Hizi ndizo ndege 10 kubwa zaidi za abiria ulimwenguni

q

Chanzo cha picha, Google

Usafiri wa anga ni uwezeshaji muhimu kufikia ukuaji wa uchumi na maendeleo. Usafiri wa anga huwezesha ujumuishaji katika uchumi wa ulimwengu na hutoa unganisho muhimu kwa kiwango cha kitaifa, kikanda na kimataifa. ... Kazi ya sekta ya uchumi, utafiti, na usambazaji wa maarifa juu ya masuala yanayohusu uchukuzi wa anga.

Hizi ni ndege kumi za abiria kubwa zaidi ulimwenguni zinazoweza kusafirisha mamia ya abiria kutoka upande mmoja wa ulimwengu ndani ya saa moja. Tazama orodha hii ya ndege kubwa zaidi za abiria duniani, kwa mujibu wa Mtandao wa masuala ya anga unaoitwa 'aerotime'.

10. Airbus A333-300

Airbus

Chanzo cha picha, Airbus

Ndege hii ilianza kuruka tarehe 2 mwezi Novemba mwaka 1992. Ndege hii ina uwezo wa kubeba abiria 250 mpaka 440. Watumiaji wakuu wa ndege hii ni Shirika la ndege la Uturuki, Air China,China Eastern Airlines (CIAH) (CEA), China Southern Airlines (ZNH) na Cathay Pacific

9. Airbus A340-300

airbus

Chanzo cha picha, Airbus

Ndege aina ya Airbus 340 300 ni ndege ya abiria iliyoundwa Ufaransa. Ilitengenezwa kwa mara ya kwanza mwaka 1993 na ina uwezo wa kubeba abiria 295 katika mpangilio wa daraja moja na 267 kwenye mfumowa madaraja mawili.

8. Airbus A340-500

Airbus

Chanzo cha picha, Airbus

Hii ni ndege ya abiria iliyoundwa Ufaransa. Ilitolewa mwaka 2006, ingawa ilitolewa awali mwaka 2002. Imebuniwa kwa ajili ya kubeba abiria 372 katika mpangilio wa siti za daraja moja na 313 madaraja mawili.

7. Airbus A350-900

Airbus

Chanzo cha picha, Airbus

Ndege hii inayojishughulisha na safari ndefu, ina uwezo wa kusafiri umbali wa kilomita 15,000 na inaweza kubeba abiria kati ya 300 na 350. A350 inashindana na ya Boeing 787-10 na safu ya 777, na vile vileBoeing 777X iliyoanza mwaka 2021.

6. Boeing 777-200

Airbus

Chanzo cha picha, Airbus

Ndege ya Boeing 777 200 ni ndege ya abiria iliyoundwa Marekani. Inaweza kuchukua abiria 440 katika mfumo wa daraja moja na 400 katika mfumo wa madaraja mawili. Ina safu ya kusafiri ya kilomita 14,260 au maili 7700 kutoka usawa wa bahari.

5. Airbus A340-600

Airbus

Chanzo cha picha, Airbus

Ilianzishwa mnamo 2002, A340-600 ni moja kati ya ndege za aina ya A340 yenye uwezo mkubwa zaidi. Bodi yake yenye injini nne inaweza kubeba abiria 380. Kuanzia Oktoba 2020, waendeshaji wakuu ni Lufthansa (LHAB) (LHA) na Mahan Air.

4. Boeing 777-300

G

Chanzo cha picha, Generic Elecrit

Ndege ya Boeing 777 300 ni ndege ya abiria iliyotengenezwa Marekani na uwezo wa kukaa watu 550 kwa mpangilio wa daraja moja na 451 katika madaraja mawili. Ina uwezo wa kusafiri maili 6,013 kutoka usawa wa bahari au kilomita 11,135.

Shirika la ndege la Emirates ni mtumiaji mkubwa wa Boeing 777 duniani, ikiwa na ndege 131 za 777-300 zinazofanya kazi.

3. Boeing 747-400

a

Chanzo cha picha, Airplane Picture

Ndege ya Boeing 747 400 ni ndege ya abiria iliyoundwa Marekani na Boeing ambayo ina uwezo wa kubeba abiria 416 kwa safu ya madaraja matatu ,524 madaraja mawili na 660 katika daraja moja. Ina safu ya kusafiri umbali wa maili 7,260 juu ya usawa wa bahar au kilomita 13,446.

2. Boeing 747-8

a

Chanzo cha picha, Airways Magazine

Ndege ya Boeing 747 8 ni ndege ya abiria iliyotengenezwa nchini Marekani. Inaweza kubeba abiria 700 ikiwa mfumo wa daraja moja wakati viti 600 vinapatikana kwa mfumo wa madaraja mawili. Ndege hiyo ina uwezo wa kusafirri umbali wa maili 8.

1. Airbus A380-800

m

Chanzo cha picha, Middle East C

Airbus A380 800 ni ndege ya abiria iliyotengenezwa Ufaransa na uwezo wa kubeba abiria 853 katika daraja moja au 644 katika daraja la ngazi mbili. Ina safu ya kusafiri ya maili 8,208 kutoka usawa wa bahari au kilomita 15,200. Ilianza safari tarehe 27 mwezi Aprili, 2005. Kufikia 30 Septemba 2020, ndege 242 zilitengenezwa, hata hivyo, kwa sababu ya mauzo duni, Airbus ilitangaza kuacha safari mwaka 2021.

Air France ilikuwa moja kati ya za kwanza kutangaza kustaafu kwa ndege zake zote za A380. Katika msimu wa joto wa 2020, Qantas ilithibitisha kuwa ndege zake 12 za Airbus A380 hazitafanya kazi kwa miaka mitatu ijayo. Mustakabali wa A380 wa Shirika la Ndege la Etihad pia uko mashakani, kwani shirika la ndege lilithibitisha kusitisha ndege zake hadi angalau majira ya baridi ya mwaka 2021.