Afghanistan: Kikosi kipya cha 'Fateh ambacho Taliban inatumia kulinda Kabul

AL-HIJRAT/TALIBAN

Chanzo cha picha, AL-HIJRAT/TALIBAN

Nchini Afghanistan, Taliban wameunda kikosi kipya cha usalama kulinda maeneo muhimu na mji wa Kabul. Hivi karibuni, makundi yenye msimamo mkali yalikuwa yamesambaza jumbe kwamba yatavuruga amani na sheria katika mji huo .

Katika chapisho la Twitter mnamo Agosti 24, akaunti ya Taliban ya lugha ya Kiarabu (@alemara_ar) ilitoa habari kuhusu kikosi hicho. Imeandikwa kwenye twitter kwamba ni 'Fateh Walk' yaani Kikosi cha Ushindi na kimeanza kuzunguka jiji la Kabul.

Wanajeshi wenye silaha wanaweza kuonekana na magari yao ya usalama kwenye picha nne zilizowekwa.

Picha moja ilionyesha foleni ya magari ya kijeshi yaliyobeba bendera nyeupe ya Taliban. Katika picha ya pili, jina la nguvu mpya linaonekana kwenye magari haya kwa Kipashto na kwa Kiingereza.

Usalama wa maeneo muhimu

Akaunti ya Twitter ya lugha ya Kiarabu ya Taliban haikutoa maelezo zaidi. Lakini akaunti inayodaiwa kuwa tawi la vyombo vya habari la Emirati hiyo ya kiislamu zilidai kwamba kwamba kikosi hicho kipya kinalinda maeneo muhimu huko Kabul, pamoja na Sarai Shahzada.

Baada ya Taliban kuiteka Kabul mnamo Agosti 15, akaunti yake ya Twitter ya lugha ya Kiarabu ilitangza kitengo kilichoitwa Badri 313 kama Kikosi Maalum.

AL-HIJRAT/TALIBAN

Chanzo cha picha, AL-HIJRAT/TALIBAN

Katika jumbe za twitter mnamo Agosti 15 na 17, Taliban ilisema kitengo cha Badri 313 kimepelekwa kulinda sehemu "za kimkakati na muhimu" za mji mkuu na vile vile Rashtrapati Bhavan.

Mnamo Julai, msemaji wa Taliban Zabiullah Mujahid aliandika juu ya kufuzu kwa wanajeshi wa kikosi cha Badri 313. Hapo awali, Zabiullah pia alikuwa ametaja juu ya kikosi hiki mnamo Novemba 2018.

Katika siku chache zilizopita, Taliban wamejaribu kutoa picha kama kwamba maisha nchini Afghanistan yanarudi kuwa hali ya kawaida

tl

Chanzo cha picha, Zabihullah/Twitter

TL

Chanzo cha picha, ZABIHULLAH/TWITTER

TL

Chanzo cha picha, ZABIHULLAH/TWITTER

China ilijitolewa kuisadia Taliban

Wakati huo huo, China imesema kuwa iko tayari kusaidia katika mchakato wa amani na ujenzi upya nchini Afghanistan. China imetoa msaada huu kwa ujumbe wa Taliban wa Afghanistan wakati wa mkutano na balozi wa China.

Nchini China, Tovuti ya habari inayoungwa mkono na serikali 'The Paper' ilinukuu maafisa wa China wakisema mkutano huo "ulikuwa wa hiari na mzuri".

Mbali na Urusi na Pakistan, China ndiyo nchi pekee ambayo imeonyesha nia ya kutaka uhusiano mzuri na Taliban.

Ujumbe wa Taliban ulikwenda China hata kabla ya kuchukua udhibiti wa Kabul, na kisha China ilikuwa imesema, pamoja na mambo mengine, kwamba "haitaingilia kati mambo ya ndani ya Afghanistan".

Taliban walikuwa wamehakikishIa China kuwa hawatakubali ardhi yao (Afghanistan) itumike dhidi ya China.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China Wang Wenbin alisema kuwa balozi wa China nchini Afghanistan, Wang Yu, alikutana na Abdul Salam Hanafi wa Taliban huko Kabul Jumanne tarehe 24 Agosti. Abdul Salam ni naibu mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Taliban huko Qatar.

Wang aliwaambia wanahabari Jumatano, "Mazungumzo ya China na Taliban ya Afghanistan yalikuwa laini na yenye ufanisi. Kabul kawaida ni mahali muhimu kwa majadiliano juu ya maswala yote muhimu kati ya pande hizo mbili."

Walakini, hakuelezea ni maswala gani yaliyojadiliwa wakati wa mkutano.

Alisema, "Sera ya Uchina kuelekea Afghanistan imekuwa sawa na wazi kabisa. Siku zote tunaheshimu uhuru na uadilifu wa eneo la Afghanistan.

Tunafuata sera ya kutokuingilia katika maswala ya ndani ya Afghanistan. "Kuwa na mtazamo wa urafiki kwa watu."

Wang pia alisema, "China inaheshimu uhuru wa watu wa Afghanistan kuamua maisha yao ya baadaye na hatima. China inaunga mkono mafundisho ya mamlaka inayoongozwa na Afghanistan."

Aliongeza, "China inataka kudumisha uhusiano wa kirafiki na ushirikiano na Afghanistan kama jirani na kuchukua jukumu la kuleta kwa amani na ujenzi wa taifa ."