Kwanini msisimko wa mwanamke kufikia kilele hutegemea misuli ya nyonga

Chanzo cha picha, Getty Images
Kufikia Kilele katika tendo la ndoa miongoni mwa wanawake ni jambo ambalo limekuwa likizungukwa na imani na hadithi ambazo leo hii zinakataliwa.
Katika hatua hii hakuna shaka kwamba kufikia miongoni mwa kilele wanaume na wanawake, kunatimiza kazi ya kisaikolojia na kifiziolojia kwa wakati mmoja. Pia hakuna mjadala kwamba wanawake wana haki ya kufurahia tendo la ndoa.
Kwa sababu hii, wataalam wa dawa za ngono na wanasaikolojia wanapaswa kueneza ukweli kuhusu msingi wa kibaolojia wa kilele cha mwanamke kwa wanawake wote bila kuzingatia maoni ya mtu kibinafsi.
"Hakuna kitu kama kilele kwenye uke wa mwanamke"
Mfano wazi unapatikana katika neno "kilele kwenye uke wa mwanamke" au "kilele kilichoafikiwa kupitia uke wa mwanamke". Zote mbili mara nyingi hutumiwa kurejelea kilele kilichopatikana wakati wa kushiriki tendo la ndoa bila msisimko wa moja kwa moja.
Lakini ukweli ni kwamba kilele cha uke hakina msingi wa kisayansi, kwa kuwa ni chombo kisicho na hisia. Ushahidi wa jambo hili ni kwamba kwa wanawake wasio na uke wa kuzaliwa), majibu ya ngono ya uke wa bandia yanafanana na yale ya kawaida.
Kinachotokea kwa wanawake wote walio na uke wa kawaida na kwa uke wa bandia ni kwamba misuli hujikaza wakati wa kilele.
Misuli yote miwili iko pande zote za uke.
Je misuli ya nyonga ina uhusiano gani na kufikia kilele?
Udhaifu wa misuli ya nyonga unaweza kuathiri moja kwa moja mahusiano ya ngono. Mara kwa mara, uvujaji wa mkojo unaweza kutokea wakati wa kupenya, wakati wa kilele, au zotembili. Kusonga kwa misuli inayozunguka uke wakati wa kupenya hurahisisha mkojo kuvuja. Inatarajiwa kwamba, baada ya kufanyia mazoezi sakafu ya pelvic, dalili za wanawake hawa zitaboreka.
Kwa kweli, misuli ya sakafu ya pelvik ina jukumu la moja kwa moja kwa kiasi na ukubwa kwa hisia ambazo mwanamke anahisi wakati wa kujamiiana. Pamoja na ukubwa wa mshiko au shinikizo ambalo mpenzi wake anahisi wakati wa tendo la ndoa.
Mikazo ya misuli ya nyonga huchangia msisimko na uwezo wa wanawake wengi kufikia kilele. Mipango ya mazoezi ya misuli ya nyonga inaboresha misuli na viungo vya pelvic. Hii ni muhimu hasa kwa misuli midogo ya misuli ya nyonga, ambayo inachangia kusisimka kwa uke.
Kwa hivyo, kudumisha misuli katika hali nzuri ya nguvu, huchangia ukuzaji wa uhusiano wa kuridhisha wa ngono.
Mazoezi ya viungo na afya ya ngono
Huu ni mfano rahisi tu wa jinsi mazoezi ya viungo yanavyosaidia kutibu matatizo yanayohusu afya ya ngono. Ingawa manufaa ya utumiaji wa masaji ya msamba, utumiaji wa vichocheo laini vya umeme, matumizi ya vyombo kama vile mipira ya Kichina pia yameonyeshwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kama wataalamu wa afya ya jamii, wataalamu wa tiba ya mwili hushiriki katika elimu kukuza afya. Kwa kuwa afya ya kijinsia ni sehemu muhimu ya ustawi wa jumla, wataalamu wa mazoezi ya viungo vya mwili katika viwango tofauti vya utunzaji wana jukumu muhimu .
Ni jukumu la wataalamu kufahamu umuhimu na uzito wa mabadiliko ya kijinsia na kuuliza maswali muhimu kwa wagonjwa walio na dalili zinazoendana na maisha ya kimapenzi.
Pia watoa matibabu lazima watoe mazingira salama na wazi ambapo wagonjwa wanaweza kujisikia huru kujadili mahusiano yao ya ngono.












