupata ushawishi kupitia vita hivyo visivyo vya moja kwa moja.

Vita kama hivyo pia vilitokea barani Asia, Mashariki ya Kati, na Amerika Kusini

Vladimir Rauta, Profesa wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Reading (Uingereza), anaonyesha kwamba uingiliaji kati huu unaweza kufanywa kwa njia tofauti.

"Msaada huu unaweza kupatikana kupitia uhamishaji wa silaha, taarifa za kijasusi au ufadhili. Njia ya kawaida ya usaidizi ni kutoa hifadhi, eneo salama," anaiambia BBC Mundo.

"Vita visivyo vya moja kwa moja hutumia njia hizi zote, lakini haipeleki wanajeshi, kwa sababu serikali inapochangia wanajeshi tayari inakuwa uingiliaji wa moja kwa moja wa kijeshi," Rauta anasema.

Madai ya Lavrov kwamba NATO inajihusisha na Ukraine katika mgogoro dhidi ya Urusi yashawahi kutolewa na Leon Panetta, ambaye ashawahi kuwa Wazri wa Ulinzi wa Marekani na Mkuu wa Shirika la ujasusi la Marekani CIA, wakati utawala wa Barack Obama.

"Hivi ni vita vya visivyo moja kwa moja dhid ya Urusi, tuseme au tusiseme," aliambia shirika la habari la Bloomberg katikati mwa mwezi Machi.

Katika mahojiano na BBC Mundo wiki iliyopita, Panetta alielezea msimamo wake kwa kuangazia Marekani na washirika wake wa NATO katika upinzani wao dhidi ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

"Wanafanya kila wawezalo kuhakikisha Urusi inajutia uvamizi huu. Wameweka vikwazo vikali vya kiuchumi dhidi ta Urusi. Wanatoa silaha kwa Uraine ili kuisaidia kukabiliana na wavamizi wa Urusi na pia wanaziimarisha nchi za NATO ili kutangaza wazi kuwa zitapinga uvamizi wowote kutoka kwa Urusi," alisema.

"Ukizingatia kiwango ambacho Marekani na washirika wetu wanafanya kila wawezalo kusaidia Ukraine katika vita vyake dhidi ya Urusi, unaweza kusema kwamba hii ni sawa na vita visivyo moja kwa moja," aliongeza.

Miezi kadhaa kabla ya uvamizi huo, Urusi ilipokusanya wanajeshi wake karibu na mpaka wa Ukraine, nchi za Magharibi zilianza kutuma silaha huko Kyiv.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Miezi kadhaa kabla ya uvamizi huo, Urusi ilipokusanya wanajeshi wake karibu na mpaka wa Ukraine, nchi za Magharibi zilianza kutuma silaha huko Kyiv.

Panetta pia aliangazia matamshi ya hivi karibuni ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin, ambaye wiki iliyopita alisema moja ya malengo ya vita hivi ni kuona Urusi inadhoofishwa.

Kauli hizo ziliibuka katika mkutano na waandishi wa habari nchini Poland ambapo afisa huyo wa Marekani alipoulizwa kufafanua ikiwa malengo ya sasa ya Washington ni tofauti na yale yalivyowekwa mwanzoni mwa uvamizi huo.

"Tunataka Ukraine ibaki kuwa nchi huru, nchi ya kidemokrasia yenye uwezo wa kulinda eneo lake huru. Tunataka kuona Urusi inadhoofika hadi haiwezi kufanya kitendo cha aina hii kwa kuivamia Ukraine," Austin alijibu.

Baada ya kuanza kwa uvamizi wa Ukraine, Bunge la Marekani liliidhinisha msaada dola za milioni 3,500 kwa nchi hiyo, ambazo kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani, zinakaribia kuisha, na serikali ya Biden iliomba msaada mwingine wa dola 33,000 Alhamisi hii ili kusaidia kupigana vita.

Washington imewasilisha risasi na silaha za kila aina, ikiwa ni pamoja na mifumo ya kuzuia ndege na vifaru, helikopta, ndege zisizo na rubani na virusha maguruneti, kwa serikali ya Volodymyr Zelensky.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg, Muungano huo kwa kufikia sasa umetumia zaidi ya dola bilioni 8 za msaada kwa kijeshi kwa Ukraine.

Vita na propaganda

Joe Biden.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Biden aliomba Congress kuidginisha rasilimali zaidi kusaidia Ukraine.

Alhamisi iliopita, Rais wa Marekani, Joe Biden, alipinga wazo kwamba nchi yake au NATO inashiriki katika vita vya visivyo vya moja kwa moja dhidi ya Urusi.

"Sio kweli na inanitia wasiwasi, kwa sababu inaashiria kukata tamaa na Urusi inadhalika kwa kushindwa vibaya na kutoweza kufanya kile ambacho walisema watafanya. Nadhani hasemi ukweli bali anatafuta kisingizio cha kushindwa kwao," alisema.

"Badala ya kusema kwamba Ukraine wana uwezo fulani wa kudhibiti vikosi vya Urusi wanafanya hivi, wanawaambia watu wao kwamba Marekani na NATO zinahusika katika kuondoa wanajeshi na vifaru vya Urusi, na kadhalika."

"Lavrov amekosea kabisa. Marekani na Umoja wa Ulaya wanatoa msaada wa kijeshi na kiuchumi kwa serikali halali ya Ukraine. Hili ni jambo la kisheria kabisa. Ni washirika na washirika wanaosaidiana," mtaalam huyo alisisitiza.

Byman pia alipinga kauli ya Lavrov kwa kuashiria asili ya mzozo huo.

"Urusi ilianzisha vita hivi na NATO inasaidia Ukraine kujilinda. Kwa hivyo sio kwamba NATO ilitaka kupigana na Moscow. Kwa kweli ni vita ambayo Urusi ilianzisha," alisema.

"Inawezekana kwamba Marekani au mataifa mengine yana malengo zaidi ya kuilinda Ukraine," alisema, akiashiriaa matamshi ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin. "Lakini kando na hilo, asili ya mzozo huu sio ule wa vita vya kutumia mtu wa tatu, bali ni uvamizi wa Urusi dhidi ya nchi nyingine ambayo inajilinda kwa msaada wa nchi zingine," aliongeza.

Wote wawili Byman na Rauta walikubaliana kwamba, kwa kutumia mfano halisi unaodhihirika katika jukumu ambalo Moscow imetekeleza nchini Ukraine katika miaka ya hivi karibuni.

"Ikiwa kuna nchi ambayo inaendeleza vita visivyo vya moja nchini Ukraine, ni Urusi, ambayo kutoka 2014 imekuwa ikiwaunga mkono waasi wanaotaka kujitenga kusini mashariki mwa Ukraine. Moscow iliunda hali hii kupitia vita visivyo vya moja kwa moja ambavyo imeanzisha dhidi ya Kiev, Rauta alisisitiza.