Moja kwa moja, Israel yafanya mashambulizi mapya dhidi ya Iran huku Marekani ikiwatambua wanajeshi wake waliouawa

Wanajeshi wanne wa akiba wa Marekani waliuawa Jumapili katika shambulizi la ndege zisizo na rubani nchini Kuwait siku ya moja baada ya Marekani na Israel kuanza mashambulizi dhidi ya Iran.

Moja kwa moja

Na Ambia Hirsi

  1. Uingereza yakodi ndege kuwaondoa raia wake nchini Oman

    Taarifa tulizopokea muda mfupi uliopita zinasema kuwa serikali ya Uingereza imekodisha ndege ya kibiashara kutoka Oman kuwasaidia raia wa Uingereza wanaotaka kuondoka Mashariki ya Kati.

    Ndege inatarajiwa kuondoka mjini Muscat leotarehe 4 Machi saa tano usiku saa za ndani (19:00 GMT), na itawapa kipaumbele watu walio hatarini zaidi.

    Ofisi ya Mambo ya Nje inasema raia wa Uingereza ambao wamejiandikisha kuwa wapo UAE na kwa sasa wako Oman wanapaswa kujaza fomu maalumu haraka iwezekanavyo, ikiwa wangependa kuabiri ndege hiyo.

    Ofisi hiyo aidha imeomba watu kutofika uwanja wa ndege hadi watakapofahamishwa na Ofisi ya Mambo ya nje.

    Inaongeza kuwa itaendelea kushirikiana na mashirika ya ndege kutafuta njia zaidi za kurejea watu nyumbani Uingereza.

  2. Qatar yasema imewakamata washukiwa 10 majasusi wa IRGC

    Shirika la habari la serikali ya Qatar linasema kuwa vikosi vya usalama vya Qatar " vilifanikiwa kukamata seli mbili" zinazofanya kazi katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) mapema Jumatano.

    Saba kati ya washukiwa hao "walipewa jukumu la kijasusi kukusanya taarifa za kijasusi kuhusu miundombinu muhimu ya taifa na kijeshi," shirika la habari linasema.

    Wengine watatu pia waliotumiwa kwa ujasusi "wana uziefu wa kutumia ndege zisizo na rubani", inaongeza.

    "Wakati wa uchunguzi, washukiwa walikiri uhusiano wao na Walinzi wa Mapinduzi ya Irani na kusema kwamba walikuwa wamepewa jukumu la kufanya ujasusi na uasi," shirika la habari la serikali linasema.

    Maelezo zaidi:

  3. Israel yaanzisha wimbi jipya la mashambulizi dhidi ya Iran, IDF inasema

    .

    Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/Shutterstock

    Jeshi la Ulinzi la Israel linasema kuwa limeanza wimbi jipya la mashambulizi dhidi ya Iran.

    "IDF imeanza mashambulizi yanayolenga maeneo ya kufyatulia makombora ya utawala wa kigaidi wa Iran, mifumo ya ulinzi wa anga na miundombinu ya ziada," Jeshi la Ulinzi la Israeli liliandika kwenye mtandao wa wa kijamii wa Telegram.

    Huku hayo yakijiri Jeshi la Marekani limewatambua wanajeshi wanne wa kwanza wa Kimarekani waliouawa katika mashambulizi ya Iran.

    Wanajeshi hao wa Akiba wa Jeshi la Marekani, kutoka Kamandi ya 103 ya Ulinzi ya Des Moines, Iowa, ni pamajo na:

    • Kapteni Cody A. Khork, 35, wa Winter Haven, Florida
    • Sajenti Daraja la kwanza Noah L. Tietjens, 42, wa Bellevue, Nebraska
    • Sajenti wa Daraja la kwanza Nicole M. Amor, 39, wa White Bear Lake, Minnesota
    • Sajenti Declan J. Coady, 20, wa West Des Moines, Iowa

    Wengine wawili waliuawa katika shambulizi la Iran dhidi ya kituo cha kijeshi huko Kuwait siku ya Jumapili, lakini bado hawajatambuliwa.

    Siku ya Jumatatu Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth alisema kwamba ngome ya kijeshi ya Marekani huko Kuwait ilipigwa wakati shambulio la kulipiza kisasi lililofanywa na Iran.

    Vifo hivyo sita pekee ndivyo vilivyothibitishwa na jeshi la Marekani tangu lilipoanzisha mashambulizi dhidi ya Iran kwa ushikiano na Israel.

    Unaweza kusoma:

  4. Natumai hujambo.