Kulipiza kisasi kwa Iran kwazua maswali kuhusu ulinzi wa anga wa Marekani

Chanzo cha picha, Getty Images
Iran imelenga kambi ya Jeshi la Wanamaji la Marekani nchini Bahrain, ikionyesha udhaifu katika ulinzi wa anga, jambo ambalo litaitia wasiwasi Washington na washirika wake katika eneo hilo.
Video zinaonekana kuonyesha makombora na ndege zisizo na rubani zikishambulia karibu na makao makuu ya Marekani ya Fifth Fleet nchini Bahrain.
Bado hakuna ripoti za majeruhi. Wanajeshi wa Marekani wanaweza kuwa walionywa juu ya shambulio hilo na kuchukua tahadhari kuhama..
Tom Sharpe, Kamanda wa zamani wa Jeshi la Wanamaji la Kifalme, anasema Bahrain inaelekea ilionekana na Iran kama shabaha ya hali ya juu ambayo, siku za nyuma, ilikuwa na ulinzi mdogo wa anga.
Hilo sasa linaonekana kuangaziwa na video inayoonyesha ndege isiyo na rubani ya Shahed ya Iran inayosonga polepole ikivunja ulinzi wake.
Huko Ukraine ndege zisizo na rubani kama hizo mara nyingi zinaweza kuangushwa kwa bunduki za kiwango cha kawaida.
Katika kipindi cha wiki chache zilizopita, Marekani inaripotiwa kusafirisha mifumo ya ziada ya ulinzi wa anga katika eneo hilo - ikiwa ni pamoja na THAAD ya kisasa na Mifumo ya Patriot - ambayo inaweza kurusha makombora ya masafa marefu. Lakini hizi ni ghali na ni chache kwa idadi.
Kwa muktadha, Ukraine ina chini ya betri 10 za ulinzi wa anga wa Patriot na bado inajitahidi kutetea mji mkuu, Kyiv.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Bado kuna uwezekano kwamba Marekani ina idadi ya kutosha kulinda kambi zake zote za kijeshi na maslahi yake katika Mashariki ya Kati.
Jeshi la Wanamaji la Marekani pia limetuma karibu dazeni la ndege za kivita aina ya Arleigh Burke kwenye Ghuba na Mashariki ya Mediterania.
Ndege za kivita zinazoshambulia ulinzi wa anga pia zinaweza kurusha droni na makombora ya balestiki.
Tayari ndege hizo zimefanikiwa katika Bahari Nyekundu dhidi ya waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen.
Kati ya 2024 na 2026, Marekani iliharibu karibu ndege zisizo na rubani 400 za Houthi na makombora.
Ndege za kivita za Marekani, ambazo zimetumwa katika eneo hilo, pia zina uwezo wa kunasa ndege zisizo na rubani na makombora. Marekani sasa ina zaidi ya ndege 100 katika eneo hilo.
Lakini hata uwezo huu muhimu hauwezekani kuwa wa kutosha kuzuia Iran kufanikiwa kufikia malengo fulani.
Kabla ya mashambulio haya ya hivi punde zaidi ya Marekani na Israel, Iran bado huenda ilikuwa na takriban makombora 2,000 ya masafa mafupi ya balistiki na ndge nyingi zisizo na rubani ..
Ndege isiyo na rubani ya Shahed ya Iran imesafirishwa hadi Urusi na inaendelea kusababisha maafa kote Ukraine. Urusi sasa inazalisha maelfu ya ndege hizi zisizo na rubani kwa mwezi na kuna uwezekano imeipa Iran usaidizi wa kuendeleza uwezo wake wa kiufundi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Sharpe anasema kwamba wakati wa kipindi chake katika Jeshi la Wanamaji la Kifalme, walifanya zoezi la kijeshi kuiga shambulio la Iran kwenye kambi za kijeshi katika Mashariki ya Kati.
Katika baadhi ya matukio, makombora na ndege zisizo na rubani zingeweza kupitia ulinzi mdogo wa anga.
"Ikiwa Wairani watatoa kila kitu - na kuharakisha mashambulizi yake baada ya serikali kuhisi kutishiwa, basi hatimaye Marekani itaishiwa na mgumo wa kulinga anga wa THAAD na vizuizi vyake vya Patriot," anasema.
Sharpe pia anasema kwamba ndege zisizo na rubani na makombora ya Iran "yametawanywa kwa kiasi kikubwa".
Lakini Edmund Fitton-Brown, mshirika mkuu katika Wakfu wa Ulinzi wa Demokrasia - taasisi ya utafiti yenye makao yake makuu nchini Marekani inayoangazia sera za kigeni - anasema kunaweza kuwa na ushahidi kwamba Wairani, huku wakiwa tayari kulipiza kisasi, huenda hawataki kueneza hili na kuwa mzozo mpana zaidi.
Anasema bado haijafahamika ni kwa kiasi gani mashambulizi ya Marekani na Israel mwaka jana yaliharibu baadhi ya uwezo wa kijeshi wa Iran.
"Dalili za awali ni kwamba ulipizaji kisasi wa Iran umekuwa wa wastani katika wigo," anaongeza.
Inafaa kukumbuka kuwa baada ya mwaka mmoja wa kuwalenga Wahouthi nchini Yemen, Marekani ilikuwa imeharibu lakini haikuharibu uwezo wake wa kurusha makombora na ndege zisizo na rubani.

Chanzo cha picha, Getty Images
Vita vinavyopiganwa kutoka angani peke yake mara chache hupata ushindi mkubwa au mabadiliko ya utawala
Kampeni ya NATO ya kuishambulia Libya mwaka 2011 inaweza kuwa ya kipekee, ingawa katika kesi hiyo machafuko yalifuata.
Iran pia ina uwezo mkubwa wa kushambulia Jeshi la Wanamaji la Marekani - ikiwa liko karibu. Ina hifadhi kubwa ya makombora ya kupambana na meli, pamoja na boti ndogo, zinazoweza kushambulia kwa kasi. Pia kuna swali ambalo halijajibiwa iwapo China inaweza kuwa imeipa Iran msaada wa kijeshi katika kipindi cha miezi michache iliyopita.
Daniel Byman, kutoka Kituo cha Mafunzo ya Kimkakati na Kimataifa chenye makao yake mjini Washington, anasema kwamba mashambulizi ya mapema yanaweza kuharibu uongozi na mali ya kijeshi ya Iran, lakini Marekani "huenda ikajitahidi kuendeleza operesheni wakati njia kuu ya Iran ni kuvumilia".
Ukraine ni ukumbusho wa umuhimu wa ulinzi wa anga. Inaendelea kuwa ombi namba moja kutoka kwa Rais Volodymyr Zelensky kwa washirika.
Ukraine pia inaonyesha jinsi ilivyo vigumu kujilinda dhidi ya mashambulizi mengi yanayohusisha mamia ya ndege zisizo na rubani na makumi ya makombora.
Marekani ina rasilimali zaidi na pamoja na Israel itakuwa ikilenga viwanda vya Iran vya droni na makombora na maeneo ya kurusha makombora.
Lakini kuondoa tishio hilo haitakuwa rahisi. Mgogoro wa muda mrefu hautakuwa changamoto kwa Iran tu, bali pia kwa hifadhi na usambazaji wa silaha za Marekani - katika vita vilivyo mbali na nyumbani.















