Diamond Platinumz: Akosolewa mitandaoni Marekani kwa kupiga picha ilio na bendera ya 'ubaguzi'

Chanzo cha picha, Diamond Platinumz
Mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platnumz anakosolewa mtandaoni kwa kuangazia bendera ya Shirikisho kwenye kanda yake ya video ya wimbo wake mpya Gidi.
Shirikisho lilikuwa ni kundi la majimbo ya kusini ambayo yalipigana kudumisha utumwa wakati wa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani - na bendera hizo zinaonekana kama ishara ya mivutano ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani.
Moja ya matukio ya picha hizo za Diamond ina bendera mbili zilizoonyeshwa wakati akicheza huku akiwa na muonekano wa Cowboy.
Baadhi ya watumiaji wa Twitter wametoa hisia zao kuhusiana na video ya msanii huyo.
"Bendera ya Muungano katika video yako inasumbua,"aliandika mtumiaji mmoja.
"Bendera ya Muungano?"Clyde Blaise aliandika na kujuumisha emoji ya pipa la taka.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Kufikia sasa Diamond hajatoa tamko lolote kuhusiana na madai hayo.
Diamond ambaye ndiye msanii maarufu zaidi katika eneo la Afrika mashariki hajaepuka migogoro katika siku za hivi karibuni.
Mwaka uliopita msanii huyo maarufu alijipata mashakani miongoni mwa wapenzi wa tuzo za BET.

Chanzo cha picha, Diamond Platnumz
Zaidi ya watu 20,000 walitia saini pingamizi mtandaoni wakitaka wasimamizi wa tuzo hizo kumpiga marufuku mwanamuziki huyo baada ya kuteuliwa kuwania orodha ya mwanamuziki bora wa kimataifa.
Nyota huyo wa muziki wa bongo Fleva alikuwa akituhumiwa na shirika lisilokuwa la kiserikali Change Tanzania kwa kuunga mkono kile kilichodaiwa kuwa uongozi wa kiimla wa aliyekuwa rais wa taifa hilo John Pombe Magufuli.












