Afghanistan: Jinsi Uingereza, Urusi na Marekani zilivyoshindwa na Taliban katika kipindi cha miaka 180 iliyopita

Una niña sentada en la hierba entre las lápidas de los muertos en las guerras de Irak y Afganistán, foto tomada el 31 de mayo de 2021 en Arlington, Virginia.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mbunge wa congresi wa Marekani mwanamke Elise Stefanik alilinganisha kuanguka kwa Kabul , mji ambao aliufananisha na Saigon, (mji wa kale wa Vietnam) sawa na : " balaa la kushindwa katika jukwaa la kimataifa ambalo halitawahi kusahaulika ."

Himaya ya Uingereza ilijaribu katika karne ya 19 , wakati ilipokuwa taifa lenye nguvu zaidi duniani, lakini katika mwaka 1919 ililazimika kuondoka Afghanstan na kuwapatia uhuru.

Halafu Muungano wa Usovieti ambao katika mwaka 1979 uliivamia nchi hiyo kwa lengo la kuendelea kuuweka mamlakani utawala wa kikomunisti , lakini ilichukua miaka 10 kwao kubaini kuwa hawangeshinda vita vile.

Uingereza na Usovieti zinafanana inapokuja katika uvamizi dhidi ya Afghanistan waliteka himaya kwanza , lakini baada ya muda mfupi zilianza kubomoka.

Miaka ishirini baada ya uvamizi ulioongozwa na Marekani mwaka 2001, vita vya mara kwa mara vilisababisha vifo vya maelfu ya watu, serikali ya Joe Biden ikaamua kuondoa wanajeshi wa nchi yake nchini Afghanistan mwezi Aprili mwaka huu.

Ulikuwa ni uamuzi wenye utata ambao umekuwa ukikosolewa vikali na kusabababisha kuanguka kwa kasi kwa Kabul, mji mkuu wa Afghanstan, mikononi mwa kikundi cha jihadi cha Taliban.

Biden ametetea kuondolewa kwa vikosi vya Marekani, akidai kwamba Wamarekani hawapaswi kufa "katika vita ambavyo Waafghanistan ambao hawajajiandaa kujipigania wenyewe."

"Hakuna idadi yoyote ya wanajeshi ambao wanaweza kufanikiwa kuifanya Afghanstan thabiti, yenye umoja na ya amani," rais aliongeza. Akisema kuwa nchi inafahamika kama "Himaya za makaburi. "

Afghanistan imekuwa ni eneo baya zaidi la maadui wakubwa katika historia ya karne za hivi karibuni, ambao wamekuwa wakijjaribu kuidhibiti-na kupata mafanikio mwanzoni mwa uvamizi- lakini mwishowe wamekuwa wakitoroka nchi.

"Sio kwamba Waafghanistan wana nguvu sana, kile kilichotokea nchini Afghanistan ni kosa la uvamizi wa himaya zenyewe ," anasema mchambuzi wa ulinzi na sera za kigeni David Isby, aliiambia BBC .

Isby anakiri kuwa Afghanistan ni eneo gumu: ni taifa gumu, masikini sana, lenye miundo mbinu duni na lisilo na maji.

Montañas de Afganistán, cerca de la frontera con Pakistán.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Afghanistan ni nchi yenye miundo mbinu duni sana na ni ngumu kijiografia

"Lakini himaya, iwe ya Usovieti, Uingereza au Marekani zimeonesha wepesi zinapoishughulikia Afghanistan. Walitaka kufanya mambo yao wanavyotaka na kwa njia zao na hawakuwai kuweza kuelewa ugumu wa nchi ," aliongeza.

Mara kwa mara imekuwa ikisikika kwamba Afghanistan "haiwezekani kuishinda", kauli ambazo sio za kweli : Wapersia, Wamongolia na Alexander the Great waliweza kipindi kilichopita.

Kile ambacho ni dhahiri ni kwamba ni kitendo ambacho kimewagarimu sana wale ambao walijaribu kukifanya. Na himaya tatu za mwisho ambazo zilijaribu kuivamia Kabul zilishindwa kirahisi.

Himaya ya Uingereza na uvamizi wake mara tatu

Kwa kipindi kikubwa cha karne ya 19 , Afghanistan ilikuwa ni kituo cha jukwaa la "Mchezo mkuu " baina ya himaya za Uingereza na Urusi wa kuwania udhibiti wa eneo la Asia ya Kati.

Kwa miongo kadhaa , Moscow na London ziliendesha mapambano ya kidiplomasia na kisiasa ambapo Uingerereza iliyashinda, lakini kwa gharama . Uingereza ilijaribu kuivamia nchi ya Afghanistan mara tatu baina ya mwaka 1839 na 1919, na ilishindwa mara azote tatu.

Baada ya kuvamia mara tatu, hatimaye Waafghanistan walivilazimisha vikosi vya uvamizi kuondoka katika mji mkuu, na matokeo ya kuondoka kwake yalisababisha maafa.

Unidad militar inglesa siendo atacada por insurgentes cerca de la ciudad afgana de Gandamak. Primera Guerra Anglo-Afgana.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jeshi la Uingereza wakati huo likiwa ndio jeshi lenye nguvu zaidi duniani, liliaibishwa na makabila ya Afghanistan, kwa silaha nyepesi wakati wa vita vya kwanza vya Uingereza na Afghanistan

"Vita hivi vilidhoofisha juhudi za kupanua himaya ya Uingereza za kutaka iwe bara na pia vikaathiri mawazo kwamba Uingereza Uingereza haishindwi ," anaeleza Isby.

Takriban miongo mine baadaye, Uingereza ilijribu tena na kupata mafanikio machache zaidi.

Vita vya pili kati ya Uingereza na Afghanstan (Anglo-Afghan War) vilivyotokea kati ya mwaka 1878 na 1880,viliiishia kwa Afghanistan kuwa chini ya uangalizi wa Uingereza, lakini London ililazimika kuacha sera yake ya kuwa na waziri mkazi mjini Kabul.

Balada yake ilichagua na kumuunga mkono Amir mpya wa Afghanstanna kuondo vikosi vyake nchini humo.

Ingawa rasmi Uingerea haikuwa tena nchini Afghanstan, inachukuliwa kuwa waliendeleza ushawishi wao kwa miaka mingi zaidi kwa nchi hiyo.

Vietnam ya Muungano wa Usovieti

Katika miaka ya 1920 Emir Amanullah Khan alijaribu kufanya mageuzi nchini humo na, miongoni mwa hatua nyingine alizozichukua ilikuwa ni kuzuia utamaduni wa uvaaji wa burqa kwa wanawake. Msururu wa mageuzi uliwaudhi baadhi ya viongozi wa kikabila na kidini, na hivyo kuibua vita vya kiraia.

Hali ya wasi wasi katika nchi hiyo ya Asia iliyosababishwa na kupigania madaraka iliendelea kwa miongo hadi Muungano wa Usovieti ulipoivamia nchi mwaka 1979 ili kuendelea kuiweka mamlakani serikali ya kikomumisti iliyogawanyika kwa kiasi kikubwa.

Un soldado soviético sobre un vehículo blindado el primer día de la retirada final de las tropas soviéticas, en Kabul, Afganistán, el 15 de mayo de 1988.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Uvamizi wa Usovieti ulisababisha umwagaji damu mkubwa kuwahi kuliko uvamizi wowote ule nchini Afghanistan

Makundi mbali mbali ya mujahideen( makundi ya kidini yenye itikadi kali) yalipinga Usovieti na kuanza mapambano ya kivita dhidi yake, kwa pesa na silaha zilizotolewa na Marekani, Pakistan, Uchina, Iran na Saudi Arabia.

Uvamizi wa Urusi ulisababisha umwagaji damu zaidi kuliko uvamizi wowote ule, ukisababisha vifo vya watu takriban milioni 1.5 na wengine milioni 5 kuwa wakimbizi.

Wakati mmoja,vikosi vya Usovieti viliweza kudhibiti miji muhimu na miji mikubwa, lakini mujahideen walitembea kwa uhuru katika maeneo mengi ya vijijini.

Soldados soviéticos en Kabul.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wasovieti waliiacha nchi katika hali mbaya

Wakati huo kiongozi wa Usovieti Mikhail Gorbachev aligudua kuwa asingeweza kuendelea kuubadilisha uchumi wa Urusi na akaamua kuondoa vikosi vyake Afghanistan mwaka 1988, lakini sifa ya nchi haikuwahi kuwa nzuri tena.

Wasovieti waliiacha nchi katika hali mbaya

Afghanistan ikawa Vietnam ya Muungano wa Usovieti. Vilikuwa ni vita vya garama na aibu. Ambavyo licha ya kuytumia nguvu zote, USSR ilishindwa na kuaibishwa na a wapiganaji wa msituni.

Marekani na ''baalaa'' lake la kujiondoa

Baada ya uingiliaji kati ulioshindwa Uingereza na Muungano wa Usovieti , Marekani iliongoza uvamizi mpya dhidi ya Afghanistan mwaka 2001, ikiahidi kuunga mkono demokrasi na kumaliza tisho la ugaidi kutoka kwa Al Qaeda, baada ya mashambulio ya Septemba 11.

Sawa na dola mbili zilizoitangulia, Washington iliweza kuiteka Kabul haraka na kuwalazimisha Taliban kusalimu amri na kukabidhi mamlaka.

Urnas con banderas de EE.UU.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Zaidi ya wanajeshi 3,500 kutoka muungano unaoongozwa na Marekani wameuawa tangu mwaka 2001, theluthi mbili kati yao wakiwa ni Wamarekani.

Miaka mitatu baadaye, serikali mpya ya Afghanistan ilichukua urais, lakini mashambulio ya umwagaji damu ya Taliban yaliendelea.

Rais wa zamani Barack Obama alitangaza kuongeza wanajeshi mwaka 2009 ambao walisaidia kuwasukuma nyuma Taliban, lakini si kwa muda mrefu.

Zaidi ya wanajeshi 3,500 kutoka muungano unaoongozwa na Marekani wameuawa tangu mwaka 2001, theluthi mbili kati yao wakiwa ni Wamarekani.

Unaweza pia kusoma:

Mwaka 2014, ambao uliishia kuwa mwaka uliokuwa na umwagaji damu mkubwa zaidi tangu mwaka 2001, vikosi vya NATO vilimaliza kazzi yake na kukabidhi jukumu lake la usalama kwa jeshi la Afghanistan.

Kitendo hiki kiliwaruhusu Taliban kuyateka maeneo zaidi ya nchi.

Katika mwaka uliofuatia,kikundi cha Taliban kiliendeela kupata nguvu na kufamya misururu ya mashambulio ya kujitolea muhanga . Kilidai kufanya mashambulio kwenye jingo la buge mjini Kabul na shambulio jingine kwenye uwanja wa ndege wa mji mkuu.

Huku uvamizi wa Usovieti ukiwa uvamizi uliosababisha umwagaji damu mkubwa zaidi, uvamizi wa Marekani ndio uliokuwa wa garama zaidi.

Wasovieti walitumia takriban sola bilioni 2 kila mwaka nchini Afghanistan, kati ya mwaka 2010 na 2012 ndani ya nchi hiyo. Lakini garama ya vita kwa Marekani ilipanda hadi takriban dola bilioni 100 kila mwaka, kulingana na takwimu zilizotolewa na serikali ya Mareani yenyewe.

Lakini kuanguka kwa Kabul pia kumelinganishwa na matukio yaliyotokea Vietnam Kusini .

"Hii ni Saigon ya Joe Biden, " mbunge wa congresi wa Republican Elise Stefanik alituma ujumbe wa Twitter akisema . "janga la kushindwa katika jukwaa la kimataifa ambalo halitawahi kusahaulika ."

Baada ya kuondoka kwa vikosi vya Mrekani na matokeo yake Taliban kupata ushindi, dunia inakabiliwa na mzozo mpya wa kibinadamu huku maelfu ya wkimbizi wakitakiwa kutafuta makao ya kuishi.

"Kwa kipindi kifupi, itakuwa muhimu kuona kama utawala wa taliban unaweza kuingizwa katika jamii ya kimataifa, jambo ambalo linatia wasi wasi mkubwa," anasema David Isby.

Na kama itawezekana kwa jamii ya kimataifa kuishugulikia Raliban, itakuwa muhimu kuona kama dola nyingine itajihatarisha kwa kujiingiza katika uvamizi mpya wa Afghanistan, kaburi la himaya.