Uraibu: Ni nini kinaendelea katika ubongo wetu kinachotufanya tuwe waraibu wa kucheza kamari?

Illustration d'un cerveau jonglant avec des cartes à jouer

Chanzo cha picha, Getty Images

Watu wengi wamegeukia kamari mtandaoni wakati wa janga la corona.

Ingawa wengi wanaweza kucheza kamari kama burudani bila kuwa na madhara makubwa, lakini janga hili limesababisha ongezeko la uraibu wa aina hii ya mchezo.

Uingereza, kwa mfano, imeshuhudia ongezeko kubwa zaidi la idadi ya wanawake wanaotafuta msaada.

Uraibu huu unaweza kusababisha afya ya akili, utambuzi, na matatizo ya uhusiano, na pia kusababisha kufilisika na uhalifu.

Tofauti na ulevi wa pombe na dawa za kulevya, dalili ambazo zinaonekana kwa mwili, ulevi wa kamari una dalili zisizo wazi.

Nakala yetu mpya, iliyochapishwa katika jarida la Lancet Psychiatry, inakagua utafiti kuhusu uraibu wa kucheza kamari na inatoa mapendekezo juu ya njia bora ya kuzuia na kutibu hali hiyo.

Kamari ni tatizo kubwa

Kulingana na makadirio ya hivi karibuni zaidi ya Shirika la Afya Duniani (WHO), katika mwaka wa 2016 hasara ya kila mwaka duniani kote kutokana na wachezaji ilikadiriwa kuwa dola bilioni 400.

Mnamo mwaka 2021, Tume ya Kamari ya Uingereza ilikadiria kuenea kwa ugonjwa wa kulazimishwa wa kucheza kamari katika 0.4% ya watu.

Homme noir sur son téléphone

Chanzo cha picha, Getty Images

Uchunguzi mwingine ulionesha kwamba viwango vya juu zaidi vya tatizo la kucheza kamari vilishuhudiwa huko Asia, ikifuatwa na Australasia na Amerika Kaskazini, zenye viwango vya chini zaidi katika Ulaya.

Watafiti wameunda mfano wa kamari ili kupima uraibu wa kucheza kamari, kama vile 'Iowa Gambling Task' na 'CANTAB Cambridge Gambling Task'.

Ya pili, ambayo inatathmini kufanya maamuzi na kushiriki kamari hatarishi, washiriki wanaulizwa kukisia ikiwa chipu ya manjano imefichwa kwenye kisanduku cha buluu au nyekundu, na uwiano wa masanduku ya bluu na nyekundu hubadilika kwa wakati.

Kisha wanaweza kuamua ni alama ngapi za kuweka kamari kwenye chaguo lao.

Ikiwa ni sahihi, pointi huongezwa kwa jumla lakini ikiwa wanapoteza, pointi hutolewa.

Lazima wawe waangalifu wasije "banduliwa", hiyo ni kusema wasipoteze alama zao zote.

Jukumu hili husaidia kugundua wacheza kamari ambao wako katika hatari ya kupata tatizo la kucheza kamari, lakini ambao huenda hawapo, hasa ikiwa wanaonyesha dalili za kuhamasishwa.

Kupitia programu hizi, utafiti umeonyesha kuwa kamari, kwa watu wenye afya, ni kawaida kati ya watu kati ya umri wa miaka 17 na 27 na hupungua kulingana na umri.

Uchunguzi mwingine uliweka wazi kwamba wacheza kamari walio na matatizo ya uraibu huelekea kuongeza uchezaji wao wa kamari baada ya muda na hatimaye kufilisika.

Uraibu wa pombe na nikotini pia umehusishwa na kulazimishwa zaidi kucheza kamari.

Illustration homme qui a gagné

Chanzo cha picha, Getty Images

Tafiti za ubongo kwa wacheza kamari

Tafiti za Upimaji kwenye ubongo wa mchezaji zinaonyesha wazi kuwa maeneo kadhaa ya ubongo yanahusishwa na kucheza kamari.

Tafiti za Upimaji kwenye ubongo wa mchezaji zinaonyesha wazi kuwa maeneo kadhaa ya ubongo yanahusishwa na kucheza kamari.

Utafiti umeonyesha kuwa maeneo muhimu yanayohusiana na kufanya maamuzi hatari ni pamoja na gamba la mbele la ventromedial (linalohusika katika kufanya maamuzi, kumbukumbu, na udhibiti wa hisia), gamba la mbele la obiti (ambalo husaidia mwili kujibu mihemko) na kizio (ambacho hudhibiti mfumo wa neva).

Kwa hivyo, wenye uraibu wa kucheza kamari wanaweza kuonyesha shughuli nyingi katika maeneo haya.

Wacheza kamari wanapotazama matokeo ya dau lao, wao pia huonyesha kuongezeka kwa uwezeshaji wa ubongo katika mfumo wa malipo wa ubongo.

Na hii inaweza kuwa na nguvu hasa kwa watu walio na uraibu wa kucheza kamari.

Vipitisha habari ambavyo husaidia seli za neva kuwasiliana, pia inajulikana kuwa kemikali muhimu katika mfumo wa malipo ya ubongo.

Utafiti ulionyesha kuwa wenye uraibu wa uchezaji kamari walikuwa na viwango vya juu zaidi vya msisimko wakati vipitisha habari vilipotolewa katika akili zao, ikilinganishwa na watu wenye afya.

Utoaji wa vipitisha habari unaonekana kuongeza shuruti ya kucheza kamari kwa kuongeza viwango vya msisimko, kupunguza vizuizi vya maamuzi hatari, au mchanganyiko wa hayo mawili.

Jetons de pari sur le clavier d'un ordinateur portable

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Watu wengi wameamua kucheza kamari mtandaoni wakati wa janga hili.

Zaidi ya hayo, sehemu ya ubongo ambayo ina jukumu katika mchakato wa utoaji malipo, imeonyeshwa kuhusika katika tabia hatari kwa vijana na watu wazima.

Eneo hili lina dopamini nyingi na linapendekeza jukumu la ziada la dopamini katika tabia hatarishi.

Jinsi ya kushinda uraibu wa kucheza kamari

Hivi sasa, ugonjwa wa uraibu wa kucheza kamari hugunduliwa kwa kutumia mwongozo wa Utambuzi na Takwimu wa Matatizo ya Akili (DSM-5), iliyochapishwa na Chama cha Wanasaikolojia cha Marekani.

Taasisi ya Kitaifa ya Ubora wa Huduma ya Afya ya Uingereza (NICE) pia inatayarisha miongozo ya matibabu na udhibiti wa ugonjwa huu, ambayo itachapishwa mwaka wa 2024.

Chaguzi za sasa za matibabu ni pamoja na aina fulani za tiba ya utambuzi wa kitabia (ambayo inaweza kuwasaidia watu kubadilisha mwelekeo wao wa mawazo) na vikundi vya kujisaidia.

Dawa fulani, kama vile vizuizi teule vya serotonin reuptake (SSRIs), zinaweza kuwa na ufanisi katika kupunguza baadhi ya dalili za ugonjwa wa uraibu wa kucheza kamari, mfano, mfadhaiko.

Pia tunajua kwamba vipokezi vya opioid kwenye ubongo husaidia kuchakata zawadi - na kwa muda mrefu vimeshukiwa kuwa vichochezi vya uraibu.

Tuligundua kuwa kuna ushahidi kwamba dawa inayoitwa Naltrexone, ambayo huzuia vipokezi vya opioid, inaweza kusaidia baadhi ya watu walio na ugonjwa wa uraibu wa kucheza kamari.

Lakini utafiti zaidi unahitajika kabla ya kuwa matibabu ya kawaida.

Pia kuna mambo unayoweza kufanya ili kudhibiti kamari yako.

Tovuti ya Wizara ya afya ya Well ina taarifa kuhusu huduma zinazopatikana kwa wacheza kamari wenye matatizo.

Anatoa ushauri kama vile kulipa bili kabla ya kucheza kamari, kutumia wakati pamoja na marafiki na familia ambao hawachezi kamari, na kushughulikia madeni.

Wachezaji pia watakuwa wenye hekima wakiepuka kuona kucheza kamari kuwa njia ya kupata pesa, kuacha kuhangaikia zoea lao la kucheza kamari, na kuepuka kutumia kadi za mkopo kulipia dau.

Kama ilivyo kwa masuala yote ya afya ya akili, jambo la msingi ni kupata usaidizi na matibabu ya mapema.

Hili ni muhimu hasa ili zawadi za kawaida, kama vile kutumia muda na familia, kwenda matembezini au kufanya mazoezi, ziendelee kuwa za kufurahisha na mfumo wa zawadi "usitekwe" na mchezo.