A380:Ndege ya mwisho kubwa zaidi yakabidhiwa mmiliki wake mpya

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Ndege ya mwisho ya Airbus A380 kuwahi kujengwa inakabidhiwa kwa wamiliki wake wapya siku ya Alhamisi, shirika la ndege la Emirates lenye makao yake Dubai.

Ni wakati muhimu. Jitu hili la anga litaendelea kuruka, lakini mustakabali wake wa muda mrefu bado haujulikani.

Emirates, ambayo inamiliki takriban nusu ya ndege za A380, inaonekana kuendelea kuzitumia kwa miaka mingi ijayo.

Lakini mashirika mengine kadhaa ya ndege yaliacha kutumia ndege yao wakati wa janga la Covid na zingine tayari zimeacha kutumiwa kabisa.

A380 ndiyo ndege kubwa zaidi ya abiria duniani. Kwa kawaida inaweza kubeba abiria 545 - ingawa kwa nadharia inaweza kubeba kiwango cha juu cha watu 853.

Ndege hii kubwa yenye ghorofa mbili ina injini nne, mabawa ya mita 80 na uzito wa juu wa kuruka ni tani 560. Pia ina mengi sana - ina takriban kilomita 530km (maili 330) za nyaya .

Ni rahisi kuipeperusha

Walakini kulingana na Alex Scerri, Nahodha wa zamani wa A380, ni rahisi sana kuruka.

"Airbus wameweza kuunda A380 ili ihisi kama ndege ndogo zaidi kama A320," anasema. "Ni mahiri sana, na haijisikii kama ndege ya tani 600."

Mradi huo ulianzishwa mwanzoni mwa miaka ya 1990. A380 ilikusudiwa kuwa ishara ya umahiri wa kiviwanda wa Ulaya, kinara wa kutengezaji wa Airbus ili kupita 747 jumbo ya Boeing.

Wakati huo, ilidhaniwa sana kwamba vituo vikuu vya viwanja vya ndege kote ulimwenguni vilikuwa na msongamano zaidi na zaidi kadiri miji inavyokua na trafiki ya ndege ikiongezeka. Hii ingeunda soko la ndege kubwa sana ambazo zinaweza kubeba abiria zaidi bila kuongeza idadi ya safari za ndege.

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Kushindwa kibiashara

Kufikia wakati A380 ilipofanya safari yake ya kwanza ya kibiashara mnamo 2007, hata hivyo, mbegu za kufa kwake zilikuwa tayari zimepandwa.

Wakati wahandisi wa Airbus wakihangaika kuleta superjumbo sokoni, Boeing ilikuwa ikiuza kwa utulivu matoleo ya masafa marefu ya injini yake pacha ya 777 - na kutengeneza 787 Dreamliner.

787 ilikuwa muundo ambao ulifanya maendeleo zaidi katika teknolojia ya injini, na vile vile katika vifaa vya mchanganyiko na aerodynamics. Matokeo yake yalikuwa ndege ambayo ilikuwa na ufanisi zaidi kuliko mifano ya awali, ilitumia mafuta kidogo na hivyo ilikuwa nafuu kuendesha.

Pamoja na Airbus A350, iliyozinduliwa miaka michache baadaye, ilibadilisha sura ya soko.

Badala ya kutumia ndege kubwa kusafirisha idadi kubwa ya watu kati ya viwanja vya ndege vya 'kitovu', kabla ya kuwaweka kwenye safari za kuunganisha hadi maeneo mengine, mashirika ya ndege sasa yanaweza kurusha ndege ndogo kwenye njia za moja kwa moja zisizo na watu wengi kati ya miji midogo ambayo haingeweza kuepukika hapo awali.

Ikilinganishwa na miundo hii mipya, A380 ya injini nne ilikuwa ghali kuinunua na ilikuwa ghali kuiendesha.

"Teknolojia kwenye A380 kimsingi ilikuwa ya miaka ya 1980," anasema Peter Morris, mwanauchumi mkuu katika shirika la ushauri la usafiri wa anga la Ascend by Cirium. "Iligandishwa katika muundo kabla ya mabadiliko ya hatua katika teknolojia ya ndege - kabla ya mchanganyiko wa kaboni na injini zenye ufanisi mkubwa".

Matokeo yake, Airbus ilihangaika kuiuza. Ni ndege 251 pekee ndizo zilizowahi kujengwa, na mpango huo ulitatizika kufaulu kando na kushindwa kurejesha zaidi ya $25bn zilizowekezwa ndani ya mradi huo

Hata hivyo kulingana na afisa mkuu mtendaji wa Airbus Philippe Muhn, mradi huo bado umeleta manufaa makubwa kwa shirika hilo, ambalo lilikuwa limeundwa kutoka kwa kikundi cha wazalishaji kutoka nchi tofauti.

"Hii ilikuwa ni ndege ambayo iliruhusu kampuni kuunganishwa, kutoka kwa mtazamo wa kiufundi, mtazamo wa kiviwanda, na kiutamaduni pia", anafafanua.

"Na kisha bila shaka uwekezaji wote katika teknolojia ya A380 ulikuwa msingi wa kile A350 kilitokea baadaye."

Lakini, ingawa inaweza kuwa kushindwa kibiashara kwa Airbus, superjumbo ndege hiyo imekuwa ya mafanikio kwa mteja wake mkuu.

Emirates iliitumia kuunda mtandao wa kimataifa wa njia zenye safari nyingi,za masafa marefu zinazoiunganisha na makao yake huko Dubai. Hilo liliisaidia kuwa mojawapo ya mashirika makubwa zaidi ya ndege duniani.

"Kwani Emirates iliunda nafasi yake sokoni", anaelezea Peter Morris.

"Bila ya A380, sidhani kwamba Emirates ingeweza kufikia kiwango ambacho ilifikia. Waliweza kutengeneza kitu ambacho kilisaidia kujenga heshima ya Dubai, na kuunda soko la ndege pia. Ilifanya kazi."

Lakini kwa mashirika mengine ya ndege, superjumbo haikuwa na mafanikio. Kujaza viti hivyo vyote kunaweza kuwa changamoto - na wakati janga la Covid lilipotokea, karibu ndege zote ilisimamishwa.

Wakati baadhi ya mashirika ya safari za ndege sasa yanazirudisha, mengine, kama vile Lufthansa na Air France yameamua kustaafisha ndege zao.

Hiyo inazua swali la nini kitatokea kwa ndege zisizotumiwa. Kwa nadharia, zinaweza kuruka kwa miongo kadhaa. Lakini kulingana na Ascend by Cirium, soko la mitumba la ndege kubwa kama hizo ni "ndogo hadi halipo".

Kuna uwezekano, basi, kwamba A380 zaidi zitaenda tu kuwekwa viwanjani , kufuatia saba ambazo tayari zimeripotiwa kutupwa.

Lakini nyingine zitabaki katika huduma. Emirates, ambayo ina ndege 118 za A380, inasema itaendelea kuzisatumia kwa miongo miwili ijayo - ingawa baada ya muda idadi yao huenda ikapungua huku ndege mpya zaidi zikiletwa.

Ingawa inaendelea kuruka kwa muda mrefu, mwanahistoria wa usafiri wa anga Shea Oakley anafikiri kwamba jumbo hiyo kubwa tayari imeweka muhuri mahali pake katika historia.

"Kwa bahati mbaya kwa Airbus, walijenga kito cha kiteknolojia, lakini walichagua maono yasiyofaa. Ilikuwa ndege nzuri, lakini chaguo baya kwa nyakati", anasema.

"Sina uhakika kutakuwa na ndege kubwa kuliko A380."