Emma Coronel Aispuro: Umaarufu wa Malkia wa dawa za kulevya na kuanguka kwake

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Emma Coronel Aispuro alikuwa na maisha ya kifahari huko New York, akifurahia matunda ya ndoa yake na muuzaji sugu wa dawa za kulevya Joaquin Guzman Loera, maarufu El Chapo.
Lakini alikamatwa, na kutupwa katika jela ya Virginia.
Nini kilitokea kwa malkia wa ulimwengu wa dawa za kulevya?Katika madirisha ya jela huko Alexandria, Emma Coronel Aispuro anashikiliwa katika kizuizi cha faragha, kwenye gereza dogo.Wakili wake Mariel Colón Miro, anasema mteja wake anasoma riwaya, "za kimapenzi", kupitisha wakati.Masharti ya nyumba ya gereza yanaonyesha tofauti kubwa na maisha aliyokuwa nayo zamani.Miezi michache iliyopita, alikuwa na mipango ya kuzindua laini ya nguo, El Chapo Guzman. (Wanandoa hao wana lebo yao ya mitindo huko Mexico na binti yake pia ametia fora kwa mtindo akitumia jina lake).Wakati nilipozungumza naye huko New York wakati wa kesi ya mume wake mnamo 2019, alikuwa amevaa vito, na saa ya bei ghali.Halafu mapema mwaka huu, Coronel, 31, alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dulles huko Virginia na kushtakiwa kwa kumsaidia mume wake uuzaji wa dawa za kulevya.
Guzman, 64, sasa anatumikia kifungo cha maisha katika kituo cha supermax cha Colorado.Maafisa wa FBI walisema Coronel alikula njama ya kusambaza cocaine na kusaidia kupanga kutoroka kwa mumewe kutoka gereza la Mexico mnamo 2015.
Stori yake ni ya kibinafsi, na mume wa kudanganya, bibi na biashara za jinai.
Hata hivyo inaangazia ulimwengu wa siri wa wauzaji wa dawa za kulevya, na wanawake wanaoishi ndani yao.
Tarehe ya kesi haijapangwa. Ikiwa atapatikana na hatia, anaweza kutumikia kifungo cha maisha gerezani.

Chanzo cha picha, Anadolu Agency via Getty Images
Kuweka kando swali la hatia au kutokuwa na hatia, wachambuzi ambao wanachunguza biashara ya dawa za kulevya wanasema kwamba Coronel alijiweka kwenye jukumu lisilo la kawaida.
Alikuwa mtu mashuhuri, mjasiriamali, na mlinda lango, akisaidia kudhibiti ni nani alikuwa na ufikiaji wa mumewe wakati alikuwa akiendesha genge hilo.Kwa kawaida , wake wa walanguzi wa dawa za kulevya wanaonekana kuwa "wa mapenzi tu" na "hawawi wakala wa dawa za kulevya", anasema Cecilia Farfán-Méndez, msomi katika Chuo Kikuu cha California huko San Diego.
Coronel alikuwa tofauti: "Alionyesha kuwa wanawake wanaweza kushikilia nyadhifa za nguvu."Nguvu ya kutumia kwenye jukumu hatari.Derek Maltz, wakala afisa wa uchunguzi anayehusika na usimamizi wa utekelezaji wa dawa za kulevya nchini Marekani, anasema: "Unapokuwa katika biashara hii, labda utashikwa au utauawa."

Chanzo cha picha, AFP via Getty Images
Coronel alikuwa na sura yenye ujasiri, na mipango yake ya kampuni ya mitindo, lakini wachunguzi wa serikali kuu walikuwa wakimfuatilia kwa ukaribu.
Kama Maltz anasema: "Ulimwengu ulikuwa umemgeukia, kuta zilikuwa zikishuka.""Ana utu sana," anasema Miro, wakili wake. "Emma ninayemjua - amejaa nguvu, akitabasamu kila wakati."

Chanzo cha picha, Alexandria Sheriff’s Office via Getty Images
Coronel, ni raia wa Mexico na Marekani, alikutana na Guzman akiwa na umri wa miaka 17, na akaolewa naye .
Wana watoto wawili, Maria Joaquina na Emali.
Wakati wa kesi ya mumewe, Coronel aliketi katika chumba cha mahakama karibu kila siku.Wakati wa mapumziko, alikuwa akipiga kelele kwenye ngazi kando ya barabara."Sinva Diva," anasema Romain Le Cour Grandmaison, mchambuzi wa usalama ambaye ameishui huko Paris na Mexico, akisoma mashirika hayo. Na rangi ya mdomo nyekundu na almasi na suruali nyembamba, alijumuisha picha maarufu ya "buchona", shauku ya mapenzi ya narco.Guadalupe Correa-Cabrera wa Chuo Kikuu cha George Mason amefanya utafiti huko Sinaloa, Mexico, ambapo kampuni ya El Chapo inafanya kazi.Anafafanua neno, buchona: "Wanavaa nguo za bei ghali, mikoba ya Louis Vuitton. Kila kitu ni kutia chumvi, na yeye ni uwakilishi kamili wa picha hiyo. Yote ni juu ya sura, upasuaji wa plastiki."Moja ya sifa zake za kushangaza, Correa-Cabrera alibainisha, ni "umbo la mgongo" wake, ambayo aliielezea kama "mbaya sana".Picha yake ya kupendeza ilikuwa tofauti na ukweli mbaya wa shughuli za gari la El Chapo.

Chanzo cha picha, AFP via Getty Image













