Afghanistan: Je, Iran inaelekea kukubali utawala wa Taliban?

Ujumbe wa Taliban

Chanzo cha picha, TWITTER//BILALKARIMI21

Maelezo ya picha, Ujumbe wa Taliban

Siku ya Jumapili, ujumbe wa ngazi ya juu wa kundi la Taliban ulifika mji mkuu wa Iran Tehran kujadili uhusiano wa kiuchumi na Iran na suala la wakimbizi wa Afghanistan.

Huu ulikuwa ujumbe wa juu wa Taliban kufika Tehran tangu Taliban ilipochukua mamlaka ya Kabul mwezi Agosti mwaka jana. Waziri wa Mambo ya Nje wa Taliban Amir Khan Mottaqi aliongoza ujumbe huu wa jumuiya ya Kiislamu.

Katika ziara hiyo, viongozi wa Taliban pia walikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hussein Amir Abdullahiyan, pamoja na viongozi kadhaa wa Afghanistan wanaopinga Taliban. Msemaji wa Taliban alisema mkutano wa Mottaqi na viongozi wa Iran ulikuwa "chanya na wenye kujenga".

Tangu walipoingia madarakani, hakuna nchi iliyotambua utawala wa Taliban kufikia sasa. Lakini ni mojawapo wan chi chache ambazo zimeshauriana na kufanya biashara na kundi hilo.

Kulingana na Iran, kwa sasa haina mpango wa kutambua serikali ya mpito ya Taliban. Lakini ziara ya Mottaqi mjini Tehran inaashiria kitu kingine.

तालिबान का प्रतिनिधिमंडल

Chanzo cha picha, TWITTER//BILALKARIMI21

Taliban 'hawako katika nafasi ya kutambuliwa'

Iran imeshikilia msimamo wake kwa miezi kadhaa iliyopita kwamba haiko tayari kutambua Taliban kama mtawala halali wa Afghanistan.

Mnamo Januari 10, Msemaji wa Wazara ya Mambo ya Nje ya Iran Saeed Khatibzadeh kwa mara nyingine tena alifafanuamsimamo wa Iran. Alisema kuwa Iran haiku katika nafasi ya kuitambua serikali ya mpito ya shirika hilo la kiislamu.

Bahadur Aminian, balozi wa Iran mjini Kabul, pia alitoa tamko sawia na hilo Januari 3 wakati wa mahojiano na Kituo cha Runinga cha kibinafsi cha Tolo News nchini Afghanistan. Alisema kuwa Taliban inataka kutambuliwa na Iran, lakini inastahili kubuni serikali inayojumuisha wawakilishi wa jamii tofauti.

Kando na hilo, kabla ya ziara ya Mottaqi nchini Iran, tovuti ya Habari ya Iran alidai kuwa serikali ya Iran inajiandaa kukabidhi ubalozi wa Afghanistan kwa Taliban.

Hata hivyo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imekanusha madai hayo, akisema itaenda kinyume na Mkataba wa Vienna wa 1961.

आयातुल्लाह अली खामनेई

Chanzo cha picha, EPA

Nini kilifanyika baada ya ziara hiyo

Katika mahojiano na Tolo News, Balozi wa Iran kwa mara nyingine alisema baada ya kuundwa kwa serikali jumuishi nchini Afghanistan, Iran haitatambua tu serikali hiyo, bali pia itaziomba nchi nyingine kuchukua hatua hiyo.

Alisema kuwa uundaji wa serikali shirikishi inaweza kubuniwa kupitia uchaguzi au kulingana na utamaduni wa Afghanistan. Yalikuwa matamshi ya kuvutia kutoka kwa mwakilishi wa nchi ambayo kiongozi wake mkuu Ali Khamenei alikejeli serikali za kifalme za nchi za Kiarabu kwa kutofanya uchaguzi mwaka jana.

Khamenei alisema mnamo Juni 2021, "Hata katikati ya karne ya 21, kuna baadhi ya nchi zinazoongozwa na kabila. Hapo harufu ya uchaguzi haijafika. Watu wanaoishi huko wana sanduku la kura na sanduku la matunda." sijui tofauti ni nini.

Kwa hivyo, inaonekana kwamba mtazamo wa watu wa Afghanistan juu ya kutambua serikali inayoongozwa na Taliban sio lazima kwa Iran, ikiwa serikali hii inajumuisha watu wa makabila yote.

Hata hivyo, Jamhoori-y-Islami, gazeti la kihafidhina linalochukuliwa kuwa la wastani, liliripoti tarehe 11 Januari kwamba kukataa kwa Taliban kufanya uchaguzi kulimaanisha kwamba "Iran ni Taliban kwa sababu ya masharti yaliyowekwa na viongozi wake wakuu." na haiko katika nafasi ya kuitambua."

तालिबान के लड़ाके

Chanzo cha picha, Getty Images

Lakini hatua nyingine iliyochukuliwa na Iran inaonyesha kuwa Iran inaelekea katika kuwatambua Taliban.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ilitoa taarifa baada ya kikao kati ya Amir Abdullahiyan na Motaki.

Taarifa hiyo ilimtaja Mottaki kama "kaimu kiongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Afghanistan". Ni hotuba ya ziada rasmi kwa mtu ambaye shirika la habari la Iran Irna lilimwita "Waziri wa Mambo ya Nje wa Taliban" siku moja kabla.