Sahau kuhusu Supersonic. Hypersonic ni ndege yenye kasi zaidi duniani

t

Chanzo cha picha, Hermeus

Ndege ya kisasa aina ya Supersonic ni mmoja ya ndege zenye kasi sana. Katika kipindi cha miezi, Kampuni ya Boom ilifanikiwa kufayia majaribio ndege yake ya maonyesho ya XB-1 na kufanikiwa kuuza viti 15 kati ya 30 vilivokuwa bado kwenye matengenezo na kupiku aina nyingi za ndege Marekani.

Virgin Galactic na Rolls Royce ziliungana na kutengeneza ndege yenye viti 19. Hata shirikisho la Urusi nalo limetangaza mpang wake wa kutengeneza ndege ya supersonic kwa ajili ya biashara.

Ukiacha Supersonic kuna aina nyingine inaitwa Hermeus Quarterhorse. Fikiria kasi ya supersonic au kasi ya Mach 1—zidisha mara tano utapata kasi ya hypersonic Quarterhorse.

Juma lililopita, kampuni moja iliyopo Atlanta ilitangaza zawadi ya dola $60 million kutoka jeshi la anga la Marekani kufadhili majaribio ya ndege. Kama ilivyo kwa ndege ya kigiriki ya Hermes, taina hii ya ndege Hermeus imetengezwa kuweza kusafiri kila pembe ya ulimwengu kwa kasi ya Mach 5.5— au 4,219 kwa saa. Hiiyo inafanya ndege hiyo kuwa ya kasi zaidi duniani, ambayo inaweza kusafiri kutoka New York, Marekani mpaka London, Uingereza kwa muda usiozidi saa moja.

yl

Chanzo cha picha, Hermeus

Kasi yake inatokana na namna mfumo wa injini yake ulivyotengenezwa, ni wa kipekee, wenye mfumo wa TBCC propulsion, mfumo ambao unatumia injini ya kawaida wakati wa kupaa na kutua tu, na kutumia mfumo mwingine unaoitwa ramjet au scramjet—ambao unazalisha nguvu zaidi, lakini ikihitaji kasi kubwa ya upepo kusaidia kuiwasha.

Hermeus imeanza vizuri. Katika kipinci cha miezi 9, imeweza kubuniwa, kutengenezwa na kujaribiwa injini yake, ambayo iko kwenye muundo wa GE J85 turbo jet, na ina faida mbili kubwa, linapokuja suala la kufanyia majaribio. Quarterhorse inaweza kuendeshwa bila rubani na hivyo ni rahisi kwa timu inayofuatilia kujua prototypes ikiwa angani na kujifunza wanayotaka kujifunza bila kuhatarisha maisha ya rubani.

Kwa sasa, upo mpango wa kuifanyia majaribia ndege ndogo ya aina hiyo mwaka 2023, mwaka 2025 watafanyia majaribio ndege ya ukubwa wa kati ya mizigo na ndege kubwa kabisa ya abiria ya kibiashara itafanyiwa majaribiwa mwaka 2029.

tl

Chanzo cha picha, Hermeus

Faida nyingine ni kuhusu mapato ya fedha kwa serikali. "Wakati ushirikiano huu na Jeshi la anga la Marekani ukionyesha msisitizo wa dhamira ya kitengo cha ulinzi Marekani kuhusu ndege hizi, na kuungana kwao na muungano wa Hermeus na NASA uliotangazwa Februari 2021, ni wazi kwamba tunachokitengeneza kinagusa masuala ya ulinzi na biasara," alisema AJ Piplica, Mtendaji mkuu waHermeus.