Emma Coronel: Mke wa El Chapo ahukumiwa kifungo cha miaka mitatu

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Mke wa mlanguzi sugu wa dawa za kulevya nchini Joaquin "El Chapo" Guzmán amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani kufuatia jukumu lake la kusaidia genge la uhallifu la Sinaloa.
Emma Coronel Aispuro, 32, alikubali makosa mwezi Juni kwa mashtaka yanayohusu njama ya usambazaji haramu wa dawa za kulevya.
Pia alikiri kumsaidia Guzmán kutoroka gereza la Mexico.
Huenda angelikabiliwa na kifungo cha maisha gerezani, lakini waendesha mashtaka wa Marekani waliomba ahukumiwe kifungo kifupi baada ya kuonesha kuwa kujutia makosa yake.
Mume wake, 64, kwa sasa anahudumi akifungo cha maisha mjini Colorado.
Kulingana na nyaraka za mahakama, Coronel Aispuro, malkia huyo wa zamani wa urembo alikula njama na wanachama wengine wa genge la wahalifu la Sinaloa kusafirisha dawa za kulevya aina ya cocaine, heroin, methamphetamine, na bangi nchini Mareakni, nakutakatisha fedha zilizotokana na uuzaji wa bidhaa dawa hizo.
Mamlaka pia zinaamini kwamba Coronel Aispuro alifanya "jukumu muhimu " katika mpango wa kumsaidia Guzmán kutoroka gereza lenye ulinzi mkali mwaka 2015 kwa kununua mali karibu na eneo hilo.
Guzmán aliweza kutoroka kupitia shimo lililochimbwa kupitia chini ya ardhi- iliyokuwa na mwangaza, vifaa vya kupmlulia na piki piki - ambayo ilikuja hadi kwa. Nyumba inayomilikiwa na genge wahalifu
Pia limpatia saa iliyowezeshwa kwa GPS- na kutuma ujumbe kwa washirika wake akiwa ndani ya jela.
Kwa miezi kadhaa hakujulikana ametorokea wapi hadi alipojitokeza kwenye mahojiano na mwigizaji Sean Penn.
Mahakamani Jumanne mjini Washington, Jaji Rudolph Contreras pia aliamuru kwamba mali yake ya thamani ya karibu dola milioni 1.5 itaifishwe na awe chini ya miaka minne ya kuachiliwa kwa kusimamiwa atakapoondoka gerezani.
Akiongea kwa Kihispania kupitia mkalimani, Coronel Aispuro alisema "najutia madhara yoyote ambayo huenda ningeweza kufanya".

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Mwendesha mashtaka Anthony Nardozzi aliomba kifungo cha miaka minne mapema mwezi huu, akisema kwamba ingawa mwenendo wake "ulikuwa muhimu", jukumu lake lilikuwa ndogo na "alikubali upesi kuwajibika kwa mwenendo wake wa uhalifu".
Mzaliwa wa Marekani na mwana wa Inés Coronel Barreras, mwanachama wa genge la Sinaloa, Coronel Aispuro alikutana na Guzmán akiwa na miaka 17 na kuoana naye mwaka uliofuata.
Baba yake alihukumiwa kifungo gerezani nchini Mexico baada ya kushtakiwa kwa kumiliki silaha mwaka 2017.
Mjomba wake, Ignacio Coronel Villarreal, alichukuliwa kuwa mmoja wa watu wanaotafutwa sana Mexico hadi alipouawa katika makabiliano ya bunduki na Jeshi la Mexico mnamo 2010.
Wakili wake, Jeffrey Lichtman, alisema Coronel Aispuro huenda akawa hatarini endapo atarejea Mexico, kufuatia ripoti za vyombo za habari kuwa alishirikiana na mamlaka za Marekani.
"Sina hakika kama anaweza kurudi nyumbani," alisema.
Katika hukumu yake, Jaji Contreras alimtakia heri ya siku zijazo, akiongeza kuwa anatumai atawalea binti zake wawili "katika mazingira tofauti na uliyopitia leo."

Coronel ni nani?
Coronel, ni raia wa Mexico na Marekani, alikutana na Guzman akiwa na umri wa miaka 17, na akaolewa naye.
Wana watoto wawili, Maria Joaquina na Emali.
Wakati wa kesi ya mumewe, Coronel aliketi katika chumba cha mahakama karibu kila siku.
Wakati wa mapumziko, alikuwa akipiga kelele kwenye ngazi kando ya barabara.
"Sinva Diva," anasema Romain Le Cour Grandmaison, mchambuzi wa usalama ambaye ameishui huko Paris na Mexico, akisoma mashirika hayo. Na rangi ya mdomo nyekundu na almasi na suruali nyembamba, alijumuisha picha maarufu ya "buchona", shauku ya mapenzi ya narco.
Guadalupe Correa-Cabrera wa Chuo Kikuu cha George Mason amefanya utafiti huko Sinaloa, Mexico, ambapo kampuni ya El Chapo inafanya kazi.
Anafafanua neno, buchona: "Wanavaa nguo za bei ghali, mikoba ya Louis Vuitton. Kila kitu ni kutia chumvi, na yeye ni uwakilishi kamili wa picha hiyo. Yote ni juu ya sura, upasuaji wa plastiki."
Moja ya sifa zake za kushangaza, Correa-Cabrera alibainisha, ni "umbo la mgongo" wake, ambayo aliielezea kama "mbaya sana".Picha yake ya kupendeza ilikuwa tofauti na ukweli mbaya wa shughuli za gari la El Chapo.














