Urusi na Ukraine: Jinsi mama alivyoshuhudia binti na mumewe wakiuawa na jeshi la Urusi

Viktoria Kovalenko
Maelezo ya picha, Viktoria Kovalenko anakumbuka tukio hilo vizuri

"Kulikuwa na mlipuko, au aina fulani ya risasi. Uliniziba masikio. Kioo cha nyuma cha gari kikapasuka. Mume wangu akapaza sauti kali , 'Toka nje ya gari.'"

Hofu ya siku ile ilikuwa kubwa kuliko unavyoweza kufikiria.

Onyo taarifa hii ina maelezo ya kuogofya ambayo yanaweza kuwatisha baadhi ya wasomaji

Siku tisa ndani ya vita nchini Ukraine, huku mapigano yakiendelea, Viktoria na mume wake Petro walikuwa wameamua hatimaye kuukimbia mji wa Chernihiv, uliopo kaskazini mwa nchi. Walitaka kuwaweka Watoto wao katika hali ya usalama. Veronika mwenye umri wa miaka kumi na miwili alikuwa mtoto wa Viktoria aliyempata katika ndoa yake ya kwanza . Binti yake mwingine Varvara, ana umri wa mwaka mmoja tu.

Walichukua walichokihitaji, na kuondoka kwa gari kwenda mbali na nyumba yao ya familia. Wakati walioondoka viungani mwa mji, wakielekea kusini karibu na kijiji cha Yahidne, waliona mawe yaliyoziba njia yao. Petro aliyavuta, akapanda nje na kuanza kuyaondoa akiyaweka kando ya njia.

Sekunde kadhaa baadaye, gari lao lilimiminiwa risasi.

Viktoria alimuona binti yao Veronika na mume wake wakiuawa mbele yake..

"Nilijaribu kuwa mtulivu, Nilikuwa nimembeba binti yangu mchanga mikononi na nilihitaji kumpeleka mahali salama".

Veronika

Chanzo cha picha, Kovalenko family

Maelezo ya picha, Veronika mwenye umri wa miaka 12-aliuawa alipokuwa akijaribu kutoroka risasi

"Binti yangu mkubwa Veronika alianza kulia, kwasbabu kichwa change kilikuwa kimekatwa upande mmoja na vioo vilivyokuwa vikipaa na nilikuwa ninavuja damu," anasema Viktoria. Huku akiongea, anatuonyesha mfupa wake mmoja wa shavu kwa juu upande wa kushoto wa uso wake, ambapo kuna kovu dogo.

"Veronika alianza kupiga mayowe, mikono yake ilikuwa inatetemeka, kwahiyo nikajaribu kutuliza. Alitoka nje ya gari na akaanza kufuata. Nilipokuwa ninatoka nje ya gari nilimuona akianguka. Nilipotazama kichwa chake kilikuwa kimeenda.

Gari lao lilikuwa limeshambuliwa na kombora la Urusi na kulipuka kwa moto.

"Nilijaribu kuwa mtulivu, nilikuwa nimempakata mtoto wangu mchanga wa kike na nilitaka kumpeleka mahala salama ".

Hakumuona Petro tena, lakini ukimya wake ulimwambia Viktoria kwamba mume wake amekufa pia.

Alikimbia kutoka kwenye gari lililokuwa linaungua. Saa 24 zilizofuatia zilikuwa ni za kung'ang'ana kujaribu kuendelea kuishi.

Viktoria na mtoto wake mchang, walipata hifadhi katika gari lililokuwa limeegeshwa, lakini tena ufyatuaji wa risasi ulianza tena . Alikimbilia kwenye jengo dogo ambalo lilionekana wazi kuwa lilikuwa likitumiwa na wanajeshi. Alipokuwa amejificha hapa, simu yake ikazima kuokoa betri yake, alijiuliza ni vipi angeweza kuulinda usalama wa binti yake.

Siku iliyofuata, waligunduliwa na vikosi vya Urusi vilivyokuwa vikifanya doria. Walipelekwa katika shule katika Yahidne na kutekwa katika chumba cha chini cha jengo.

Mama na mtoto wake mchanga walikaa siku nyingine 24 pale, katika hali mbaya. Viktoria alishuhudia watu wakifariki karibu naye, bila uwezo wa kupata usaidizi wa kimatibabu aliouhitaji. BBC iliweza kutembelea chumba hicho cha maficho, na kuzungumza na watu wengine wanaoshikiliwa pale. Mateka wanaelezea kuhusu miili iliyotapakaa bila kukusanywa kwa saa kadhaa, na wakati mwingine siku kadhaa

Viktoria and Petro Kovalenko

Chanzo cha picha, Kovalenko family

Maelezo ya picha, Petro, ambaye alikufa katika eneo la shambulio, na mke wake Viktoria

Kulikuwa na watu 40 katika chumba, anasema Viktoria , huku kukiwa na sehemu ndogo ya kusonga au kutembea. Hapakuwa na mwangaza, kwahiyo walitumia mishumaa na mianga ya sigara. Kulikuwa na vumbi na joto, na Viktoria anasema watu walihisi vigumu kupumua.

Wakati mwingi watu walikuwa hawaruhusiwi kwenda nje au hata kutumia choo. badala yake walilazimika kutumia ndoo.

"Kutoweza kutembea kwa watu kuliwafanya waugue, waliketi kwenye viti, walilala kwenye viti. Tuliweza kuona mishipa yao, na walianza kutoka damu, kwahiyo tulitengeneza vitambaa vya kuzuia kutiririka kwa damu ," anakumbuka Viktoria.

Ni katika hali hizi Viktoria alianza kufikiria kuuawa kikatili kwa mume wake na binti yake mkubwa. Aliniambia alibakia kuwa mtulivu na kujikaza kadri awezavyo, na kuweka nguvu zake zote katika kuyanusuru Maisha yake na ya mtoto wake aliyebaki.

Lakini aliwaomba watekaji wake Warusi kuuleta mwili wa Petro na Veronika katika shule ili awazike.

Alimtuma mume wake wa zamani, baba yake Veronika kwenye kifusi cha gari ili aweze kuchukua picha za mabaki ya miili yao. Hawakuwa wanatambuliwa kama binadamu.

The Kovalenko family's burned out car

Chanzo cha picha, Kovalenko family

Maelezo ya picha, Gari lao liliungua, na ni vitu vyao vichache pekee vilivyobaikia

Viktoria anakumbuka siku ambayo miili iliwasili .

."Ilikuwa ni tarehe 12 Machi. Waliniita na kusema, 'Twende, na utaona ni wapi watazikwa.' Walizikwa katika msitu, katika makaburi mawili, boksi moja lilikuwa dogo na jingine lilikuwa kubwa. Naishara mbili za misalaba miwili.

"Tulikaa na tukaanza kufunika maboksi kwa udongo, lakini makombora yakaanza, kwahiyo tulitimua mbio kwenda mbali hata kabla ya kumaliza kuwazika. Ilikuwa inatisha sana ."

Viktoria alipoulizwa ni nini angesema kwa watu waliofanya hivi kwa familia yake akajibu: "Ningepewa uwezekano wa kumpiga risasi Putin , ningefanya hivyo ," alijibu. "Mkono wangu usingetetemeka ."

Sasa Viktoria na nd Varvara wako katika eneo salama kiasi la Lviv, magharibi mwa Ukraine. Siku moja kabla ya kufaya mahojiano haya na yeye, alikuwa amefanyiwa matibabu ya kwanza na Mwanasaikolojia . "Ninapokuwa na watu au ninapofanya jambo fulani na kuwasiliana, huwa ninasahau yaliyotokea. Lakini nikiwa peke yangu, Nimepotea ."

Machozi yanamtiririka, kila anapoongea maneno.

Anaonyesha kijisanamu kidogo cha ng'ombe chenye moyo kwenye kifua chake. Ilikuwa ni zawadi aliyopewa na Veronika.

Unaweza pia kusoma